1985 - 2007

 

32. Kufanana Na Yesu

Tunda la Roho ni asili ya Mwana wa Mungu

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
1 Yoh 3:1-3;  Flp 2:1-11

 

Mstari wa Kukariri
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria (Gal 5:22, 23)

 

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, unaweza kuwaza kuhusu mtu ye yote unayemfahamu, au kwa kuangalia kwenye historia, au kutoka kwenye vyombo vya habari, anayeishi sikuzote maisha haya ya kufanana na Kristo?

 

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Tafakari kimyakimya maana ya kibiblia ya kila neno katika haya: upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, na kiasi.
Jichunguze misimamo yako mwenyewe na uone jinsi unavyoweza kufikia viwango vya juu kwa msaada wa Mungu.

 

Kazi Ya Stashahada
Andika aya tisa fupifupi ukionesha kutoka kwenye vitabu vya Injili mahali Yesu alipoonesha tunda la Roho

 

Tafakari Andiko Hili
2 Pet 1:3, 4

 

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Austria. Idadi ya watu ni 8,000,000. Asilimia

83% ni Wakatoliki. Kuna tatizo kubwa la uchawi, ulevi, na watu kujiua.

 Mungu anafanya kazi kubwa kuachilia ndani yetu tunda la Roho Mtakatifu, ambalo ni asili njema ya Yesu. Je, ni aina gani ya tunda analolitafuta katika maisha yetu?

 

1. Upendo, Lakini Wa Aina Gani?

 

Kuna aina nyingi za upendo kwa mfano kwenye Biblia tunakuta upendo wa familia au marafiki, upendo wa kuwa wa kwanza, upendo wa ndugu na dada, kupenda fedha, upendo wa mwanamke kwa familia yake, upendo wa mwanadamu na kupenda raha. Aina zote hizo ni za upendo wa kibinadamu, unaojulikana kama phileo. Lakini upendo mkuu wa Mungu una jina lingine, nalo ni agape. Anakupenda bila masharti, upendo wake hauongezeki wala kupungua kutokana na kushindwa au kushinda kwako. Anakupenda tu basi.

 

Mungu mwenyewe ni agape! (1 Yoh 4:8)

Kwa upendo huo alimpenda Yesu (Yn 17:26)

Mungu anawapenda watu kwa namna ileile na anaonesha upendo huo kwa kutoa zawadi ya Mwanaye (Yn 3:16) (1 Yoh 4:9, 10)

Baba anayo agape kubwa zaidi kwa wale wanaompenda Mwana wake Yesu (Yn 14:21)

 

Upendo Wa Agape Ukitenda Kazi

Wakati tulipokuwa bado wenye dhambi Kristo alitufia. Huo ni upendo wa agape (Rum 5:8).

Ona jinsi Yesu alivyoonesha kwa ukamilifu upendo wa agape katika Yn 13:1-34.

Yesu alituamuru kupendana, upendo wa agape, sisi kwa sisi, na kuwapenda watu wengine wote kwa upendo huohuo (Yn 13:34, 35) (1 The 3:12) (1 Kor 13:1-8).

 

Je, Maisha Yako Ya Upendo Yakoje?

Je, unalazimika kwenda ukisukumwa na agape? (2 Kor 5:14-20)

Jambo la kufanya na agape (1 Yoh 3:16-18)

Mahali pengine pa kupata agape (Rum 5:5).

 

2. Furaha, Ya Bwana

 

Yesu amepakwa mafuta ya furaha (Ebr 1:9). Yesu alifurahia watu, harusi, na tafrija. Neno katika Lk 10:21 aliruka kwa furaha, na kwa kuiona furaha mbele kulimsaidia Yesu kustahimili Msalaba (Ebr 12:2).

 

Kumfuata Yesu Kunaleta Furaha

(Lk 10:17) (Mdo 13:52)

Miji inaweza kupata furaha (Mdo 8:8)

Furaha ni lengo mojawapo la huduma (Flp 1:25) (2 Kor 1:24).

Yesu anataka uwe na furaha tele. Ukitaka kujua ni kwa namna gani, soma kutoka Yn 15:1-11).

 

3. Amani, Kama Mto

 

Maneno ya Biblia eirene na shalom yana maana ya utulivu katika taifa; hakuna vita hata baina ya mtu na mtu, kuna usalama, kuna kustawi, na furaha. Nafsi ya mtu aliyeokolewa ina amani na haihofii lo lote kutoka kwa Mungu, imeridhika na maisha, na imehakikishiwa uzima wa millele. Yesu ndiye Mfalme wa amani, naye huwapa amani watu wasiokuwa nayo. Hatushangai basi ni kwanini Paulo huanza nyaraka zake kwa maombi ya amani, eirene (Isa 9:6) (2 The 3:16) (Lk 7:50; 8:48).

 

Jinsi Ya Kuipata Amani Ya Mungu
Kutokana na ahadi  ya Flp 4:1-7 mahusiano yanakuwa mazuri.

Mtindo wa maisha wa kusifu katika mazingira yote.

Jua kwamba Bwana yu karibu kukutana nawe.

Usihofu, badala yake omba na kumwuliza Mungu.

Amani yake itaulinda moyo wako na ufahamu wako.

 

4. Nipe Uvumilivu, Sasa!

 

Hapa kuna neno makrothumia lenye maana ya ustahimilivu mwingi, uvumilivu, na uwezo wa kuzuia hasira yako kwa muda mrefu unapochokozwa. Neno hilo lina maana ya ustahimilivu tunaokuwa nao tunaposubiri kwa muda mrefu tukiwangojea watu wenye mioyo migumu waje kwa Kristo. Mungu naye anastahimili kwa muda mrefu wakati tunapochelewa kumjua (Rum 2:4; 9:22)

 

Kwa Imani, Na Kwa Uvumilivu

Tunapokea ahadi za Mungu (Ebr 6:12).

 

5. Fadhili Na Utuwema

 

Hapa kuna maneno mawili yanayofanana; chrestotes lenye maana ya utu wema katika kuhurumia, na la pili ni agathosune lenye maana ya kulifanyia kazi jambo lililo jema.

 

Yesu Alikuwa Mwema Na Alifadhili

Yeye alikuwa chrestotes, alionesha utu wema na huruma kwa yule mwanamke mwenye dhambi lakini aliyekuwa tayari kutubu. Lakini pia aliweka utu wema, agathosune, kwenye matendo alipolitakasa hekalu (Lk 7:37-50) (Mt 21:12, 13). Soma Mdo 10:30 ili uone vitu viwili vilivyosababisha Yesu atiwe mafuta.

 

6. Uaminifu

 

Yesu aliwaahidi wanafunzi wake kwamba atawatangulia kwenda Galilaya. Alionesha uaminifu kwa kuitunza ahadi yake, na neno lenye maana hiyo ni pistis. Kwa maana katika kulitunza neno lake Yesu alilazimika kupitia Gethsemane, kwenda Msalabani, kaburini, kuzimu, Mbinguni, kufufuka na hatimaye Galilaya (Mt 26:32).

 

Mpango wa Mungu Ni Kukufanya Wewe Uwe mwaminifu

Je, unaposema, ‘ndiyo’ unamaanisha, ‘ndiyo’? (Mt 5:37)

Je, unazitunza ahadi zako? (Zab 15:4)

Je, Mfalme atakuita wewe ‘mtumwa mwema na mwaminifu’? (Mt 25:21)

 

7. Upole

 

Neno praotes lina maana ya upole na unyenyekevu kama ule wa Yesu, unaotufanya sisi kukubaliana na yale yote Mungu anayotufanyia kuwa mema, hata kama hatuyapendi. Yesu ni Simba wa Yuda, lakini pia ni Mwanakondoo wa Mungu, mpole na mnyenyekevu mbele za Baba. Wenye upole wamebarikiwa (Mt 5:5). Tunapaswa kujifunza kutoka kwa Yesu (Mt11:29).

 

8. Je, Waweza Kuwa Na Kiasi?

 

Kama jibu ni ‘hapana’ basi unahitaji egkrateia, yaani kuwa na kiasi, ndiyo kusema uwezo wa kuudhibiti mwili wako dhidi ya tamaa.

 

Yesu Alijua Kusema Hapana!

Ukisoma kutoka Lk 4:1-14 utaweza kuona jinsi alivyojidhibiti mwenyewe katika kipindi cha udhaifu.

Wakati Yesu alipokuwa na njaa, Shetani alimwambia tumia vibaya uweza ulionao kwa hitaji lako binafsi la chakula. Yesu: HAPANA!

Shetani alimjaribu Yesu kwa kumpa njia fupi na rahisi ya kuukwepa Msalaba. Yesu: HAPANA!

Shetani alipendekeza njia ambayo Yesu angeweza kujipatia umaarufu haraka walipokuwa juu ya kinara cha hekalu. Yesu: HAPANA!

 

Tunahitaji Msaada Wa Mungu Ili Tuweze Kuwa Na Kiasi

Kuteka nyara fikira (2 Kor 10:5).

Kuufuga ulimi (Yak 3:8) (Mdo 2:4)

Kuidhibiti miili yetu (1 The 4:4)

 

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

 

India

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Multani (Siraiki Hindi)

Siraiki

20,000

Muria (Jhoria)

Muria, Western

12,900

Nahari

Nahari

19,000

Panika

Pamika

30,700

Pao

Pao

23,500

Saharia (Sor)

Saharia

174,300

Sondwari

Sondwari

31,500

 






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk