1985 - 2007

 

26.Tafakari

Tumia dakika chache kuwaza na kuomba

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Zaburi 91

Mstari Wa Kukariri
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapostawi sana (Yos 1:8).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Ni ahadi zipi zimetolewa kwa wale wanaoweka mawazo yao na mioyo yao kulishika neno la Mungu usiku na mchana?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Kama bado huna, tafuta mahali pa siri pa Aliye Juu. Weka jina lako hapo, panga muda, na kisha andaa utaratibu wa kukutana na Mungu mahali hapo kila siku. Tutakapokutana tena uwe tayari kutufahamisha unavyoendelea.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Mwombe Bwana akuoneshe kwa undani mstari mmoja wa Biblia wiki hii, na kisha kwa kutumia fahamu zako zote, uandike taarifa ya kurasa mbili ukielezea yale yote aliyokufunulia.

Tafakari Mistari Ifuatayo Neno Kwa Neno
Mit 24: 3, 4

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Canada. Idadi ya watu: 28,000,000. Idadi ya ‘Wakristo’ ni asilimia

85%  

 

Watu wengi wanapendekeza utaratibu wa tafakari, na dini za nchi za Mashariki wanapenda sana kuutumia utaratibu huo. Tahadhari- tafakari ya kidunia ina lengo la kukuacha mtupu kifikra, na iwapo utafanya hivyo, hakika Shetani atakujaza  na mambo yake. Je ulishagundua kwamba katika vita mapambano hufanyikia juu ya ardhi isiyokuwa na mwenyewe katikati ya pande hizo mbili? Kwa usalama wako na mawazo yako, hakikisha wakati wote upo upande wa Mungu.

Tafakari ya Kibiblia huujaza ufahamu wako na Neno na hili limekuwa ni sehemu ya kutembea kwetu na Mungu tangu zamani.

1. Manufaa Ya Kutafakari

Neno la Mungu ni mlango wa kuingilia kwenye mawazo ya Mungu, na tafakari ni njia za kuingilia kwenye vyumba vilivyojaa hazina tele. Tafakari ni mahali pa kukutana na Mungu na unaweza kutazamia ufunuo, kukua, kutiwa moyo, uweza na ufahamu wa vita vya kiroho, na kushuhudia.

Tafakari Neno Mchana Na Usiku
Utapata maendeleo na mafanikio
Utazaa matunda kwa wakati wake
Makuzi yako mapya hayatanyauka

Utastawi kwa lo lote utakalofanya

Utapata uweza mkubwa zaidi wa kufahamu mambo

Utabarikiwa katika yale uyafanyayo

Utakuwa na wema umehifadhiwa ndani yako

(Yos 1:8) (Zab 1:2, 3) (Zab 119:99) (Yak 1:25) (Mt 12:35).

2. Sababu Mbili Za Kutafakari

Ya Kwanza, Ni Kumbariki Mungu

Daudi alitaka maneno ya kinywa chake na tafakari ya moyo wake vimpendeze Bwana (Zab 19:14).

Ya Pili, Ni Kujawa Na Neno

Paulo alisema, " Neno la Kristo na likae ndani yenu kwa wingi". Ndipo mtakapoweza kufundishana na kuonyana kwa hekima yote (Kol 3:16).

3. Unatafakari Juu Ya Nini?

Tafakari ni muda mzuri wa kujifunza kuhusu mawazo ya Yule umpendaye, kumgundua, jinsi anavyowaza, hekima yake na njia zake. Utashangaa jinsi Mungu atakavyozungumza na wewe mara tu panapokuwa na utulivu ndani mwako na ukaweza kuisikia sauti yake. Waandishi wa Zaburi waliandika kuhusu mielekeo yao katika tafakari. Walisemaje?

Tunatafakari juu ya upendo wako unaodumu

Nitatafakari juu ya kazi zako zote

Tunatafakari ukuu wa matendo yako yote

Ninatafakari juu ya kanuni zako

Ninatafakari njia zako

Ninatafakari sheria yako mchana kutwa

Ninatafakari juu ya ahadi zako

(Zab 48:9) (Zab 77:12) (Zab 119:15, 97,148).

4. Unatafakari Namna Gani?

Kutafakari kuna maana ya kuchukua muda na kuwa makini katika jambo  unalowaza; kuwaza juu ya jambo au kulizungumzia kwa uangalifu; kuwaza kwa makini na kwa undani; kujenga picha katika fikra zako namna ambavyo jambo linaweza kuwa; kujifunza au kuchunguza ili ujue; kusema jambo kwa sauti ya chini ambayo haisikiki vizuri kwa ajili ya kuwa na mawazo; kumshirikisha mtu mwingine hisia zako au misisimko yako bila kutamka maneno; na hata kulalamika. Zifuatazo ni njia zilizojaribiwa za kukusaidia wewe kuwa na muda mzuri wa kutafakari. Ukiwa mvumilivu katika kutafakari, tabia hiyo itakufanya ustawi katika ukristo wako kwa viwango vya juu kuliko unavyoweza kufikiria.

Unahitaji Kuwa Na Mahali Pako Pa Siri Pa Aliye Juu

Soma Zaburi ya 91. Ikiwa ni kwenye kona, au chumbani, ikiwa ni darini, au chumba cha chini ardhini, Mungu anaweza kukutana na wewe po pote. Mama mmoja alizoea kujitupia aproni yake kichwani, na anapofanya hivyo familia nzima walijua kwamba huo si muda wa kumsumbua kwa lo lote! Lakini kwa Isaka, mahali pa siri pa kukutana na Mungu ni shambani (Mwa 24:63).


Unahitaji Utulivu

Mahali ambapo ni mbali na makelele ya wanafamilia na watu wengine, mbali na kelele za mitaani, mbali na simu, mbali na TV. Je, hapana mahali pa namna hiyo karibu nawe? Je, hali ya utulivu ikoje saa kumi na moja alfajiri? Hapo ndipo mahali pangu pa siri.


Unahitaji Kuwa Na Nidhamu

Ya kwenda mahali pako pa siri kila mara na pia kukabiliana na vishawishi na majaribu yanayokujia kwenye mawazo yako na pengine kwenye tumbo lako. Uwe na daftari la kuandika yale ambayo akili zako zinasema ni muhimu. Ufahamu wako utaridhika na hilo. Uwe na muda wa kutosha wa kupata utulivu ndani yako. Kwangu mimi inanichukua kama dakika 20 au zaidi. Omba na kumkaribisha Bwana azungumze nawe na kukuelekeza.


Unahitaji Njia Ya Kufuata

Jambo linalokupendeza, linalokamata mawazo yako haraka, au mstari wa Biblia anaokupa Mungu. Halafu unaweza kuingia katika ufahamu wa Mungu kwa kadiri anavyokufunulia na kukufafanulia neno lake. Yeremia alisema, “Maneno yako yaliponijia, niliyala; yakawa furaha kwangu na shangwe kwa moyo wangu…” (Yer 15:16).


Chukua Muda Wako

Kupitia hilo andiko neno kwa neno, ukitumia uwezo wako mtakatifu wa kufikiri, kuona, kusikia, kunusa, kugusa, na hata kuonja kile kinachotokea katika hayo maneno. Sikiliza kutoka kwa Roho Mtakatifu mawazo ya ubunifu na ufafanuzi wa kipekee.


Sasa Endelea Kwa Wakati Wako 
Soma Ayu 23:10 -12 hatua kwa hatua.

Anaijua  

njia . . ninayoiendea.

Atakapokuwa amenijaribu,  

Nitajitokeza kama dhahabu.

Kwanini?

Kwa sababu miguu yangu inafuata kwa karibu . . hatua zake. .

Sasa endelea, tafakari, tafuna, waza kwa kina, fikiria, chunguza, nong’ona, shirikisha uliyo nayo, na hata kulalamika lakini mbele za Yesu.


Au unaweza ukatafakari juu ya jambo kama majina ya Mungu, pengine jina moja kwa siku moja.

Yehova Tsidekenu – Bwana Haki yangu.

Yehova M’Kaddesh – Bwana Atakasaye.

Yehova Shalom – Bwana ni Amani yangu

Yehova Shammah – Bwana Yupo.

Yehova Rophe – Bwana ni Mponyaji.

Yehova Jireh – Bwana ni Mpaji.

Yehova Nissi – Bwana Bendera yangu.

Yehova Rohi – Bwana Mchungaji wangu.

Je, umegundua kwamba kila somo linakupa mstari mwafaka wa kuutafakari unapokuwa mahali pako pa siri?

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu
Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Ujerumani

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Wanaonena Ki-Urdu 

Ki-Urdu

16,000






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk