1985 - 2007

 

36. Mamlaka

Chifu bado ni mtu mwenye mamlaka juu ya watu wake barani Afrika

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Mt 8:5 -13;  1Pet 5:1-11

Mstari wa Kukariri
Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi (1The 5:12, 13).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
 Unajisikiaje kuhusu mamlaka na unyenyekevu? Je, hivyo ndivyo unavyopaswa kujisikia?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Watembelee watu wenye mamlaka ya juu unaoweza kuwafikia katika mamlaka ya mji, au kwenye jeshi la polisi, au viongozi wa kijiji, na wachungaji, na uwahakikishie kwamba utawaombea. Waulize mahitaji yao ili upate kuwaombea. Unaweza ukashangaa namna watakavyofurahia jambo hilo.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika orodha ya mamlaka kuu zilizoko katika taifa lako ukianzia na mkuu wa nchi kushuka chini hadi kufikia mjumbe wa nyumba kumi. Waandikie kuwaambia kwamba unawaombea.

Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Kut 20:12.

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Afghanistan. Idadi ya watu ni 23,000,000. Kuna makabila 41. Asilimia 99% ni Waislamu. Wakristo wanaweza kufikia 1000 tu. Nchi imekumbwa na vita na mavamizi.

 

Mamlaka ni moja ya maneno yasiyoeleweka vizuri na kutumiwa vibaya katika kanisa katika siku zetu. Kunaweza kukawa na msisimko mkubwa! Mchungaji Rick Godwin anafundisha kwamba ziko aina saba za mamlaka zinazotugusa; nazo ni:

Mamlaka Kuu Ya Mungu
Hii ni mamlaka tunayoitii bila kuuliza swali (Isa 9:7) (Efe 1:22) (Flp 2:9-11).

Mamlaka Ya Neno La Mungu
Maneno hayo yana uzito sawa na Mungu mwenyewe (Yn 17:17). Tunapata neno la Mungu lisilobadilika kutoka kwenye kweli ya Biblia (Yn 1:1; 14:6) (2Tim 3:16). Hakuna mabadiliko, neno la Mungu linabakia vivyo hivyo milele. Jumbe za kinabii zaweza kuwa za kweli, lakini haziwezi kuwa kama neno la Mungu lililoandikwa.

Mamlaka Ya Dhamiri
Dhamiri ni zawadi ya Mungu kwa ajili yako, isikilize. Uwe makini na utamaduni, ubaguzi au pendeleo zinazokujia katika maneno ya kiroho kuhusu mambo yale ambayo hayakushughulikiwa moja kwa moja katika Biblia, kwa mfano elimu kuhusu genes ambazo ni sehemu za chembechembe ndogo za viumbe hai yaani cells, na nguvu za nyuklia (Rum 2:12-16; 14:1-23).

Mamlaka Zilizokasimiwa Kwa Wanadamu Na Mungu
Sasa kwa mara ya kwanza mamlaka ya Mungu inapitia kwenye kinywa cha mwanadamu (Efe 4:11) (Ebr 13:7, 17).

Mamlaka Ya Maagano Ya Kisheria
Ndiyo yetu na iwe ndiyo, na hapana yetu pia iwe hapana (Mwa 29:18-30).

Mamlaka Ya Mila Na Utamaduni
Yawezekana namna wanavyofanya mambo yao si kama wanavyofanya kule ulikotokea wewe, uwe mwangalifu basi kama unajaribu kuwabadili ili kwamba wafanye kama unavyotaka wewe (Mwa 29:26) (1Kor 11:16).

Mamlaka Ya Kiutendaji
Hii ni mamlaka ya uwezo, kwa mfano katika ajali ya barabarani daktari anaweza kumsaidia majeruhi, fundi makanika akatenganisha magari, polisi akaelekeza magari, na mtume mkuu mwenye mamlaka yawezekana hata asitafutwe kwa ushauri kwa sababu kiutendaji hakuna ajualo! (Efe 5:21).

1. Mstari Utokao Mbinguni Mpaka Duniani

Mamlaka ya Mungu iliyokasimiwa inashuka kutoka juu kuja chini na kuwafikia hata watoto wachanga. Po pote mamlaka ya Mungu inapojitokeza ufalme wa Shetani unaondoka, na badala yake utawala wa Mungu unadumu katika maisha ya watu.

Hapo mwanzo Mungu, (Mwa 1:1) (Zab 90:2) (Yak 4:7) (Ebr 12:9).

Mamlaka yote amepewa Yesu (Mt 28:18) (Zab 2:2) (Ebr 5:9) (Yn 13:13).

Yesu anakasimu mamlaka kwa Viongozi wake ili walinde, waelekeze, wadhibiti na kulisha kundi lake (na si lao), (Efe 4:11) (Ebr 13:17).

 

Tunaambiwa pia:
Kutii Serikali (Rum 13:1-7) (Tito 3:1).

Wake kuwatii waume zao (Kol 3:18) (Efe. 5:24).

Kutii wazazi (Efe 6:1-4) (Kol 3:20).

Kutii waajiri (Kol 3:22).

Kuwatii waamini waliokomaa (1Kor 16:16).

Kuwatii wazee (1Pet 5:5).

Kunyenyekeana (Efe 5:21).

 

Kuondoka kwenye mstari wa Mungu kunaweza kuwa na maana ya kukosa nguvu na kutengwa. Chukua tahadhari!

2. Jinsi Ya Kuwatambua Viongozi Wabovu

Kiongozi mbaya huwafanya watumwa wale anaowaongoza, anawanyonya, na kwa kufanya hivyo hujipenyeza na kwenda mbele, na kuwapiga kofi la uso (2Kor 11:7-11, 20).

Kiongozi mtumishi wa Mungu hujidhili, na kuwakweza wengine, anahubiri Injili bila malipo, anawatumikia, anawapenda, na hawi mzigo kwa ye yote (1Pet 5:2-4).

3. Mamlaka Ina Maana Ya Uwajibikaji

Kuaminika na kupewa mamlaka kutoka kwa Mungu maana yake ni kufanya yale Mungu anayofanya na kuwajibika. Mhubiri anayewatembelea na ambaye hawajibiki kwa kanisa lo lote, hana mamlaka ya moja kwa moja kwa kanisa. Na vilevile mume asiyewajibika kwa mkewe hana mamlaka juu ya mkewe. Halikadhalika sisi hatuwezi kuwa na mamlaka juu ya mji kwa ajili ya Kristo kama hatutawajibika kwanza kuupenda mji huo.

4. Je, Kunyenyekea Maana Yake Nini?

Biblia imetumia maneno tofauti kama hupotasso ambalo ni neno la kijeshi lenye maana ya kuingia kwenye mstari; au hupeiko lenye maana ya kurudi nyuma, kukubali kutenda jambo ambalo hukutaka kulitenda, kunyenyekea; na hupakouo, lenye maana ya kusikiliza, kuhudumia na kutii. Neno lingine maalum ni peitho lenye maana ya kushawishiwa au kupatikana, kama lilivyotumika katika Ebr 13:7 na Yak 3:3.

Mifano Ya Unyenyekevu Katika Biblia
Kristo anamnyenyekea Mungu kwa furaha (Yn 6:38; 4:34; 5:30; 12:49)

Yule Kamanda wa jeshi mwenye uwezo alinyenyekea kwa upole mbele za Yesu (Mt 8:8)

Daudi anamnyenyekea Sauli hata katika wendawazimu wake (1Sam 24:6)

Viongozi wa kanisa walinyenyekeana na kuheshimiana (Mdo 15:2-6, 22)

Paulo mtume aliwanyenyekea viongozi wa kanisa (Mdo 11:1-4; 18:22)

5. Kwanini Ni Vigumu Kuheshimu Mamlaka?

  1. Kutaka uhuru kutoka kwenye mamlaka imekuwa ni tabia ya kila mwanadamu tangu anguko.
  2. Uchu wa madaraka na udhibiti ni tabia ambayo pia iko ndani ya kila mwanadamu, hata ijifiche namna gani.
  3. Mababa wakatili na wanaopenda kudhibiti sana wanatuumiza.
  4. Mababa wadhaifu wametoa mwanya kwa wamama kutupa mfano mbaya.
  5. Kukosekana kwa baba ama kwa kifo au talaka, au kuwepo kwa ‘mababa’ wengi kumeharibu heshima.
  6. Matumizi mabaya ya mamlaka shuleni, au jeshini, au hata kanisani kunatufanya kuwakwepa watu wenye mamlaka.

Jawabu la matatizo haya si kuwa na msimamo wa kukataa mamlaka. Njia bora ni kumtafuta mtu halali wa Mungu mwenye mamlaka unayeweza kumwamini na kumheshimu. Mtu anayeweza kukupenda na kujenga upya kuta zilizobomoka ili kukujengea tena imani na kujiamini.

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Iran

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Herki

Herki

18,000

Karingani

Karingani

15,000

Khorasani Turk

Khorasani Turkish

400,000

Parsee

Parsi-Dari (Parsee-Dari)

2,000,000

Pushtun, Pathan, Afghan

Pashto, Western

79,300

 






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk