1985 - 2007
35. Mateso
Ni magumu, hata kwa Wakristo
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika Biblia Yako Soma
1Pet 4:12 – 5:11
Mstari Wa Kukariri
Lakini nawaambia, ‘Wapendeni adui
zenu, waombeeni wanaowaudhi; ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni;
maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na
wasio haki (Mt 5:44,45).
Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Mateso yenu wenyewe, na kisha
mwombeane ninyi kwa ninyi, na kufarijiana kila mmoja na mwenzake.
Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana
Tena
Watafute, wafariji, na kuwatia
moyo watu wanaoteseka kwa umaskini,
kutengwa, magonjwa kama ukimwi, na walio kifungoni. Jipatie rafiki angalao mmoja
kutoka kila kundi.
Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Elezea kwa undani zaidi zile
sababu tatu zinazosababisha kuwepo na mateso, na kisha uone kama unaweza kupata
nyingine zaidi
Tafakari Mistari Hii
Lk 6:20-23
Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Libya. Idadi ya watu ni 5,500,000. Asilimia
97% ni Waislamu; Asilimia 3% ni Wakristo wa mataifa ya nje. Hakuna injili ya waziwazi.
Mateso yanamgusa kila mmoja wetu na kwa wengine yanaweza kuendelea hata kwa miaka kadhaa kutokana na magonjwa, ajali, au kuumia kimawazo kunasababishwa na kukata tamaa na huzuni kubwa. Vifo, kukosa ajira, na usaliti ni vitu ambavyo kwa kweli vinatia uchungu vinapotokea kwenye ndoa, familia au kanisani. Umaskini nao huleta mateso kwa kusababisha ukosefu wa chakula, maji safi, na madawa. Kadhalika siasa au dini huweza kusababisha mateso makubwa kutokana na matumizi mabaya, kutotendewa haki, kukosekana usawa, na kutengwa.
1. Mungu, Uko Wapi?
Mateso ni halisi, na ili Mungu awe Mungu ni lazima awe Mwenyezi na hujidhihirisha mwenyewe kama Mungu wa upendo. Wanadamu wamekuwa wakipambana na hali hii kwa miaka mingi.
Mwandishi wa vitabu Steven Chalke
Aliwahi Kuandika Haya:
" Pengine Mungu anataka kufanya
jambo fulani, lakini anashindwa. Pengine kukomesha umaskini wa dunia ni kazi
kubwa sana inayomshinda. Kama hivyo ndivyo, basi huyu si Mwenyezi. Pengine Mungu
mwenyewe ni Mwenyezi, lakini hajali sana kukomesha mateso ya watu. Kama hivyo
ndivyo, basi Mungu huyo hana upendo. Lakini pengine Mungu huyo anajali, na ni
Mwenyezi, lakini kwa mtazamo wake wa muda mrefu haoni kama mateso na uovu ni
halisi, au kuwa ni tishio kama sisi tunavyoona. Pengine haya yote ni sehemu tu
ya mchakato wa mafunzo kabambe. Kama hivyo ndivyo, basi mateso na uovu si
halisi.
Je, Kuna Jibu Lo Lote?
Watu wengine wanasema kwamba
kupata mateso si jambo baya sana; wengine wanasema ni sehemu tu ya picha kubwa
zaidi ya kutusaidia kujifunza; wengine wanasema ni matokeo ya dhambi za watu
wenyewe; na wengine pia wanasema kwamba mateso yanasababishwa na Shetani katika
vita vya kiroho. Majibu haya kwa pamoja yanaonekana kutoa sehemu tu ya maelezo,
lakini hatuwezi kuelewa mpaka Yesu atakapotoa maelezo sahihi huko mbinguni.
2. Tunajua Sababu Tatu
Ulimwengu Uliopotoka
Kwanza,tunaishi kwenye ulimwengu uliopotoka, ambao umeathiriwa sana na dhambi kutoka anga za juu sana mpaka duniani, vitu vidogo sana na vya ngazi za atomiki na hii inakuwa ni sababu ya madhara ya hali ya hewa, maafa ya asili na matatizo ya kiafya katika miili yetu.
Hiari Ya Mwanadamu
Pili, hiari ya mwanadamu, ambayo ni uwezo aliopewa na Mungu wa kuchagua jema au ovu. Matumizi ya uwezo huu yamemsababishia mwanadamu mateso makubwa, na Mungu amejizuia ili kuheshimu uhuru wa mwanadamu wa kuchagua.
Shetani Mwovu
Shetani ni mwovu, na ili uovu upate kushamiri watu wema wanatakiwa kukaa kimya bila kufanya lo lote. Luther King aliwahi kusema, “Kufikia mwishoni mwa karne ya 20 wengi wetu hatutatubu kwa uovu mwingi tulioufanya, lakini ile hali inayotuzuia sisi kufanya cho chote”.
3. Yesu Aliteseka Na Aliteswa
Watu wake mwenyewe hawakumpokea, walimtukana, walikula njama dhidi yake, walimtesa na hatimaye wakamwua kwa mateso makali ya aina yake; baada ya kesi iliyoendeshwa kimizengwe mizengwe, ikiwa na mashahidi wa uongo, haikusikilizwa na jopo, hapakuwa na utetezi wala huruma. Soma (Zab 69:20) (Isa 50:6; 53:5) (Zek 13:6) (Mk 15:34) (Lk 22:44) (Ebr 2:10; 5:8; 13:12) (1Pet 1:11; 2:21; 3:18).
4. Paulo Aliteseka Na Aliteswa
Kama ilivyokuwa kwa wafuasi wa Yesu na
watu wa Mungu wengi wa zama za kale
(Mdo 9:29; 13:50; 14:5,19; 16:22; 18:12; 21:36; 22:22; 23:10) (1Kor 4:12) (2Kor
4:9; 11:24) (2Tim 2:9; 3:11).
Hatutazamii Tofauti Yo Yote
Yesu alisema, "Mtumwa hawi mkuu
kuliko bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na ninyi pia. Ulimwenguni
humu mnayo dhiki. Lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu (Yn 15:20;
16:33). Paulo alisema, “Kila mtu anayetaka kuishi maisha ya kimungu katika
Kristo Yesu atateswa” (2Tim 3:12). Katika vizazi vyote waamini wameteswa na
kuuawa kwa kumfuata Kristo, hata huko Rwanda na Iran mwaka 1997. Hata leo yapo
majaribu ambayo waamini wanapaswa kuyastahimili kwa ajili ya Kristo.
Kuteswa, Mdo 9:16.
Maudhi Na Chuki, Mt 5:11; 10:22.
Kupoteza Nafsi, Mt 10:39.
Kupoteza Mali, Jamaa, Mt 19:29.
Kupoteza Hadhi 1Kor 4:10; 2Kor 4:5.
Mauti, 2Kor 4:11; 12:10; Flp 1:29.
Je, Tunamtii Mungu Au Mwanadamu?
Jibu kutoka kwa kanisa linaloteseka, kwanza kabisa ni kulitii neno la Mungu. Na ikibidi tukubali adhabu inayoweza kutolewa na mwanadamu kwa ajili ya kumtii Mungu (Mdo 5:29; 4:19).
5. Jinsi Ya Kushinda Mateso
Shukuru katika mazingira yote.
Msifu Mungu katika mazingira yote (1Pet 4:12-19).
Omba kila wakati, kata rufaa mbinguni ili upate haki yako kutoka kwenye mahakama iliyo kuu kuliko zote.
Wasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.
Pigana vita vya kiroho, kwa kuwa mapambano yetu si dhidi ya nyama na damu (Efe 6:12).
Pengine Mungu anaweza akaamua kutuma tetemeko la ardhi kama alivyofanya kule Filipi ili kuwatoa gerezani Paulo na Sila; au akatuma malaika kama alivyofanya kwa Petro na kumtoa gerezani; au akaamua kutembea na wewe motoni (Mdo 16:25-30; 12:1-12) (Dan 3:24,25).
Ushauri Kutoka Kwenye Biblia
Tunapaswa kuwapenda adui zetu
Tunapaswa kuwabariki wale wanaotulaani.
Tunapaswa kuwatendea mema wale wanaotuchukia.
Tunapaswa kuwaombea wale wanaotutesa.
Usilipize ubaya kwa ubaya.
Wahudumie wanaoteseka.
(Mt 5:43-48) (Kut 23:4, 5) (Ayu 31:29) (Mit 24:17; 25:21, 22; 20:22; 24:29) (Mt 5:39-44) (Rum 12:14-21) ( Lk 6:27,35; 23:34) (1The 5:15) (Mdo 7:60) (Law 19:18) (1Pet 3:9) (1Pet 5:9-11).
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Ambao Hawajafikiwa Na Injili Hapa Ulimwenguni, Ukiwataja Kwa Majina
Iran | ||
Jina la watu |
Lugha yao |
Idadi yao |
Gilaki |
Gilaki |
2,400,000 |
Gurani (Bajalani) |
Bajelan |
20,000 |
Gurani (Bajalani) |
Hawrami |
18,000 |
Harzani |
Harzani |
24,000 |
Hazara (Khawari) |
Hazaragi |
604,000 |
1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya
for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk