1985 - 2007

 

17. Watu Wasiofikiwa Bado

Katika dirisha la ‘10/40’ maskini ndio waliopotea na waliopotea ndio maskini kuliko wote

Support Pages   Index To All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Kitabu cha Yona

Mstari Wa Kukariri
Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja (Mt 24:14).

Baadaye Zungumzieni Kuhusu Jambo Hili
Je, unaishi wapi? Ni katika ulimwengu upi A, B au C?
Kwanini unafikiria hivyo. Hebu yafikirie mataifa mengine yaliyoko barani mwako, yapo katika ulimwengu upi?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Chukua kipande kigumu cha karatasi, kwa mfano kasha; halafu chora ramani ya dunia na kisha ongezea dirisha la ‘10/40’ na uandike majina ya mataifa ndani yake. Itundike karatasi hiyo mahali unapoweza kuiona kirahisi. Weka alama ya vema kwenye kila taifa ukiisha kuwaombea watu wake.

Kazi Ya Kuandika ya Stashahada
Kwa kutumia atlasi andika orodha ya mataifa mengi kadiri uwezavyo kwenye dirisha la 10/40. mbele ya kila jina andika dini kubwa katika taifa hilo na siasa zake.

Tafakari Mistari Ifuatayo Neno Kwa Neno
Isa 54:2-5

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Omba kwa ajili ya Wachina (Ethnos).  

Idadi yao ni karibu 1,000,000,000; Hawajasikia Injili.

 

Katika Mt 28:19 tunaagizwa kwenda kuwafanya mataifa yote (ethnos) kuwa wanafunzi. Neno ethnos lina maana ya makundi ya watu wanaoletwa pamoja kwa historia yao, lugha, na  utamaduni wao.

Kwa mujibu wa Mdo 1: 8 kuna maeneo matatu ambako tunapaswa kwenda kufanya kazi.

Yerusalemu, ikiwa na maana ya eneo la nyumbani ambako kuna watu tunaofanana nao kwa lugha, na hata mazingira yake tunayafahamu vizuri.

Yudea na Samaria, ni jirani tu na kwetu, na watu wenyewe tunafanana, ingawa tunaweza kuwa tumetofautiana kidogo utamaduni wetu na lugha. Hapa pia kunaweza kukawepo namna fulani ya ubaguzi.

Miisho Ya Nchi, huko watu ni tofauti kabisa; utamaduni wao, lugha yao, dini yao, mtindo wa maisha, na hata hali ya hewa ni tofauti kabisa.

Lengo ni kufanya kazi katika maeneo yote matatu kwa wakati mmoja.  Ni wazi kwamba tunaweza kufanya vizuri zaidi katika Yerusalemu yetu kwa sababu tupo watenda kazi wa kutosha, vitendea kazi na fedha. Uwezo wetu unaweza ukapungua kidogo kadiri tunavyotoka nje ya mipaka ya Yerusalemu yetu kuelekea Yudea, Samaria; na kwenye Miisho ya Nchi, uwezo wetu unaweza ukapungua zaidi.

Wengine wanadhani kwamba tunapaswa kuhakikisha kuwa Yerusalemu yetu inakuwa ya Wakristo watupu kabla hatujahamia Yudea na Samaria na hatimaye Miisho ya Nchi! Haipaswi kuwa hivyo; ingekuwa hivyo, ungekuta hata leo kanisa bado lipo katika jiji la Yerusalemu.(Inasemekana kwamba jiji la Yerusalemu ni moja ya miji ambapo Injili inakataliwa sana hapa duniani).

1. Tuuangalie Ulimwengu Huu Kwa Mtazamo Mpya

Tunaweza kuugawa ulimwengu huu katika makundi matatu:

Kundi A, ni ulimwengu wenye watu wengi sana ambao hawajafikiwa bado!
Kundi B, ni ulimwengu ambamo  wenye dhambi wengi wanaishi na wakristo ambao ni chumvi na nuru yao.
Kundi C, ni ulimwengu uliojaa wakristo kwa wingi, washuhudiaji kwa wingi, na vitendea kazi pia.

2. Kundi A Ni Ulimwengu Ambao Haujafikiwa Na Injili

Ukristo katika maeneo hayo ni kati ya 0 – 0.05%. Mifano: Afghanistan, Syria, Maldives, Sahara Magharibi, Korea Kaskazini, Djibouti, Uzbekistan.

Dirisha la 10/40
Wakati mwingine watu wanapenda kuita ulimwengu wa Kundi A dirisha la 10/40 kwa sababu kijiografia ni eneo lililo kati ya longitudi 10 na 40 Kaskazini ya Ikweta; na kuenea kuanzia Afrika Magharibi hadi Japan. Katika dirisha hilo ndiko waliko wengi wa watu waliopotea na maskini wakubwa wa dunia.

Barabara Ya Hariri
Kunako dirisha la 10/40 ndiko pia palipokuwa na ile Barabara ya Hariri ambayo mwaka 1000 KK ilikuwa imeliunganisha bara la Ulaya na Mashariki ya Mbali. Na kwenye barabara hiyo ndiko matukio yote ya Biblia yalikotokea; ustaarabu wa kale sana ulitokea humo; dini kuu kama dini ya Kihindu, ya Kibudha, na ya Kikristo zilisafiri kwenye barabara hiyo pamoja na wafanyabiashara. Ya mwisho ni Uislamu ulioenezwa kwa kutumia nguvu, na hii ndiyo sababu ya upinzani mkubwa dhidi ya Injili uliopo katika eneo hilo leo hii. Wengi wa maskini wa dunia hii wanaishi kwenye barabara hiyo ya hariri, na hii si kwa bahati tu. Wengi wanaamini kwamba Barabara Ya Hariri itakuwa pia njia itakayotumiwa na wamishenari wengi wa Kichina wakirejesha Injili Galilaya.

3. Je, Unaufikiaje Ulimwengu wa Kundi ‘A’?

Ijapokuwa ni mbali na makanisa ya Magharibi, lakini Mungu amepanda makanisa mapya mengi katika maeneo yaliyo jirani sana na hawa watu ambao hawajafikiwa. Kwa mtu wa Magharibi, umisheni kwa watu wasiofikiwa bado kunadai miaka ya kujifunza, lugha na kuzoea mazingira. Lakini kwa mwamini Mhindi, au Mchina, au Mwafrika, hawa watu ambao hawajafikiwa ni majirani na pengine hata utamaduni na lugha zao zinafanana.

Moja ya mambo mazuri yanayoweza kufanywa na makanisa ya Magharibi ni kuyasaidia makanisa katika nchi zinazoendelea ulimwenguni kote; na jambo zuri linaloweza kufanywa na kanisa katika nchi zinazoendelea ni kuwa na maono ya umisheni, kutenda kazi kwa ubia na kanisa au misheni ya Magharibi, na kutuma wamishenari wake.

4. Ulimwengu Wa Kundi ‘B’ Umefikiwa Na Injili Lakini Waliofanyika Wanafunzi Bado Ni Wachache

Hao ni kiasi cha 41% ya ulimwengu pale ambapo washuhudiaji wamejikita kwa miaka mingi. Mifano: India, Cuba, Myanmar, Syria, Indonesia, Chad, na Nigeria. Katika nchi hizo watu waliookoka wanaishi na watu wasiookoka na hivyo kuwafikia inakuwa ni rahisi.

5. Ulimwengu Wa Kundi ’C’ Ni  Wetu Wakristo

Sisi ni aslimia 33% ya ulimwengu wote na mataifa yetu yanamiliki sehemu kubwa ya utajiri wa dunia. Kundi ‘C’ ni nchi kama Uingereza, Guatemala, Brazili, Australia, Kenya, Norway, Marekani, na Canada. Tatizo ni kwamba Wakristo walioko katika kundi ‘C’ hawatilii maanani wajibu wao wa kuwaendea hata watu wa kundi ‘B’ ambao hawajafikiwa ukiachilia mbali watu wa kundi ‘A’.

Inakadiriwa Kwamba Katika Kila Watu Kumi Wanaoishi Leo
Wanne ni wa ulimwengu wa Kundi A…Hawajafikiwa

Watatu ni wa ulimwengu wa Kundi B…Wanaishi jirani na Wakristo

Watatu ni wa ulimwengu wa Kundi C…Hawa ni Wakristo

Ni nani katika Kundi C aliye tayari kuomba, kutoa fedha au mali, au kwenda kwa kundi B, au kwa Kundi A lenye mataifa 1,700 ya watu ambao hawajafikiwa? Katika hao 1,700 kila taifa lina watu 10,000 na zaidi. Yapo pia mataifa mengi yenye watu wachache zaidi. Safari kutoka Kundi C kwenda Kundi B au Kundi A kwa maombi au kwa namna nyingine yo yote ndiyo njia pekee ya kuwafikia mataifa hao. Je, unaweza kuona uhusiano wo wote kati ya mataifa hawa na kurudi kwa Yesu? (Angalia Mstari  wa Kukariri Hapo juu).

6. Kuwafikia Wasiofikiwa Bado

Makanisa katika nchi zinazoendelea wana watenda kazi na utayari wa kuwaendea wale ambao hawajafikiwa. Wanachopungukiwa ni mafunzo na fedha. Hapa zipo njia anazoweza kutumia mwamini katika nchi zinazoendelea akawa mmishenari bila kuhitaji fedha nyingi sana:

Serikali nyingi, kama China na Libya huwafadhili wanafunzi wageni kwenda kusoma katika vyuo vikuu nchini mwao. Watumishi wa ndani wanaweza pia kuwa wamishenari wazuri huko Mashariki ya Kati.Wafanyabiashara wanaweza kufanya biashara za kimataifa. Wakimbizi wanaweza kusambaa na Injili. Ukipata fursa, nenda! Jifunze Kiingereza, au jipatie maarifa ya kompyuta, na ulimwengu unafunguka.Watamfundisha mtaalamu, bali wao watampokea mmishenari.

 

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Ambao Bado Hawajafikiwa na Injili Ya Yesu Kristo

 

China

Jina la Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Miao, Guiyang Northern

Miao, Guiyang Northern

84,000

Miao, Guiyang Southern

Miao, Guiyang Southern

28,000

Miao, Guiyang Southwestern

Miao, Guiyang Southwestern

70,000

Miao, Huishui Central

Miao, Huishui Central

40,000

Miao, Huishui Eastern

Miao, Huishui Eastern

14,000

Miao, Huishui Northern

Miao, Huishui Northern

70,000






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk