1985 - 2007

 

29. Maisha Ya Imani

Imani ni kutulia na kumwamini Mungu

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Waebrania 11

Mstari Wa Kukariri
Yesu akajibu, akawaambia, “Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, ye yote atakayeuambia mlima huu,’ng’oka ukatupwe baharini’, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake” (Mk 11:22, 23).

Baadaye Fanya Maombi Kuhusiana Na Mambo Haya
Taja milima iliyosimama mbele yako, inayozuia maendeleo yako. Isemeshe katika maombi, na kuiamuru kuondoka.

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Andaa orodha ya ahadi zote za Mungu kwa ajili yako. Chunguza moyo wako uone kama bado unamwamini Mungu katika ahadi hizo licha ya hali ngumu au mazingira yanayosababisha upinzani. Ukitaka waweza kutubu na kumwamini tena Mungu, huku ukimshukuru kwa imani kwa majibu.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika maelezo ya kurasa mbili ukielezea aina mbalimbali za imani zinazopatikana kwenye Biblia.

Tafakari Andiko Hili
Filemoni 6

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Japan. Idadi ya watu: 126,000,000. Watu ni matajiri lakini wamepotea. Wengi wao wanaabudu mizimu. Lipo dhehebu la kiinjili lenye wafuasi wapatao 250,000 tu.

 

 

1. Imani ni nini?

Jibu rahisi linapatikana katika kitabu cha Waebrania 11:6 ambapo Biblia inasema kwamba unatakiwa kuamini kwamba Mungu ni halisi, na kwamba Yeye huwapa thawabu hao wamtafutao kwa bidii.

Katika bara la Afrika nimekutana na mtu aliyezaliwa machakani katika hali ya umaskini, lakini leo anamiliki kiwanda, nyumba nzuri na gari. Yeye ni mwajiri na pia mzee wa kanisa, akiendelea kufurahia maendeleo na majukumu aliyopewa na Mungu katika nchi yenye umaskini mkubwa.

Je, Hayo Yalitukiaje?
Alisema, “Siku moja miaka mingi iliyopita mmishenari mmoja alihubiri injili katika kijiji chetu chenye Waislamu watupu. Nikiwa mtoto nilimwamini Mungu, na kumpokea Yesu. Nilianza kumwomba Mungu anisaidie ili niweze kwenda shule, kisha chuo kikuu, na kuendelea. Niliziamini ahadi za Mungu”.

2. Kwa Imani. . .

Kutoka Ebr 11:1-39

Tunaweza kuufahamu ulimwengu huu na mahali tunakotoka (ms 3)

Tunaweza kuabudu kama Habili (ms 4)

Tunaweza kumfurahisha Mungu kama Enoko (ms 5)

Tunaweza kuepuka majanga, na kuziokoa familia zetu kama Nuhu (ms 7)  

Tunaweza kupokea wito wa Mungu na kutii kama Abramu (ms 8)

Tunaweza kuyafanya yale yasiyowezekana katika hali ya kawaida (ms 11)  

Tunaweza kujua kwamba mwisho wa dunia umekaribia na kutimiza wajibu wetu (ms 13-16)

Tunaweza kujitoa mhanga tukiujua uaminifu wa Mungu kama alivyofanya Ibrahimu (ms 17).  

Tunaweza kuondokana na maisha ya dhambi na kuona visivyoonekana, kama alivyofanya Musa (ms 25,27).

Biblia inasema kwamba, “Watu hawa wote waliendelea kuishi kwa imani hadi kufa kwao”, na kwamba, “Hawa walipongezwa kwa imani yao, ingawa hakuna hata mmoja kati yao aliyeipokea ile ahadi” (ms 13, 39).

Kwanini Imekuwa Hivyo?
"Mungu alikuwa anatuwazia mambo mazuri sana ambayo ni ya manufaa kwao pia, na wasingeweza kupokea tuzo mpaka sisi nasi tumemaliza mbio."

3. Ni Nini Basi Hii Imani Muhimu Namna Hiyo?

Imani ni kuwa na uhakika kwamba Mungu ni halisi, na kwamba anatunza ahadi (Hes 23:19). Mwanamama mmoja aliambiwa na daktari wake kwamba uwezekano wa yeye kupata mtoto ulikuwa mdogo sana. Mama yule alikataa kufanyiwa matibabu ya majaribio na akaweka imani yake kwa Mungu na ahadi yake katika Kut 23:25. Miaka kadhaa ilipita, na mama yule akalia sana, na imani yake ikapungua. Mwezi mmoja baada ya maombi maalum kwa ajili yake, mama yule hatimaye alipata ujauzito. Daktari yuleyule aliyesema, “haiwezekani” alimzalisha yule mama mtoto wa kike akaitwa Elisabet, maana yake Mungu ametunza ahadi.

Imani Ni Kumwita Mungu

Ni nini kilichowatokea wale watu waliopotea katika maisha? (Zab 107:4-9)

Na waliopotea katika dhambi je? (ms 10-16)

Na wale waliopotea katika magonjwa? (ms 17-22)

Na hata wale waliopotea katika safari ya hatari? (ms 23-31).

4. Je, Imani Hutoka Wapi?

Kuna imani iokoayo, karama ya Mungu (Efe 2:8), na

Imani katika huduma (Rum 12:3) (2 Tim 1:6)

Kuna imani inayosamehe (Lk 17:5).

Imani huja kwa ‘kusikia’ analosema Mungu kupitia Biblia, kwa njia ya mahubiri, kanda za kunasia sauti na vitabu (Rum 10:17).

Kuna karama ya imani (1Kor 12:9).

5. Imani Maana Yake Uamini Moyoni Mwako

Sisi tu mwili, nafsi na roho (1 The 5:23), lakini kwa kuwa Mungu naye ni Roho (Yn 4:24), tunamwamini katika roho zetu. Neno roho katika Biblia lina maana ya mioyo yetu. Moyo ni nyumbani kwa imani iliyo hai na yenye joto, na Mungu ameufanya kuwa msingi wa akili zetu ambazo ni kisima cha elimu na maarifa (Mk 11:23, 24) (Rum 10:10). Mithali 23:23 inatuambia tuinunue kweli na wala tusiiuze, ikiwa na maana kwamba kweli ina bei, na hiyo bei yaweza kuwa ni kuziamini ahadi za Mungu dhidi ya hali zo zote zilizo kinyume. Wakati mwingine   akili ya mtu aliyesoma na ambaye si wa kiroho,inaweza ikaamua kuuza kweli ya Mungu na kushikamana na kweli za kibinadamu ambazo kwa kweli zinapaswa kuwekwa nyuma ya imani ya kweli itokanayo na neno la Mungu. Paulo, mtu msomi kwelikweli wa enzi zake, alisema tunapaswa kuishi kwa imani na si kwa kuona (2Kor 5:7).

Kwa miaka mingi ndugu mmoja aliazima gari, lakini mwenye gari hilo aliangukia kwenye nyakati ngumu na baraka ile ikaisha. Alisoma katika Kum 28:31 kwamba laana moja ya torati ni kwamba punda wako atachukuliwa na hatarudishwa. Akasema, “Kwa jina la Yesu nimebarikiwa”. Kwahiyo akaikataa hiyo laana na kumwomba Mungu ampe punda mpya. Kwa wiki kadhaa alitembea kila mahali akimshukuru Mungu moyoni mwake kwa kumpatia ‘punda’ mpya. Katika hali ya kawaida hapakuwa na tumaini la kupokea, lakini ghafla alipigiwa simu na kupokea gari kutoka kwa mwanamaombi aliyeongozwa na Mungu ili kumnunulia gari hilo.

6. Imani Ni Sasa

Katika Waebrania 11:1 utakuta imani ya ‘sasa’. Imani si kwamba Mungu anaweza, au kwamba atatenda jambo fulani, bali kwamba amekwisha kutenda. Imani halisi ni kwamba jibu tayari limekwisha kuwepo katika Mungu ‘sasa’, na baraka ni zangu ‘sasa’ hata kabla hazijaonekana au kupokelewa. Kwa mfano, si kwamba Mungu anaweza kuniokoa, au ataniokoa. Ndio, anaweza!

Ukweli Wenyewe Ni Kwamba:
Yesu tayari alishafanya wokovu pale Msalabani.

Ninagundua jambo hili kwa ufunuo,

Ninampokea, ninashukuru,

Na wokovu wake unakuwa wangu.

Halikadhalika, mlango wa uponyaji, wa kufunguliwa, wa baraka na maendeleo haupo katika nyakati zijazo, ukiamini kwamba Yesu anaweza, au hata atakutana na hitaji lako. Imani ya ‘sasa’ inaniwezesha kupokea kutoka Msalabani ambako kazi aliyoimaliza miaka 2000 iliyopita imekutana na kila hitaji langu! Mwamini, msifu, mshukuru, na kisha subiri kwa imani.

7. Imani Hukabiliana Na Kweli Na Kuamini

Kama Ibrahimu baba wa imani yetu alivyofanya kuwa mfano kwa wote watakaomfuata. Yeye ni baba wa imani yetu.  Soma habari hizi katika Warumi 4:19-21.

Baada ya Tomaso kusema, “Siamini”

Yesu alikuja na kumwambia, “Usiwe mwenye shaka, anza kuamini”. Tomaso alikiri kwa kusema, “Bwana wangu na Mungu wangu”. Alitubu kwa kutokuamini kwake, kisha akaenda kuhubiri India. Je, wewe ungependelea uwe nani, Ibrahimu au Tomaso? (Yn 20:24-29).

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

India (2)

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Bison Horn Maria (Dandami)

Maria, Dandami

150,000

Burig (Bhotia)

Purik

240,000

Chero

Chero

28,400

Churahi Pahari

Churahi

34,700

Dehati (Deshiya)

Maithili, Dehati

38,000

Dhanwar (Dhanvar)

Dhanwar

21,100






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk