1985 - 2007

 

27. Kumsikia Mungu

Martin Luther alimsikia Mungu na akaanza Matengenezo

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Yohana 10:1-16; Zaburi 29; Mathayo 4:4

Mstari Wa Kukariri
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako (Mit 3:5, 6).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Kwa kawaida watu wanapataje mwongozo kabla hawajaamua la kufanya? Linganisha jibu lako na dondoo za somo hili ili upate njia iliyo bora na kisha usonge mbele.

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Anza utaratibu wa kuandika mambo yote Mungu anayokuambia. Andika mistari ya Biblia, matukio, na riziki anazokupa, na kisha ufanye rejea ili kugundua ufunuo mzima.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Angalia orodha ya njia zisizo za kawaida za kupokea miongozo, halafu katika ukurasa mmoja andaa orodha ya matukio ya jinsi hiyo na kuonesha ni wapi yalikotukia katika Biblia.

Tafakari Mistari Ifuatayo Neno Kwa Neno
Ufunuo 19:9,10

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Tibet. Watu  2,200,000 ni wafuasi wa Dalai Lama

Ilivamiwa na China na kuna uwezekano walikufa watu 1,000,000. Ni mabudha. Kuna wakristo wachache.

 

1. Je, Mungu Ataniongoza?

Watu wengi katika upumbavu wao wamegeukia mapepo wakitafuta mwongozo (Isa 8:20) lakini hakuna aliye bora katika kuwaongoza watu wake kama Mungu. Soma (Mit 3:3-5) (Rum 12:1,2) (Zab 25:9) (Zab 32:8,9) (Zab 37:23,24) (Zab 48:14).

Njia Ni Ipi?
Yesu ndiye Njia, Kweli, na Uzima. Anasema, “Nifuate” (Yn 14:6) (Lk 1:79) (Ufu 7:17). Ukitaka kujua yote kuhusu njia za Mungu mtazame Yesu kwa sababu Yeye na Baba ni wamoja (Yn 6:38) (Yn 10:30) (Ebr 1:3).

Je, mtumishi wa Ibrahimu alisema nini? (Mwa 24:27).

Kwanini watu waliopotea walifurahi? (Zab 107:7).

Kwanini wafalme walifurahi sana? (Mt 2:9-12).

Ni nani aliyemwambia Petro kwenda? (Mdo 10:9-19)

Ni nani aliyesema wapelekwe? (Mdo 13:1-3).

Ni nani anayemwongoza Paulo? (Mdo 16:6-10).


Ni nani atakayesema nawe na kukuongoza hata kwa matatizo yako ya kila siku?

"Siku moja nikiwa safarini Ufaransa nilikuta mgomo na barabara zote zilikuwa zimezibwa na malori. Mtu mmoja mwanamume alitujia na kutusemesha kwa lugha ya Kihispania na kutupa maelekezo ya kina jinsi ambavyo tungeweza kufika Hispania kwa kutumia njia za uchochoroni au ‘njia za panya’. Niliandika maelekezo yote, na niliponyanyua kichwa changu, alikuwa ameshaondoka. Siku ile ni gari letu pekee lililomudu kuvuka mpaka. Yule mtu alikuwa nani? Yeye alijuaje kwamba mimi nakifahamu Kihispania? "


Mungu Hayuko Kimya

Kwa kweli amekuwa akisema tangu mwanzo. Kuisikia sauti ya Mungu ni hatua ya kwanza ya kujua maongozi ya Mungu (Mwa 1:3) (Ebr 1:1,2).

2. Je, Mungu Anasema Nasi Kwa Namna Gani?

Mungu Anasema Kupitia Neno Lake

Utashangaa namna utakavyosikia kwa moyo wako kadiri unavyosoma kwa macho yako (Zab 119:105) (Ebr 4:12). Kila mara ukumbuke kwamba Mungu anayekupa wewe ufunuo ndiye anayestahili kuulizwa tafsiri ya ufunuo huo na matumizi yake.


Mungu Husema Kupitia Roho Wake

Anaishi ndani yako, (Yn 14:17).

Analifanya neno la Mungu kuwa hai, (Mwa 1:2,3) (Zek 4:6).

Anasema nasi kwa ndani, (Rum 8:16).


Je, Roho Hufanya Nini Zaidi?

Huwaongoza wana wa Mungu, (Rum 8:14).

Husema wakati wa ibada (Mdo 13:2).

Husema kupitia unabii, lugha na tafsiri, maneno ya maarifa, hekima na utambuzi, (Lk 2:25-38).

Hufungua na kufunga milango (Mdo 16:10).


Isikilize Sauti Yake Moyoni Mwako

Baadhi ya wafanyabiashara wakristo walikuwa wanamfanyia usaili meneja mmoja mzoefu kwa ajili ya nafasi muhimu ya ajira. Wote walijua nafsini mwao kwamba mtu huyo ni mwongo, lakini hakuna hata mmoja aliyethubutu kulisema hilo. Miezi michache baadaye meneja yule akasababisha hasara kwa kampuni. Wale wafanyabiashara walipokutana tena, walikiri mmoja baada ya mwingine kwamba walikuwa wameonywa na sauti ya Mungu, lakini hakuna aliyetii!


Mungu Hunena Nyakati Za Maombi

Ukimwita Mungu atakujulisha mambo makubwa usiyoyajua (Yer 33:3).

Daudi alijijengea tabia ya kumwuliza Mungu jambo la kufanya (2Sam 5:19).


Mungu Hunena Katika Njia Zisizo Za Kawaida

Mungu hutuma ndoto, maono, maneno ya kusikika, tahadhari, hofu na mashaka. Hufanya ishara elekezi kama vile nguzo ya wingu au ya moto, kichaka kinachoungua, hata nyota na mawimbi (Ayu 3:14-28) (Kut 13:21) (Kut 3:2) (Mt 2:2) (Yon 1:12).


Juanita alikuwa katika safari ya kimisheni kwenda Afrika Magharibi akipitia Senegal. Siku moja Bwana akanena naye katika ndoto ya usiku akisema, “Unahitaji viza kuingia Senegal”. Alipiga simu kwenye shirika la ndege, lakini wao walimwambia, “Hapana, huhitaji viza”. Baadaye alipiga simu katika ubalozi nao wakamwambia, “Ndiyo, unahitaji viza”. Safari ile ilifanikishwa kwa ile ndoto ya Bwana.


Mungu Hunena Kupitia Malaika Anaowatuma Kwetu

Gabrieli na malaika wengine hata sasa hutuletea jumbe kutoka kwa Mungu kama walivyowahi kufanya siku za nyuma (Dan 10:4-21) (Lk 1:11-20) (Lk 1:26-28) (Lk 2:10-15) (Ebr 13:2) (Ufu 19:9,10).


Mungu Hunena Kupitia Watu

Waamini wenzetu na hasa wale waliokomaa, wake kwa waume,  wazee na wahudumu, hutuletea ujumbe wa neno la Mungu kwa kuhubiri, kufundisha, kushauri, na kwa karama za Roho (Mdo 15:28).


Mungu Hunena Kupitia Mathibitisho

Kama huna uhakika na chanzo cha uongozi unaoupata, usiogope kumwuliza Mungu na kumwomba athibitishe hekima yake kwako (Yak 1:5-7) (1Yoh 4:1). Usiondoke bila kupata uthibitisho wa refa wa Mungu, yaani karama ya amani yake moyoni mwako na nafsini mwako (Kol 3:15).


Mungu Hunena Kwa Uongozi Wake

Mungu hukutia moyo kwenda kwa kukufungulia milango, na kukupa watu, fedha au vifaa (Ezr 1:5-7).

3. Je, Tunapokeaje Uongozi Wa Mungu?

Ni kama eropleni inayotaka kutua. Kutoka mbali inaelekezwa na rada ili kupata mwelekeo wa mahali ulipo uwanja. Kisha kuna mawasiliano ya redio yanayomwelekeza rubani njia na baadaye taa zinamwonesha uwanja. Taa zingine zinamwonesha rubani waziwazi njia iliyoko chini mahali ambapo ndege itatua, na baada ya kutua yupo mtu anayemwelekeza rubani mahali pa kuegesha ndege. Kwa maneno mengine, uongozi huja kwa njia nyingi, na wala hauji hatua zote kwa mara moja; bali huja hatua kwa hatua na kuongezeka kwa kadiri safari ya imani inavyoendelea (Mit 16:9).

Wakati mwingine Mungu hukawia kudhihirisha matakwa yake ili muda wake unapowadia apate kuuonesha utukufu wake. Uwe na subira; unajuaje kama hutapata zaidi ya matarajio yako kama ilivyokuwa kwa dada zake Lazaro! (Yn 11:5-44). Je, utathubutu kuacha kuufuata ufunuo wa Mungu? Usihofu kwa maana Mungu amekuwekea usalama wa kutosha. Kama tukitaka mapenzi yake, sauti ya Mungu ipo kila wakati ili kuthibitisha, kusahihisha, na hata kufutilia mbali mipango yetu (Isa 30:21).

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu
Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Ghana

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Nabra (Nabt)

Nabt

46,000






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk