1985 - 2007

 

10. Toa Mapepo
Utaijua kweli nayo kweli itakuweka huru

Support Pages   Index To All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Gal 3:1-14 na Mdo 8: 1-25

 Mstari Wa Kukariri
…Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi (1Yoh 3:8).

Baadaye Zungumzieni Juu Ya Jambo Hili
Kwa kile alichokifanya Yesu pale Msalabani; umepokea msamaha, umeokoka, umepona, umepokea uhuru na utajiri. Ikatae kila kazi ya Shetani inayolenga kukuibia baraka hizo.

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Chunguza maisha yako mwenyewe uone kama kuna laana yo yote itokanayo na wakati uliopo au uliopita. Mwendee Mchungaji wako ama waendee wazee wa kanisa au kikundi cha wanamaombi; waeleze hisia zako. Wasihi waombe pamoja nawe. Ungama dhambi zako na za mababu zako, na kwa pamoja mmwombe Mungu aingilie kati. Kumbuka, Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa neema wanyenyekevu.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Kutokana na mifano iliyotolewa, andika taarifa ya kurasa mbili kuonesha jinsi mtu anavyoweza kujilaani mwenyewe.

Tafakari Mistari Hii
Hes 23:19-23

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Mali. Idadi yao ni 10, 000,000; Wasomi ni asilimia10%. Asilimia 86% ni Waislamu; na Wakristo ni asilimia 4% tu, na karibu wote wanaishi kwenye umaskini mkali.

 

Hakikisha umewafundisha wengine somo hili.
Kila mara omba na kujiandaa ukiongezea mistari mingine ya Biblia
na mifano yako mwenyewe ili kufanya somo lieleweke vizuri zaidi.

 

1. Utuokoe Na Yule Mwovu

Katika Wagalatia 3:2-5 tunasoma jinsi Paulo alivyoshangazwa na jambo ambalo halikutarajiwa; yaani kurudi nyuma kwa makanisa ya Galatia. Wagalatia hao si kwamba waliijua kweli peke yake, bali pia walijazwa Roho Mtakatifu na waliona miujiza. Sasa watu hawa walikuwa wanamwacha Bwana, wakiipoteza furaha yao na kuiamini injili ya tofauti. Walikuwa wanarudi nyuma ili waishi kwa kuzitegemea juhudi zao na dini yao, na kuwa na ushirika na watu wageni. Paulo alikabiliana na tatizo hilo katika Gal 4:8-11 na Gal 5:7-12 akiuliza,

" Ni Nani Aliyewaloga Ninyi? "
Maana ya neno kuloga ni kupakazia au kumharibia mtu kwa kumletea sifa za uongo, au kupotosha kwa jicho ovu, matumizi ya hirizi, kuleta nguvu za uchawi juu ya mtu, mvuto mkubwa, au kuongoza mtu kuelekea kwenye mafundisho potofu. Wakati mwingine kuna matatizo katika maisha yetu, katika familia zetu, katika makanisa yetu; ambayo yanatushangaza na ufumbuzi wake unaonekana kuwa mgumu. Iwapo matatizo yanaonekana katika maisha yako, kila mara kumbuka kwamba Mungu anataka kukubariki katika furaha kama vile kukuinua, kukupa afya njema, kukupa watoto, kukufanya mshindi, na kukufanikisha
(Kum 28:1-14).

2. Lakini Je, Kuna Mtu Aliyekuloga Basi?

Dalili za uhakika za mtu aliyelogwa au laana ni mafadhaiko ya muda mrefu ya kushindwa kupokea baraka za Mungu; kuchanganyikiwa na kukutana na kikwazo kikubwa cha maendeleo; na mateso ya uovu wa mara kwa mara kwa mtu binafsi au ni tatizo la kihistoria katika familia. Ukisoma kutoka Kum 28:14-68, utaona dalili zifuatazo:

Hii ni baadhi ya mifano ya kawaida  ambayo si lazima mara zote iwe imetokana na kulogwa, lakini pia kukosa utii mbele za Mungu kwa anayepata mateso hayo.

3. Je, Laana Zinatoka wapi?

Ni matokeo ya dhambi ya asili, kukosa utii na uasi.
Laana ya kazi zisizo na mafanikio (Mwa 3:17) (Mwa 5:29).

Laana ya utoro na kukosa makao duniani (Mwa 4:14).

Laana ya kuwa mtumwa (Mwa 9:25).

Laana ya kuchanganyikiwa (Mwa 11:1-9).

 

Kwa Wafuasi wa Shetani
Laana isiyo na sababu haimpati mtu, lakini kama wakristo watatenda dhambi kwa makusudi, laana inaweza kuwapata (Mit 26:2).

 

Watu Wanaweza Kujilaani Wenyewe Kwa Njia Zifuatazo ~

Uweza wa maneno tutamkayo (Mit 18:21)

Dhambi za kimaadili (Kum 27:20-23)

Kuabudu miungu wengine (Kum 27:15)

Udhalimu (Kum 27:17,18)

Kutukana wazazi (Kum 27:16)

Uzembe na kukosa uaminifu katika kazi ya Mungu (Yer 48:10)

Kumtumainia mwanadamu (Yer 17:5)

Kutokuwajali maskini (Mit 28:27)

Kumwibia Mungu (Mal 3:9)

Nakadhalika.

 

Watu Wanaweza Kuwalaani Wengine

Kwa kutumia mamlaka, matusi, kwa kufanya maombi kwa miungu wengine, au pengine wahenga wetu walilaaniwa.

Uhuru kutokana na laana unaweza kupatikana tu kwa Yesu anayebadilishana laana zetu na baraka za Mungu (Gal 3:13-16).

4. Mabadilishano Ya Kimbingu Yalifanyika Msalabani

Alisulibiwa  kwa maovu yetu.

Alipigwa kwa makosa yetu.

Aliadhibiwa ili sisi tupate amani.

Alijeruhiwa Yeye ili sisi tupate kupona.

(Isa 53) (1 Pet 2:24).

 

Alichukua dhambi zetu ili sisi tuhesabiwe haki.

Alikubali kufa ili sisi tupokee uzima wa milele.

Alikuwa maskini ili sisi tuweze kuwa matajiri.

Alikataliwa ili sisi tukubalike.

(2 Kor 5:2) (Ebr 2:9) (Rum 6:23)

(2 Kor 8:9) (Efe 1: 5,6).

 

Badala Ya Laana, Baraka Nyingi.

Badala ya kazi isiyokuwa na malipo, katika Yesu kazi yetu si bure (1 Kor 15:58)

Badala ya kutangatanga, tunakwenda kwa malengo (Mt 28:19)

Badala ya utumwa, tunao wito mkuu wa utumishi (Flp 2:6).

Badala ya kutawanywa, tunaweza kuunganishwa ulimwengu mzima kwa uweza (Mwa 11:6). Na badala ya kuchanganyikiwa, tunayo baraka ya Ibrahimu kwa mataifa yote (Mwa 12:1-3).

 

Je, Ibrahimu Alibarikiwaje?

Ibrahimu alibarikiwa kwa kila namna.

Sisi nasi tumebarikiwa kwa ahadi ya Roho Mtakatifu ili kututia nguvu na kutuwezesha kulitimiza kusudi la Mungu kwa mataifa (Mwa 24:1) (Mdo 1:8)

5. Hatua Saba Za Kuondokana Na Laana

Ulozi ni kazi ya mapepo wachafu wanaofuata maelekezo ya wanadamu na maombi maovu; lakini hebu soma 1 Yoh 4:4 na 1Yoh 3:8. Maombi katika Jina la Yesu na mamlaka yake huvunja nguvu zote za uovu. Waombe ndugu na dada zako katika Kristo, ambao unawaamini na wao wanakupenda , waombe pamoja nawe kama ifuatavyo ~

  1. Tambua kwamba sababu ya tatizo lako ni katika ulimwengu wa kiroho.
  2. Tubu  na kuacha dhambi zilizosababisha tatizo hilo kujitokeza, na kwa msaada wa Mungu chagua kumfuata Yesu awe Bwana na Mwokozi wako.
  3. Pokea msamaha kwa Jina la Yesu, na kwa Jina la Yesu msamehe kila aliyekutendea mabaya na kukuumiza.
  4. Mkatae Shetani na kazi zake zote.
  5. Mkumbushe Shetani kuhusu damu ya Yesu na jinsi alivyoshindwa pale Msalabani. 
  6. Waombe rafiki zako wakemee kila kazi ovu, wakiamuru nguvu zote ovu ziondoke, na kila laana ivunjike kwa Jina la Yesu.
  7. Jaza tena maisha yako na Roho Mtakatifu wa Mungu na siku zote umtukuze Yesu, ukiendelea kuishi katika Roho na katika Neno la Mungu.


Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu
Huu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili; Wataje Kwa Majina
 
 

Brunei

Jina La Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Bajau 

Bajau

10,000







 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index To All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk