1985 - 2007

 

23. Roho Mtakatifu

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Matendo 2

Mstari Wa Kukariri
“Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja” (1Kor 12:13).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, ulimpokea Roho Mtakatifu mara ya kwanza ulipoamini? Au pengine baadaye? Je, umeendelea kujazwa tangu hapo?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Kusanyikeni kwa maombi, na kisha mpitie hatua mbalimbali za kumkaribisha na kumpokea Roho Mtakatifu, mkiombeana ninyi kwa ninyi hadi wote mmejazwa.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Angalia maneno haya pletho na pleres.
Andika maelezo ya ukurasa mmoja useme yanaweza kuwa na maana gani leo.

Tafakari Mstari Ufuatao Neno Kwa Neno
Gal 5:5

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Latvia. Idadi ya watu: 3,000,000. Taifa hili liko Kaskazini mwa Ulaya   (USSR ya zamani)

Asilimia 20% ni Waprotestanti. Asilimia 20% ni Wakatoliki. Asilimia 15% ni Orthodox.

 

Ili mwamini aweze kutekeleza wito wa Mungu katika maisha yake anahitaji uweza wa Roho Mtakatifu wa Mungu ndani yake; na ingawa Wakristo wanaweza kuwa na maoni tofauti kuhusu ni lini na vipi tunavyompokea Roho Mtakatifu, hakuna mwenye shaka kwamba tunamhitaji. Kila mara  uwe mwepesi kusikiliza mawazo ya wengine kwa lengo la kujifunza na kushirikisha wengine mawazo yako bila kuleta mabishano au kuonesha namna ya kutawala mazungumzo. Hapa pana ufahamu ulio maarufu sana.

1. Ahadi Ya Ubatizo Mwingine

Katika Mdo 1:4-8, neno ubatizo ni baptizo, lenye maana ya kuzamisha au kuchovya.  Neno hilo halina maana ya  baptisma lilioko katika Efe 4:5, yaani tendo lenyewe la kubatiza; na wala si baptismos ya Ebr 6:2, lenye maana ya kutakasa.

2. Ahadi Hiyo Ilitabiriwa

Neno moja la ‘kujazwa’ ni pletho lenye maana ya kuwa kama sponji lililochovya ndani ya maji na linapokuwa limetolewa linachuruzika maji kila mahali. Neno lingine la Biblia ni pleres lenye maana ya kapu la mikate lililojaa sana, mpaka likafurika na kudondosha chakula kila mahali.

3. Roho Mtakatifu Ni Ahadi Ya Baba

Nyakati za Agano la Kale Roho alikaa juu na si ndani ya watu wa Mungu (Hes 11:25). Hata hivyo palikuwepo na matukio maalum kama vile kwa Bezaleli na Yoshua (Kut 31:3) na (Kum 34:9).

4. Roho Mtakatifu Ni Ahadi Ya Yesu

Yesu alisema Roho Mtakatifu anakuja, (Yn 7:37-39) (Yn 14:16) (Yn 16:7).

Ataishi nanyi na kukaa ndani yenu (Yn 14:17).

Atawavika uweza (Lk 24:49).

Yesu aliamuru wafuasi wake kumpokea Roho Mtakatifu (Yn 20:22) (Mdo 1:5-7).

 

5. Yesu Alituahidi Uweza

Katika Mdo 1:8 neno lililotumika dunamis, lina maana ya uweza wa kutenda lo lote, au kutenda miujiza (Mt. 25:15)  (Gal 3:5) (Mdo 8:13) (Mk 6:5). Neno lingine la Biblia lenye kumaanisha uweza ni exousia, na hili hasa lina maana ya mamlaka (Lk 10:19).

Exousia hutupa haki, lakini tunahitaji dunamis ili tuweze kutumia exousia.  Mtu anaweza kuwa na mamlaka ya kutwaa shamba la mtu mwingine, lakini atahitaji uweza wa kumwondoa katika shamba hilo. Wewe una mamlaka juu ya mapepo wachafu, lakini unahitaji uweza wa Mungu kuyatoa.

6. Ahadi Inaanza Kutekelezwa

Katika Mdo 2:1-11, Roho Mtakatifu anakuja na uweza, na waamini 120 kila mmoja ananena kwa lugha mpya ambayo hakuwahi kujifunza (1 Kor 14:5,18). Watu kutoka mataifa mbalimbali wanakuja mbio ili wapate kusikia maajabu ya Mungu katika lugha zao wenyewe. Hata leo bado ni kusudi la Mungu kutujaza Roho wake. Petro alisema kwamba kuja kwa Roho Mtakatifu kuliashiria mwanzo wa siku za mwisho (Yoeli 2:28-32) (Mdo 2:16-21).

7. Ahadi Inatoka Nje

Waamini wa Kiyahudi walijazwa na Roho Mtakatifu tena na tena. Na kisha Wasamaria waliokuwa jirani walipoamua kumfuata Yesu nao pia walimpokea Roho Mtakatifu (Mdo 8:4-8,14-17).

Petro alimtembelea Kornelio, yule askari Mrumi, na alipoanza kunena habari za Yesu, Roho Mtakatifu aliwashukia watu wote waliokuwepo mahali pale; jamaa yake na rafiki zake (Mdo 10:44-46).

Vilevile tunaona kwamba baadaye hata watu wa Uturuki nao walijazwa (Mdo 13:52) na (Mdo 19:1-7).

Paulo aliandika kwamba tunapaswa kuwa tunaendelea kujazwa na Roho Mtakatifu (Efe 5:18) (Mdo 4:31).

8. Ahadi Hiyo Ni Yako Leo

Mdo 2:38, 39 inatuonesha kwamba hakuna kikwazo cha wakati hata kwa sisi tulio mbali. Unaweza kuona picha ya namna ya kumpokea Roho Mtakatifu kwa uzoefu wa Maria katika Lk 1:35. Roho Mtakatifu anaweza kuja juu yako na uweza wa Mungu ukakufunika, na kuruhusu mtoto mwingine mtakatifu wa Mungu kuzaliwa.

Je, ulimpokea Roho Mtakatifu mara ya kwanza ulipoamini? (Mdo 19:2).

Je, umejazwa Roho Mtakatifu hata sasa?

Je, unachuruzika baraka za Mungu kama lile sponji; au kufurika mkate wa uzima kama lile kapu?

Je, unataka dunamis maishani mwako?

Je, unamtaka kweli Roho Mtakatifu maishani mwako? Yeye hushuhudia kwa habari ya dhambi, hukuwezesha kuishi maisha matakatifu, na anaweza pia kukuita hata miisho ya nchi.

9. Mkaribishe Roho Mtakatifu Sasa

  1. Uwe na kiu na Mungu (Yn 7:37)
  2. Litakase ‘hekalu’ lako kwa kumwomba Mungu akusamehe dhambi zako  (1 Kor 6:19) (2 Kor 6:14-7:1) (1 Yoh 1:9).
  3. Kataa kwa jina la Yesu kila roho mwingine uliyewahi kumpokea.
  4. Mwombe Baba akupe zawadi ya Roho Mtakatifu (Lk 11:9-13).
  5. Mkaribishe kwa maombi ya imani.
  6. Mpe uhuru wa kuingia po pote apendapo; mwilini mwako, nafsini mwako, katika mawazo yako, katika roho yako; katika maisha yako ya zamani, ya sasa, na yajayo.
  7. Sasa pumzika na kuipokea hiyo zawadi, mnywe kwa wingi (Yn 7:37) (1 Kor 12:13).

Ushinde kila namna ya woga na kiburi, mshukuru kwa kuja, jisalimishe kwake na utazamie amani, furaha, kicheko, machozi, au vyote kwa pamoja. Pengine utanena kwa lugha, au utamsifu Mungu, au utaabudu, au utatabiri mara moja au baadaye kidogo. Mara utagundua uwepo wake katika kila eneo la maisha yako (Mdo 2:4) (Mdo 10:46) (Mdo 19:6).

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili

 

Ethiopia

Jina la Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Bale

Kacipo-Balesi

10,000

Saho

Saho

24,000






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk