1985 - 2007

 

15. Ahadi Ya Mungu Katika Umisheni

Kama ukifuata nyayo za Ibrahimu, basi utahitaji Pasi ya kusafiria nje ya nchi

Support Pages   Index To All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Mwa 11:26-12:5;  Gal 3:6-29

Mstari Wa Kukariri
Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi (Gal 3:28,29)

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, unafikiri ahadi saba zinaweza kuwa na maana gani katika maisha yenu kama ungeweza kuziamini na kuzifanyia kazi?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Ziandike hizo ahadi saba kwa herufi kubwa katika kipande cha karatasi ngumu, kisha ibandike ukutani au mahali unapoweza kuiona kirahisi. Kila unapowaza kuhusu ahadi hizo, zitafakari, rudia tena, zikiri kwa imani, na kisha pokea baraka.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Ona anachosema Petro katika 1 Pet 2:9 na kisha andika maelezo ya kurasa mbili; ujumbe huo unaweza kuwa na maana gani kwa watu wa Mungu hivi leo?

Tafakari Mistari Hii
Ebr 11:8-10

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Botswana  

Idadi ya watu: 1,500,000.  Wakristo ni wengi, na ambao hawajafikiwa pia ni wengi.

 

Zamani za kale, kijana Abramu alikuwa anaishi katika mji wa zamani uitwao Uri, na familia yao waliabudu vinyago (Mdo 7:2,3) (Mwa 11:31) (Yos 24:2). Siku moja  Mungu wa kweli na aliye hai aliamua, na kwa sababu zake mwenyewe, kuzungumza na Abramu akisema,

" …toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonesha…” (Mwa 12:1)

Mungu anafanya kazi, na familia ya Abramu inaondoka pamoja na Lutu, kuelekea Kanaani. Hatimaye baba yake Abramu, Tera, alikufa na Mungu akamjia tena Abramu ili kumkumbusha yale aliyokuwa amemwambia alipokuwa angali mjini Uri.

Safari Hii Mungu Anaongeza Ahadi Saba -

Nitakufanya taifa kubwa,

Nitakubariki,

Nitalikuza jina lako,

Wewe utakuwa baraka,

Nitawabariki wanaokubariki,

Nitawalaani wanaokulaani,

Na watu wote wa dunia watabarikiwa kupitia kwako.

Baadaye Mungu anaeleza kwamba uzao wa Abramu utakuwa kama mchanga, na kama nyota za mbinguni. Mungu akabadilisha jina la Abramu na kumwita Ibrahimu, likiwa na maana ya baba wa mataifa mengi; kwahiyo Ibrahimu husikia ahadi hiyo ikitamkwa kwake kila mara. Na ingawa Ibrahimu alibarikiwa sana, lakini hatuwezi kusema kwamba ahadi zote hizo zilitimia katika uhai wake. Sasa ilikuwaje? Soma Mwa 13:14; 15:5; 17:1-7 na 24:1.

Ahadi Inamjia Isaka

Isaka ni mtu anayependa kukaa nyumbani, si kama baba yake Ibrahimu. Mungu anamtokea na kuja na ahadi zilezile, lakini hata mpaka siku Isaka anafikia mwisho wa maisha yake yaliyokuwa na baraka nyingi, ahadi zote zilikuwa bado hazijatimizwa. Soma Mwa 26:4.

Sasa Tuje Kwa Yakobo, Mjukuu Wa Ibrahimu

Yakobo ni tapeli, si kama baba yake Isaka wala babu yake Ibrahimu. Siku moja  wakati anakimbia kuokoa maisha yake, Mungu anakutana naye na mara anagundua kwamba kumbe hata yeye ni mrithi wa zile ahadi. Soma Mwa 28:14.  Baadaye baada ya kupata mateso mengi, Mungu anabadilisha jina la Yakobo na kumwita Israeli.

Kutoka Yakobo hadi Yusufu

Watoto wa Yakobo walikuwa na chuki na ndugu yao Yusufu na mwishowe walimwuza utumwani Misri. Miaka mingi baadaye alipata madaraka na kuokoa maisha ya familia yake. Ahadi inaambatana nao hadi Misri ( Soma Mwanzo 42 hadi 47). Miaka mingi ilipita na Yusufu alipokufa nyumba ya Yakobo ilidhiliwa, ikapata mateso na hatimaye ikaingia utumwani.

Sasa Ikawaje Kuhusu Ahadi?
Miaka 400 ilipita nao wakamlilia Mungu. Na ili kujua kwa undani kilichofuata baada ya hapo soma kitabu cha Kutoka mlango wa 1 hadi wa 12. Watu wa Mungu wanaondoka Misri kwa ukombozi wa nguvu wakielekea Kanaani kupitia Bahari ya Shamu. Mungu hajasahau ahadi yake hata mara moja, na walipofika Mlima Sinai alirudia kuzitaja ahadi hizo na hata kuzikuza kwa ajili ya nyumba ya Yakobo, akisema ~

 

Ninyi mtakuwa watu wangu wa thamani;

Ninyi mtakuwa ufalme wa makuhani;

Ninyi mtakuwa taifa takatifu;

 

Nyumba ya Yakobo waliposikia na kujua kwamba kazi yao ni kupeleka baraka za Mungu ulimwenguni kote, walisema, ‘Ndiyo’; lakini waliposikia kuhusu mtindo wa maisha unaotazamiwa kutoka kwao kama taifa takatifu,

 

Walikataa,

Walikataa kumtolea Mungu,

Walimkataa Mungu,

Mioyoni mwao walirudi Misri.

Matokeo yake kulikuwa miaka 1500 ya utupu wa kidini mpaka Yesu alipokuja. 
( Kut 19:4-19) (Ebr 12:19) (Mdo 7:39,42)

3. Je, Inakuwaje Neno La Mungu Linapokaa Bila Kutimizwa?

Wakati Yoshua alipouharibu mji wa Yeriko, Mungu alimtaka atamke laana kwa ye yote atakayethubutu kuujenga tena mji huo. Miaka mingi baadaye mtu mmoja aliujenga Yeriko lakini kwa gharama ya watoto wake sawasawa na neno la Mungu lililokuwa limetamkwa juu ya mji huo kupitia kinywa cha Yoshua. Neno la Bwana halitamrudia kamwe  hata limetimiliza  kusudi la Mungu la kulituma neno hilo. Ndiyo kusema litasubiri mpaka limpate mtu ambaye neno hilo litatimilizwa kupitia kwake (Yos 6:26) (1 Fal 16:34) (Isa 55:11).

4. Ni Nini Kimetokea Kwa Ile Ahadi?

Paulo anaeleza kila kitu katika Gal 3:8-29. Katika mstari wa 8 na wa 9 tunaona kwamba ile ahadi kwa kweli ni unabii wa Injili ya wokovu kwa imani kwa sababu mataifa yote watabarikiwa kupitia kwa Ibrahimu aliye baba wa imani yetu.

Halafu katika mstari wa 16 tunaona kwamba ahadi hiyo inasubiri mbegu au mtu fulani.

Hiyo Ahadi Kwa Kweli Ni Ya Yesu

Sasa soma tena kwa sauti zile ahadi saba, na safari hii litangulize jina la Yesu, ukisema,

Yesu, nitakufanya wewe kuwa. . .

Ahadi Ile Ni Kwa Ajili Ya Kanisa Pia
kwa sababu kama usemavyo mstari wa 29, ninyi ni wa Kristo, na kama mwili wa Kristo mmekuwa warithi wa ahadi zote saba. Na sasa rudia tena kusoma kwa sauti zile ahadi saba, na safari hii tanguliza jina la kanisa lako au misheni yako na usikie Mungu akinena nawe.

Kanisa, nitakufanya wewe kuwa . . . 

Rudia tena na tena hadi ukweli huu umekolea nafsini mwako.

4. Je, Hii Ina Maana Gani Kwetu?

Maana yake ni kwamba kwa imani sasa unaweza kwenda kwenye nchi yo yote  Mungu atakayokuonesha, huku ukijua kwamba ipo ahadi ya siku nyingi kutoka kwa Mungu nayo inakusubiri wewe uirithi kwa kutii kwako. Maandiko yanasema kwamba wewe ni mrithi wa ulimwengu na kwamba ahadi inahakikishwa kwa imani na kwa neema. Mungu pia ametufanya sisi kuwa kile Israeli walichokataa kuwa (Rum 4:13,16) (1Pet 2:9,10).

 

Kwa Kumalizia Omba kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

 

China

Jina la Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Baheng, Sanjiang

Baheng, Sanjiang

29,000

Baonuo

Bunu, Naogelao

25,000

Beidalao

Beidalao

15,000

Bunuo

Bunu, Bunuo

20,000

Chrame

Chrame

39,000

Dongnu

Bunu, Dongnu

160,000


  






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk