1985 - 2007

 

16. Kumaliza Kazi

Nguvu za vikundi mbalimbali kanisani huachia uweza wa Mungu

Support Pages   Index To All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma Haya
Mdo 16:6-15;  1The 1:4-10

Mstari Wa Kukariri
“…bali tukiwa na tumaini kwamba, imani yenu ikuapo, tutakuzwa kwenu kwa kadiri ya kipimo chetu, na kupata ziada;  hata kuihubiri Injili katika nchi zilizo mbele kupita nchi zenu…” (2Kor 10:15,16).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, jambo hili linaweza kufanyika kanisani kwako au makanisa mengine unayoyafahamu? Kama jibu ni Hapana, ni kwanini?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Fikiria kuhusu vikundi mbalimbali na uone ni nani unaowafahamu ambao wanaweza kufaa katika kila eneo. Je, unaweza kuona watu ambao vikundi vinaweza kuwalenga katika maombi na huduma yao; hao ni akina nani na wako wapi?

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Angalia tena orodha ya vikundi halafu andika mawazo mengine, pengine yaliyo bora zaidi na yanayofaa kwa vikundi katika taifa lako, mazingira na utamaduni wako.

Tafakari Mistari Hii
Mdo 6:3,4

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Peru

Idadi ya watu: 25, 000,000 ; 89% ni Wakatoliki; Kanisa la Kiinjili nalo linakua kwa kasi

 

 

1. Rejea Upesi, Bwana Yesu

Watu kila mahali wanasubiri kwa hamu kurudi kwa Yesu, na atarudi wakati ambapo Injili ya Ufalme itakuwa imehubiriwa  kwa mataifa yote ya ulimwengu. Sasa tupo karibu zaidi na kurejea kwake kuliko ilivyowahi kuwa, na huu ni muda mzuri zaidi kwa kanisa kuvuka mipaka yake kwa ajili ya kuwafikia wale ambao hawajafikiwa.

2. Kukamilisha Kazi

Wataalamu wa mambo ya umisheni wameorodhesha mikakati muhimu 12 ambayo kila kanisa linaweza kuifanyia kazi ili kuweza kutimiliza Agizo Kuu. Orodha hiyo inaanza na lile lililo jepesi zaidi na kumalizia na lile lililo gumu zaidi.

  1. Maombezi na vita vya kiroho.
  2. Kuwa na mtandao na Kanisa la Ulimwengu mzima.
  3. Uwazi mpya wa matumizi ya karama za Roho katika umisheni.
  4. Kurejesha hali ya uharaka ndani ya kanisa.
  5. Kupanua wigo wa uinjilisti hadi ng’ambo ya mipaka ya kijiografia na ya kitamaduni.
  6. Kuoanisha kazi za kijamii na kuhubiri Injili.
  7. Kuwafikia wana wa ulimwengu.
  8. Kuwafikia wanawake wa ulimwengu ambao wamefungwa na desturi za kidini.
  9. Kuifikia miji mikuu ya ulimwengu.
  10. Waendee viongozi wa makanisa maskini ili kuwasaidia; waandae na kuwategemeza.
  11. Wafikie wale watu ambao hawajafikiwa.
  12. Wahubirie tena Injili wale waliohubiriwa kwanza.

Kwa Mchungaji orodha hii inaweza kuwa na maana kwamba afanye kazi zaidi, wakati hata muda uliopo kwa sasa haumtoshi. Mweka Hazina naye anaweza kuwa na wasiwasi kwa sababu huduma hii inaonekana kuwa ya gharama kubwa , na fedha alizo nazo hazitoshi. Kwa upande mwingine watu wengi wanapata msisimko wanaposikia habari za kwenda ng’ambo kuhubiri Injili lakini hawajui wafanyeje. Je, jawabu ni nini?

3. Vikundi Vinaweza Kuachilia Uwezo Wa Watu

Huduma ya vikundi inaweza kulisaidia kanisa lako kusonga mbele na kufanya huduma ulimwenguni bila kumtwisha mzigo mkubwa mchungaji, au kumwumiza kichwa mweka hazina.

Je, Huduma ya Vikundi Ni Nini?
Huduma ya vikundi inafanyika wakati washirika kati ya 5 na 15 wanapokutana na kutaka kufanya jambo watakalochagua wenyewe kwa ajili ya umisheni. Mchungaji atawaandaa kwa habari ya mahusiano kati yao na yeye, na baina yao wenyewe. Atateua kiongozi wa kila kikundi, na mzee wa kanisa kuwa mwangalizi. Wanakikundi wataomba, watazungumza, na kisha watawasilisha kwa mchungaji malengo na mipango yao.

Ni Nani Atakayelipia Gharama?
Kila kikundi kinapaswa kuchanga fedha zake chenyewe kwa imani na kufanya kazi. Anachopaswa kufanya mchungaji ni kuwaruhusu waendelee. Hana kazi nyingine ya ziada mbali na kuwatia moyo, kuwasikiliza, na kukagua maendeleo yao kila baada ya miezi sita. Kuachiliwa kwa nguvu kunaweza kukawa kukubwa na kufanya malengo ya kanisa kufanikiwa sana katika kuombea umisheni, kutoa kwa ajili ya umisheni, kwenda na kutuma watu wengine katika huduma ya umisheni.

4. Ni Aina Gani Za Vikundi?

Hebu tuwaze kikubwa na kupendekeza mawazo yafuatayo. Tutachukua orodha ya mkakati na kuanza na yale yaliyo rahisi kuliko yote ambapo kila mtu anaweza kushiriki; na kisha tutamalizia na yale yaliyo magumu kushinda yote.

Pengine mwanzoni kutajitoteza kikundi kimoja au viwili, lakini Mungu atasababisha ukuaji kwa jinsi watu watakavyoelewa maono na kutaka kujiunga.

  1. Wale wanaotaka kuomba kwa ajili ya mataifa, kwa ajili ya wamishenari, kwa ajili ya kanisa la ulimwengu wote - na hasa makanisa yanayoteseka, wanaweza kukutana mara moja kwa wiki.
  2. Kwa wale wanaopenda kuandika, wafanye hivyo ili waliunganishe kanisa lako na makanisa mengine ulimwenguni mwote. Utapokea watumishi watakaokuja kukutembelea, na pengine Mungu anaweza kufungua milango kwa ajili yako ukapata fursa ya kuwatembelea wengine na kujifunza kutoka kwao.
  3. Wale wanaotabiri au wenye kuona maono wawemo katika huduma wakipokea maneno ya maelekezo kwa misheni, kwa wamishenari, na safari zao.
  4. Hao wenye kuliongoza kanisa wawe na kikundi chao na waongoze kwa mfano (Isa 54:2-5).
  5. Hao wenye kuimba wajiandae na kulifanya kanisa lote lijue upana wa ulimwengu wa Mungu na wito wa misheni.
  6. Hao wanaotaka kuwafikia watu wa tamaduni nyingine wakutane na wageni waishio ndani ya nchi ili wagundue mambo na kujifunza kutoka kwao jinsi wanavyoupokea ujumbe wa injili.
  7. Kwa wale wapendao kazi za mitaani waweke mpango wa kutembelea mji mkubwa ulioko jirani ambako mamilioni ya watu wamenaswa kwenye uhalifu, madawa ya kulevya, na ukahaba. Wanapaswa kuitafuta miji mikuu ya dunia na kuwasiliana na waamini walioko huko na ambao bila shaka watahitaji msaada.
  8. Na hao wanaowapenda maskini wafanye mipango ya kuwafikia wenye njaa, walio uchi, na wagonjwa, na hasa wanawake na yatima. Tafuta uone ni nani wanaweza kusaidia kwa sababu shughuli kubwa kama hii inahitaji kufanyika kwa ubia.
  9. Na kwa wale wanaolia kwa ajili ya watoto waliosahaulika ulimwenguni mwote wafanye mipango ya kuwafikia watoto hao kwa upendo wakiwa na chakula, mavazi, na ada ya shule.
  10. Na hao wanaohisi kwamba wameitwa kuwaendea watu ambao bado hawajafikiwa, wawe wako jirani au mbali, wafanye mipango ya kupeleka timu za watenda kazi. Zingatia maeneo, gharama, lugha, mafunzo na usafiri. Usisahau kwamba Ulaya, kiroho ni bara lililoko kwenye giza kuu kuliko mabara yote hapa duniani. Hao wenye kujua lugha wasaidie timu za kimisheni.
  11. Wale wenye karama na neema ya kupata fedha waone jinsi wanavyoweza  kutumia fedha zao kufadhili umisheni na wamishenari.
  12. Na wale wanaoifahamu Biblia wafanye mpango wa kuwatembelea waamini wenye njaa ya kweli ya kuyajua Maandiko, na ambao hawana Biblia wala mchungaji wa kuwafundisha. Wapo maelfu kwa maelfu ya wachungaji hapa ulimwenguni ambao ni kama hawajui cho chote kwenye Biblia.

Lililo bora kuliko yote ni kugundua kwamba Mungu yupo pamoja nawe kwa namna mpya. Usiogope kumwomba msaada, au kuingia ubia na makanisa au misheni nyingine ambazo zinaweza kukusaidia kushiriki katika huduma ya ulimwengu.

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili Ya Yesu Kristo

 

 

China

Jina la Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

E (Kjang E)

E

30,000

Jiamao

Jiamao

52,300

Kang

Kang

37,000

Mahei (Mahe, Mabe)

Mahei

12,000

Malu (Lansu, Diso)

Maru

13,000

Man Cao Lan

Man Cao Lan

72,000






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk