1985 - 2007
18. Kuwafikia Wasiofikiwa Bado
Watu wa mwisho kabisa ambao hawajafikiwa ni wale wanaozuiwa na siasa au dini
Support Pages
Index To All Lessons
School of Finances
World Christian News
Who
Are We?
Site Index
Katika Biblia Yako Soma
Zaburi 139;
Mithali 8.
Mstari wa Kukariri
Panua mahali pa hema yako, na
wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako;
vikaze vigingi vya hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa
kushoto; na wazao wako watamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa
kukaliwa na watu (Isa 54:2, 3).
Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Tazama ramani ya watu wasiofikiwa
bado ili kuona mahali walipo. Je, ni akina nani hao? Je, wako jirani au mbali
nawe? Je, bila fedha unaweza kuwaendea au la?
Jambo la Kufanya Kabla Hatujakutana
Tena
Zungumza na mchungaji wako au
wazee wa kanisa kuhusu uwezekano wa kanisa lenu kuanzisha utaratibu wa kuombea
kundi la watu ambao hawajafikiwa bado, kufanya utafiti na pengine kwa neema ya
Mungu watu hao waweze kufikiwa na timu kutoka kanisani kwenu.
Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Fikiria kwamba unaishi katikati ya
kundi la watu ambao bado hawajafikiwa. Wewe ni nani, na unaamini nini? Hofu yako
kubwa ni nini? Andika kurasa mbili.
Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Yer 8:20
Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Tajikistan
Idadi ya watu: 6,300,000
Waislamu ni 82% ; Kuna Wakristo wachache tu; Na watu wengi hawajafikiwa.
Fanya Rejea Ya Masomo Yafuatayo
16. Kumaliza Kazi
Kuliandaa kanisa kwa ajili ya Agizo Kuu, kufungua maudhui ya mataifa ambayo
hayajafikiwa.
17. Watu Wasiofikiwa Bado
Jinsi ulimwengu unavyoonekana, kwa mtazamo wa kimbingu.
74. Kanisa La Kimishenari
Kuuingia ulimwengu wa umisheni, na namna ya kuanza.
Pengine ni mara ya kwanza umewezeshwa kuelewa kuhusu mataifa ambayo hayajafikiwa; na hapa mataifa ina maana ya makundi ya watu waliounganishwa na lugha moja, historia moja, au utamaduni mmoja. Unajua kwamba Yesu hawezi kurudi mpaka haya mataifa yawe na kanisa la kitaifa linaloweza kushuhudia watu wake, hata kama kanisa hilo ni dogo kiasi gani!
Kwa Hao Waliopewa Vingi,
Kwao Vitadaiwa Vingi
Haya ni maneno ya Yesu katika Lk
12:48.
Kanisa La Magharibi
Limepewa Vingi
Kwa sababu kanisa katika nchi za
Magharibi limepewa vingi kwa maana ya nuru, maono, na mali, vingi vitadaiwa
kutoka kwao. Si mpango wa Mungu kwamba waamini waingie katika maisha ya starehe
kabla watu wa ulimwengu wote hawajapata fursa ya kusikia habari za upendo wa
Mungu na wokovu.
Makanisa Ya Karismatiki Ni
Zaidi
Kwa kuwa makanisa haya yamepokea
vingi kwa maana ya uwepo wa Roho Mtakatifu na karama zake, vingi vitadaiwa
kutoka kwao. Si mpango kamili wa Mungu kwamba waamini na wachungaji wao watumie
muda mrefu daima wakiogelea katika upako wa Roho Mtakatifu, baraka na karama
zake, kwa manufaa binafsi tu wakati sehemu tu ya huu uweza wa Roho ukitumiwa kwa
usahihi unaweza kupeleka injili kwa watu wasiofikiwa bado na ambao wanaweza
wakapotea milele.
Viongozi Wa Kanisa Wamepewa
Vingi Zaidi
Kwa vile viongozi wa makanisa ya
nchi za Magharibi na katika ukanda wa uamsho ulimwenguni kote wamepewa watu
wengi na fedha, Bwana atadai vingi kutoka kwao. Kamwe si mpango mkamilifu wa
Mungu kwamba nguvu nyingi itumike katika mashindano baina ya makanisa katika
kujenga mahekalu makubwamakubwa na makundi makubwa ya wakristo wa majina
wanaovutwa na vipindi vya burudani, wakati wanaume na wanawake wanaendelea
kuangamia milele kwa kukosa kuisikia injili angalao mara moja.
Kwahiyo kwa sehemu kubwa , ni makanisa ya Magharibi na yale ya karismatiki na viongozi wao ndio wenye wajibu mkubwa wa kuwezesha kukamilika kwa Agizo Kuu katika kizazi chetu. Ingawa kazi kubwa inaweza kufanywa kwa uzuri zaidi na makanisa ya nchi zinazoendelea ambayo yako karibu zaidi na walengwa, yanahitaji kwa haraka maombi, mafunzo, na msaada wa fedha, ambazo zinaweza kupatikana kutoka makanisa yenye nguvu ya Magharibi. Na kwa ule mfano wa talanta, kama watumishi hawatumii karama wataipoteza (Mt 25:14-30).
Je, wasiofikiwa wanawezaje kufikiwa hata na kanisa la watu wasiokuwa na uzoefu, lakini wana moyo wa kufanya hivyo, na hawana kitu kikubwa cha kutoa? Mpango Wa Yoshua Wa Mwaka 2000 BK unaoratibu kazi miongoni mwa mataifa yaliyobakia kufikiwa unatupatia hatua rahisi zifuatazo:
1. Kwanza Ainisha Mataifa
Ambao Hawajafikiwa
Kwa kutumia anwani hii ya Mradi Wa
Yoshua
http://www.joshuaproject.net/index.php unaweza kupata taarifa muhimu
na za karibuni kabisa kuhusu maeneo ya dunia yenye watu ambao hawajafikiwa na
injili. Utawajua ni akina nani, ni mahali gani walipo, na ni nani, kama yupo,
anayejaribu kuwafikia. Unaweza kuagiza vipeperushi kwa kila kundi la watu kutoka
kwa Bethany Prayer Centre kwa kupitia anwani ya Mradi Wa Yoshua. Ndani ya
maktaba ya
http://www.dci.org.uk/ kuna Kitabu Cha Anwani ambapo misheni nyingi
zimeorodheshwa. Waweza pia kufungua tovuti hii
http://www.missionfrontiers.org/ kwa msaada zaidi.
2. Pata Watu Wenye Mawazo
Kama Yako Kanisani Au Kwenye Internet
Kazi hii si rahisi kwa mtu mmoja,
au kwa kanisa au kwa dhehebu. Ufumbuzi ni kwa makanisa ya nchi za Magharibi
kuwasiliana na nguvukazi ya makanisa ya uamsho ulimwenguni kote, na kwa pamoja
wawasiliane na makanisa yasiyokuwa na uwezo lakini ambayo yako jirani na watu
ambao hawajafikiwa. Na kwa pamoja wawe na mkakati wa maombi, watu, fedha, vifaa,
na hekima.
3. Kipekee Fanya Utafiti
Kuhusu Mataifa Uliochagua Kuwaendea
Zaburi 8:4 inauliza swali,
“Mwanadamu ni nani?” Tunapaswa kuwafahamu vizuri watu tuliochagua kuwaendea,
kwahiyo tunarudi tena kwenye tovuti ya Mradi Wa Yoshua
http://www.joshuaproject.net/index.php na kisha kwenye maktaba yako,
na ensaiklopedia iliyoko kwenye mtandao wa internet. Taarifa za maelfu ya
mataifa (ethnos) zinapatikana humo.
4. Anza Kuwafahamisha Watu
Kinachoendelea
Ukiisha kuchagua mataifa
unaokusudia kuwaendea ni muhimu kulifahamisha kanisa lako lote na makanisa
mengine ya ndani ya nchi, pamoja na waratibu wa kimataifa ili wajue
unachokusudia kukifanya, ili kwamba ushirika uandaliwe, na pia kuepuka uwezekano
wa kazi moja kufanywa na timu mbili badala ya moja. Kutoa taarifa kama hizi ni
muhimu kwa ajili ya maombi, kuhamasishwa, na kuwekwa mkakati.
5. Maombi Yako Yatafungua
Njia
Unaweza kufanya maombezi kwa ajili
ya watu walioko katika dirisha la 10/40 ukiwa nyumbani kwako na katika nchi
yako. Wakati mwingine watu wa huduma ya AD2000 na YWMA huratibu maombi ulimwengu
mzima kwa malengo maalum, mathalani kwa ajili ya Wahindu. Kutembelea maeneo kwa
ajili ya kufanya maombi, wakati mwingine kimyakimya na kutokuvuta watu ikiwa ni
lazima, kwafaa sana maana kunaweza kulibadili taifa.
6. Hatua Inayofuata Ni Kwa Kanisa Kuchagua Taifa (ethnos)
7. Lengo Ni Kupanda Kanisa
Taifa haliwezi kufikiwa mpaka
pawepo na uwezekano wa kanisa lililojitosheleza, na la watu walio tayari
kushuhudia. Zipo njia nyingi za kufanikisha jambo hili, lakini kwa vyo vyote
vile mtu asijaribu kwenda mstari wa mbele bila mshirika (mbia) wake, ushauri, na
msaada. Vitu muhimu vya kutilia mkazo katika mpango wa muda mrefu ni masuala ya
uongozi, kujipanga vizuri, malengo, utafiti, kupima kazi, ushauri na kanisa la
kitaifa lililoko jirani, kufanya umiliki wa pamoja wa mpango wa mwisho,
kushirikisha wengi, kushirikiana kwa pamoja kwenye eneo la umisheni, na kufanya
tathmini. Vitabu vingi vyenye ushauri mzuri na uzoefu vinapatikana kutoka AD2000
na Kituo cha Kimarekani cha Umisheni kinachoweza kupatikana kwenye mtandao kwa
kutembelea tovuti hii:
http://www.missionfrontiers.org/
Kujua La Kufanya Ni Muhimu Kwako
Unaweza ukakatishwa tamaa na ukubwa wa changamoto hii, lakini kushiriki kwako binafsi kunaweza kukawa ni kichocheo kinachoweza kufanya mambo yatendeke, na ukawa sababu ya taifa kufikiwa na injili ya Yesu. Kama asemavyo Isaya, “…usiwakataze; …Panua mahali pa hema yako, …enea upande wa kuume na upande wa kushoto”.
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili,Ukiwataja Kwa Majina
China (3) | ||
Jina la Watu |
Lugha Yao |
Idadi Yao |
Miao, Luobohe |
Miao, Luobohe (2nd dialect) |
60,000 |
Miao, Mashan Central |
Miao, Mashan Central |
70,000 |
Miao, Mashan Northern |
Miao, Mashan Northern |
35,000 |
Miao, Mashan Southern |
Miao, Mashan Southern |
10,000 |
Miao, Mashan Western |
Miao, Mashan Western |
14,000 |
Miao, Qiandong Eastern (Hmu Eastern) |
Miao, Qiandong Eastern |
350,000 |
1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original
English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is
granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for
sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk