1985 - 2007

 

28. Ibada

Mwabudu Bwana katika uzuri wa utakatifu

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Ufunuo 4 na 5

Mstari Wa Kukariri
Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako,  na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza (Kut 23:25, 26).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Taja baadhi ya sanamu na miungu ya uongo ambayo wanadamu huitumikia na hivyo kumfanya Mungu aone wivu na kukasirika.

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Andaa hafla maalum kwa ajili ya kumfanyia Mungu ibada wakati wa jioni. Watafute na kuwashirikisha wapakwa mafuta, na kumfurahisha Mungu kwa nyimbo za kusifu na kuabudu.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andaa orodha ya mistari mbalimbali katika Zaburi inayoonesha njia mbalimbali zilizotumika kumwabudu Mungu.

Tafakari Andiko Hili Neno Kwa Neno
Waefeso 5:19,20

Tumia Dakika Moja Kuubadili Ulimwengu

Ombea taifa la Albania; Idadi ya watu: 3,500,000;

Ni taifa la kwanza ambalo awali kabisa halikuamini kwamba kuna Mungu. Na sasa limeharibiwa na kutokuwepo na serikali pamoja na tatizo la wakimbizi. Kitakachotamalaki sasa ama ni Injili au Uislamu.

 

Kimsingi mwanadamu ni kiumbe anayeabudu. Ibada ni sehemu ya asili yake. Swali pekee la kujiuliza ni nani mungu anayemwabudu? Ye yote tunayemwabudu, hatimaye huyo ndiye tutakayemtumikia. Kanuni ni kwamba, kwa kadiri tunavyoendelea kuabudu cho chote au ye yote tunayemwabudu ndivyo hivyo tutakavyoendelea kujitoa kwake, na kwa kasi iyo hiyo tutaendelea kufanana na kile tunachokiabudu.

1. Kuabudu Kuna Maana Gani?

Neno la Kiebrania shachah lina maana ya kuabudu, kusujudia,  kuinama kwa kuonesha unyenyekevu, kuonesha heshima kubwa au kuanguka kifudifudi. Neno la Agano la Kale proskuneo halikadhalika lina maana ya kubusu mkono, au kupiga magoti na kugusa ardhi kwa paji la uso kwa unyenyekevu mkuu.  Maneno mengine mawili ya kuabudu yana maana ya kutumika, kufanya ibada takatifu na kumtolea Mungu sadaka.

2. Waache Watu Wangu Waondoke, Ili Wapate Kunitumikia

Dai hili Mungu alilolirudia mara kwa mara lilipelekea Farao kuwaruhusu watu wa Mungu kutoka Misri. Tangu wakati huo, Mungu, Mungu mwenye wivu, amekuwa akipambana na watu wake akiwazuilia kuabudu miungu mingine na sanamu, na badala yake  wamwabudu Mungu aliye hai na wa kweli.

Ibada ni kumtukuza Mungu na kumfurahia daima. Mungu anawatafuta watu wa kumwabudu, na kufanya ibada ndiyo wito wetu wa kwanza (Yn 4:23). Ibada ya kweli ni pale tunapomruhusu Roho Mtakatifu atuongoze kutoka katika roho zetu au mioyo yetu kuabudu katika roho na katika kweli (Flp 3:3).

Ibada ni tendo la thamani kubwa, ni la kipekee na linamhusu Mungu na Mwanaye Yesu Kristo ambao peke yao wanastahili. Lucifer, aliyekuwa mhusika mkuu wa ibada huko mbinguni, alitaka ibada hiyo iwe kwa ajili yake, maana yake aabudiwe yeye; na hilo ndilo lililopelekea kuanguka kwake (Isaya 14 na Ezekieli 28). Hata wakati fulani alitaka Yesu amsujudie ili eti ampe falme zote za dunia lakini Bwana alikataa (Mt 4:8-10).

3. Ibada Hukifanya Chumba Kujawa Na Mungu

Katika nyakati za Biblia watu wengi wake kwa waume walipakwa mafuta na Mungu na kisha kuteuliwa na viongozi wao kuwaongoza watu wa Mungu zamani hizo, kufanya ibada ya kinabii na si kama sisi tanavyofanya katika siku zetu kwa kuimba tu nyimbo katika makusanyiko yetu (1Nya 25:1,6-8).

Ibada huandaa njia ya Mungu kushuka na kukujaza wokovu maishani mwako (Zab 22:3) (Zab 50:23). Ibada ya watoto ina uwezo wa kumnyamazisha adui (Zab 8:2).

4. Nitambariki Bwana Nyakati Zote

Je, ni wakati gani tuabudu? Nyakati zote. Kwa nyakati zilizotengwa  Zaburi ya 100 inatuelekeza namna ya kuanza, lakini zaidi ya yote tunapaswa kuishi maisha ya ibada bila kukoma. Kwa kila tunapopumua, kwa kila wazo, kwa neno na tendo, tunapaswa kumwabudu Mungu wetu mzuri tunayemtumikia milele na milele (Zab 145:1,2).

5. Ibada, Zamani, Sasa Na Wakati Ujao

Watu walianza kuliitia jina la Bwana zamani sana. Wakati Abramu alipokuwa akiiendea ile Nchi ya Ahadi, jambo la kwanza alilolifanya kila alikokwenda ni kujenga madhabahu kwa ajili ya ibada (Mwa 4:26) (Mwa 12:6).

Siku zilipita na watu wakafanyia ibada kwenye Hekalu na kwenye masinagogi; lakini siku hizi miili yetu ni hekalu la Mungu (1Kor 6:19). Maana yake ni kwamba sisi tunaweza kuabudu bila kukawia, mahali po pote, katika mazingira yo yote. Paulo na Sila walifanyia ibada gerezani (Mdo16:25).

Lakini ibada yetu hapa duniani ni picha tu ya ibada ya mbinguni. Yakupasa kusoma aya za utukufu za Ufunuo 4, 5, na 19:1-10 ili upate kuona kwamba ibada ya mbinguni imejawa na rangi, nuru, sauti, miondoko na shughuli. Ibada yetu inapaswa kufanana na hiyo ya mbinguni.

6. Je, Tunafanyaje Ibada?

Biblia inatufahamisha jinsi watu walivyotumia mioyo yao, mawazo yao, mikono yao, viganja vyao, miguu yao, na midomo yao katika uimbaji. Walipaza sauti zao kwa furaha na kusujudu, kucheza, kusifu, kubariki na kushukuru.

Maneno kama halal na haleluya kutoka katika Zaburi yana maana ya kusifu, kumwinua na kumwadhimisha Bwana. Neno Yadah lina maana ya kunyoosha mikono hewani, na neno barak lina maana ya kupiga magoti katika ibada ya kumbariki Mungu.

Kuitoa miili yetu katika kumhudumia Mungu na mwanadamu ni ibada pia (Rum 12:1). Watu pia humwabudu Mungu katika sanaa zao, katika uandishi wao, katika michezo ya kuigiza, katika muziki, katika usanifu wa majengo, na hata katika utoaji wa fedha zao kwa ajili ya Injili.

7. Ibada Kanisani

KatIka kanisa makusanyiko yetu yanapaswa kujawa na zaburi, nyimbo, na tenzi za rohoni ambazo zinaweza kuongozwa na Roho katika lugha mpya anazotupatia Yeye. Kwahiyo mikutano mingi ya kisasa haina tofauti sana na burudani za kikristo kama kwenye kumbi za starehe. Watu huwa wanaangalia tu, lakini je, wanaabudu? Uwepo wa Mungu na Roho wake katika ibada zetu utawafanya watu wasioamini kuanguka chini na kuabudu (Kol 3:16) (1Kor 14:15,16,25,26) (Efe 5:19) (Mdo 2:4). 

Je, Kusifu Na Kuabudu Ni Kitu Kilekile?
Tunapaswa kumsifu Mungu kwa jinsi alivyo na kwa matendo yake; lakini Mungu mwenyewe anawatafuta na anawataka wafanya ibada, na si mradi ibada tu.

Kusifu kwaweza kufanywa hadharani, lakini ibada mara zote ni jambo la ndani ya moyo.

Kusifu mara zote kunaweza kuonekana au kusikika, lakini ibada yaweza kuwa ya kimyakimya na iliyofichika.

Kusifu kunaonekana, kuna kutumia nguvu, kuna misisimko na furaha; lakini ibada mara zote ni heshima na hofu katika uwepo wa Mungu.

8. Ibada Ya Kweli Ina Gharama

Biblia inazungumzia habari za sadaka za kusifu. Daudi alicheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote, na akakataa kumtolea Mungu kafara ambayo isingemgharimu cho chote (2Sam 6:14;  24:24). Wale mamajusi wa Mashariki walitoa zawadi za gharama kubwa walipokuja kumwabudu Yesu (Mt 2:9-12), na mwanamke mmoja alimpaka Yesu kwa mafuta ya gharama kubwa, akamwosha miguu yake kwa machozi yake, na kuifuta kwa nywele zake (Lk 7:36-50).

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

India (1)

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Agariya (Agria)

Agariya

11,800

Baiga (Baigani, Bega)

Baiga

10,000

Bathudi

Bathudi

104,500

Bedia

Bedia

32,200

Bhim

Bhim

19,900

Bhottara (Dhotada)

Bhottara

342,000






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk