1985 - 2007

 

30. Maono

Handel aliuona utukufu wa Mungu akatunga wimbo "The Messiah"

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Isaya 43:18;  Ufunuo 1:9-18;  1 Nyakati 28:11, 12

 

Mstari wa Kukariri
Pasipo maono, watu huacha kujizuia; bali ana heri mtu yule aishikaye sheria (Mit 29:18).

 

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Kwahiyo unaona nini? Washirikishe wenzio maono yako, mateso yako, kushindwa kwako, au kukosa maono. Muwe wazi.

 

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Uchunguze moyo wako mwenyewe na uone maono ambayo Mungu anaanza kukupa.
Usikubali kupokea mabaya, bali uyapokee yale yaliyo mpango wa Mungu na hatima yako, familia yako, huuduma yako, kanisa, na zama zijazo. Andika maelezo mafupi na kuyahifadhi mahali kwa ajili ya rejea miaka michache ijayo.

 

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Endeleza maudhui ya wale tai kwa maandishi. Ni kwa namna gani wanaweza kuathiri maono mapya kiutendaji? Je, ni nini kinachoweza kutokea?

 

Tafakari Andiko Hili
Kut 25:8

 

Tumia Dakika Moja Kuubadili Ulimwengu

Ombea taifa la Mexico. Idadi ya watu: 98,000,000, wengi wao ni maskini. Ni taifa linalokua, na lina matatizo mengi ya kijamii na ya kisiasa. Asilimia

88% ni Wakatoliki, na 5% ni madhehebu ya Kiinjili. Kuna historia ndefu ya mateso.

 

 

Yeremia alikuwa kijana mdogo tu alipoanza kutembea na Bwana akihudumu hekaluni. Siku moja Bwana alimtokea na kumwambia kwamba alimfahamu hata kabla hajazaliwa, na kwamba yeye alikuwa kijana maalum aliyetengwa na Mungu ili kuwa nabii. Yeremia alikataa kwa kusema kwamba yeye ni mtoto, lakini Bwana akamtia moyo na kumpa ahadi za mambo makubwa. Kisha Bwana akamwuliza swali (Yer 1:4-12).

 

Yeremia, Unaona Nini?

Yeremia akatoa jibu sahihi. Aliona dalili za kuwepo kwa maisha mapya kwa nchi yake.

Bwana akasema, Sawa, ninaliangalia neno langu ili kulitekeleza!

 

1. Je Wewe Unaona Nini Kutoka Kwa Bwana?

 

Ni nani awe na maono motomoto?

Ni kila mwamini peke yake, familia yake, huduma yake na hatima yake.

Ni kila kiongozi kwa ajili ya kanisa la Mdo 2:42-47 na  mahali na eneo lililopata kibali cha Bwana.

Ni kila kanisa kwa ajili ya ulimwengu wote.

Biblia inasema kwamba bila maono watu wataangamia (Mit 29:18). Na wa kwanza kuangamia anaweza kuwa ni wewe kwa kuchoshwa katika maisha yako ya kikristo.  Kuwa na maono ni zaidi ya kuwa na picha ya kusanyiko la ibada ya karismatiki. Huu ni ufahamu wa ndani wa kujua ni kwanini wewe umezaliwa sasa, na zaidi ya hilo, kwanini ni wewe na si wengine, waliozaliwa mara ya pili kwa mkono wa Mungu.

 

2. Maono Ni Unabii Wa Maisha Mapya Kutoka Kwa Mungu

 

Ni kuona japo kwa muda mfupi, mambo yajayo kabla hayajatukia, ilimradi tunamtii Mungu. Lakini tahadhari ni kwamba, Shetani anachukia ahadi ya maisha mapya. Alijaribu kumwua mtoto Musa ambaye hatimaye Mungu alimtumia kukomboa taifa. Alijaribu kumwua mtoto Yesu ambaye hatimaye Mungu alimtumia kuukomboa ulimwengu mzima. Leo hushambulia watoto wakiwa katika matumbo ya mama zao. Huwashambulia wakristo wachanga, na kwa mtindo huo hata maono mapya yatashambuliwa!

 

Maono Na Tai

 

Miaka kadhaa iliyopita tulikuwa tunasafiri jangwani huko Afrika Magharibi tukiwa njiani kuitembelea shule ya Biblia iliyokuwa ndanindani sana. Kwa mbali tuliwaona tai wakizungukazunguka hewani katika eneo fulani, na kwa ujuzi wetu wa kuangalia filamu za wachungaji wa ng’ombe wa nchi za Magharibi, tuliweza kugundua kwamba mahali hapo kuna kiumbe ama kinakufa au tayari kimeshakufa. Kinaweza kuwa ni kitu gani? Tulibadilisha mwelekeo na kufika mahali pale dakika chache baadaye.

 

Tai
Tulipowasili mahali pale tuliwakuta tai weusi wakubwa saba, wametua chini na walikuwa wakifuatilia kwa karibu kitoto cha mbuzi kilichokuwa kimezaliwa wakati huo na mama mbuzi alikuwa bado dhaifu kuweza kumtetea mwanaye. Tuliwafukuza tai wale hadi kitoto kile kilipopata nguvu za kukimbia chenyewe. Kwa kuwaangalia tu tai hao, tuliweza kupata picha ya nguvu za giza na jinsi zinavyoshambulia maono na mipango mipya iliyozaliwa. Biblia inaziita hizo nguvu za giza, ‘nyuni wa angani’. Tai hawa wataanza watakuandama mara tu unapokuwa umezaa mpango mpya. Lengo lao ni kushambulia maono yako na kukupa wakati mgumu wa kuanza na kusonga mbele.

 

3. Nyuni Wa Angani

 

Tai Namba 1 Anaitwa Kutokuamini
Huyu atakaa begani mwako na kulia tena na tena akikuuliza, “Je, una uhakika kwamba Mungu amesema hayo?"

 

Tai Namba 2 Anaitwa Shaka
Huyo anasema, “Usimtumaini Mungu wala mwanadamu; hata wewe mwenyewe usijitumaini”. Musa aliisikiliza sauti ya tai na kumwambia Mungu, “Mimi ni nani? Hawataniamini! Siwezi kusema! Tafadhali mtume mtu mwingine!”.

 

Tai Namba 3 Anaitwa Hofu
Huyo anasema, “Watu watasemaje iwapo utakosea, utabadilika njiani au kushindwa?”  Anasema wala usithubutu, haina uhakika.

 

Tai Namba 4 Anaitwa Kukatishwa Tamaa
Yoshua alitahadharishwa na Mungu kuhusu hawa tai weusi wenye sura mbaya (Yoshua mlango 1) (Kum 31:6).

 

Tai Namba 5 Anaitwa Uvivu
Hagai alimwona huyo tai, na kuwaambia watu wajitie nguvu na kufanya kazi (Hag 2:4).

 

Tai Namba 6 Anaitwa Vishawishi
Tai huyo ana uweza mkubwa wa kushawishi. Atakaa begani mwako na kukunong’oneza kuhusu mambo mengine ambayo unatakiwa uyafanye sasa. Lengo ni kukuondoa kwenye mpango wa Mungu (Lk 8:14).

 

Tai Namba 7 Anaitwa Kukosa Uvumilivu
Huyo ni msiri na katili. Kama akishindwa kupunguza kasi yetu kwa njia ya hofu, basi atatufanya tuende kwa kasi kubwa sana ili tumtangulie Mungu. Ikiwa imani ingegeuka kuwa jambo la kufikirika, maono yaliyokuwa yakiongozwa na Roho yatabadilika na kuwa matendo ya mwili ambayo hayatafanikiwa! Ni lazima kuchukua tahadhari kwa sababu huyo ni msiri na anaweza kujipatia ushindi dhidi yako kwa kukosa saburi.

 

Kwanini Tupate Mashambulizi Ya Namna Hiyo Kutoka Kwa Shetani?
Ni katika Mit 29:18. Hata kwa maono ya mtoto mchanga ni watu wachache tu watakaoangamia. Katika Mathayo 25 utakuta wale wanawali wenye maono ya kuwa tayari, watumwa wenye maono ya kutumia karama zao kikamilifu, na wanakondoo wenye maono ndani yao ya kuwahudumia wengine.

 

4. Kwahiyo Unaona Nini?

 

Je, inawezekana huna maono?

Kama hivyo ndivyo, fanya kile alichofanya Yohana, ingia katika Roho na kumwona Yesu! (Ufu 1:10).

 

Pengine unaona kidogo sana?
Je, maono yako hayakufanikiwa? Yazike kwenye kaburi la uhakika na tumaini la ufufuo bora (Mdo 16:6-10).

 

Je, Umeyakimbia Maono?
Kumbuka kwamba neno la Bwana lilimjia Yona mara ya pili; na Yohana na Marko pia (2 Tim 4:11).

 

Je, Unateseka Kwa Ajili Ya Maono?
Kumbuka Yusufu alikuwa na maono halisi, lakini aliteseka mwili na nafsi (Zab 105:19), na Habakuki pia aliteseka moyo na nafsi (Hab 2:3). Soma alichosema Danieli katika Dan 10:7,8,16,17. Ilibidi atiwe nguvu na Mungu ili aweze kusonga mbele. Kama ilivyokuwa kwa Danieli (Dan 10:14) uwe makini na wakati wa Mungu, muda uliyo sahihi ni muhimu.

 

Na Kwa Wengi Wenye Maono -
Fanya kama alivyofanya Ibrahimu katika Mwa 15:5-10;

Katika maono hayo ongezea hapo kujitoa mhanga kibinafsi.
Wafukuze nyuni wa angani (ms 11).
Mtazamie Mungu kuthibitisha maono yako (ms 13).

 

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

 

India

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Dhurwa (Parji, Thakar)

Duruwa

90,000

Dom Gypsy (Wogri Boli)

Domari

19,000

Gaddi (Pahari Bharmau)

Gaddi

88,000

Groma

Groma

14,000

Harauti (Hadauti)

Harauiti

886,000

Kahluri Pahari

Kahluri

66,200






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk