1985 - 2007

 

37. Upendo

Upendo maana yake ufanye jambo fulani

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Efe 5:21 – 6:9

Mstari wa Kukariri
Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi (Yn 13:35).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, ni lugha gani ya upendo unayoifahamu vizuri zaidi?
Bila shaka watu wanatofautiana!

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Fanya utafiti kwa kutazama, kwa kusikiliza, na kwa kuuliza; ili upate kujua ni lugha gani ya upendo ambayo watu unaowafahamu wanaielewa na unapata jibu unapoitumia k.m. mkeo, mumeo, wazazi, na marafiki. Tenda jambo fulani, au sema neno fulani litakalowajaza furaha maishani mwao kwa kutumia aina ya lugha ya upendo wanayoifahamu vizuri zaidi!

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Kama ungekuwa mchungaji ungewezaje kuhakikisha kwamba zile lugha tano za upendo zinanenwa kwa watu wako? Je, ungeweza kunena nao kwa njia zipi? Andika maelezo ya kurasa mbili.

Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Efe 4:26

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Hungary. Idadi ya watu ni 11,000,000.

Panahitajika tena uamsho kama siku za nyuma. Asilimia 62% ni Wakatoliki, na 25% ni Waprotestanti.

 

Jifunze kuziweka pembeni tamaa zako ili kwamba uweze kuwa na saburi na uadilifu, na kwa furaha umwache Mungu akuambukizie tabia yake. Hilo litakuwezesha kupiga hatua inayofuata, yaani kuwafurahia watu wengine na kuwapenda; na hatimaye upendo wako kwao utakua sana (2Pet 1:6-8).

Katika 1Kor 13:1-13 Paulo anaelezea upendo halisi, kwamba upendo ni katika matendo kwa utukufu wa Mungu, na si misisimko tu kama tunavyoona kwenye filamu siku hizi.

1. Upendo Ndio Unaotufanya Sisi Kuwa Watu Maalum!

Mungu si kwamba tu ana upendo, au anagawa upendo, lakini yeye mwenyewe ni upendo, ndiyo asili yake, na tabia yake, na kuwako kwake. Na sisi kama familia yake tunaonekana tofauti wa watu wengine wote kwa sababu ya uwepo wake katikati yetu, na kwa asili yake ya upendo anaouonesha, kupitia kwetu, kwa ulimwengu ambao kwa kawaida watu hujipenda wenyewe, na kuwapenda wapenzi wao na wale tu walio karibu nao.

Ama Ni Upendo Au Si Cho Chote

Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi (1Kor 13:1,2).

Je, Tumpende Nani?

Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Jirani yetu kama nafsi zetu.

Tujipende wenyewe.

Washirika wetu katika ndoa.

Ndugu na dada katika Kristo.

Wazazi wetu (Efe 6:2) (1Tim 5:4).

Watumishi wa Mungu (1The 5:13)

Wananchi wenzetu (Rum 9:3; 10:1)

Wageni (Law 19:34) (Kum 10:19).

Hata adui zetu (Mt 5:44).

Na watu wote po pote walipo (Gal 6:10).

2. Je, Tutawezaje Kuwapenda Watu Wote Hawa?

Na ashukuriwe Mungu kwa kuwa tunao msaada tunaouhitaji kwa sababu Paulo anatuambia Mungu huumimina upendo wake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetupa sisi. Tutaweza kupenda kama yeye kwa kutumia upendo wake, maana upendo wetu hata ungekuwa mkubwa kiasi gani, kamwe hautoshi (Rum 5:5).

3. Kwanza Kabisa Tunataka Kumpenda Mungu

Katika Marko 12:30, Yesu anasema amri iliyo kuu na ya kwanza ni kumpenda Bwana Mungu wetu, kama ifuatavyo:

Kwa Moyo Wetu Wote,

Moyo au roho, ndicho kituo cha uhai wenyewe.

Kwa Nafsi Zetu Zote,

Ndiko kwenye tamaa, kutaka, na hisia.

Kwa Akili Zetu,

Ndiko kwenye ufahamu na mawazo.

Kwa Nguvu Zetu,

Ndiko kwenye uwezo na nguvu za kimwili.

4. Kumpenda Mungu Maana Yake Ni Kuwapenda Majirani

Na ya pili inafanana na ya kwanza, ‘…Mpende jirani yako kama nafsi yako…’(Mk 12:31). Kwa namna ileile tunavyojitunza na kujipatia mahitaji yetu vivyo hivyo tuwafanyie jirani zetu.

Je, Ni Yule Aliye Jirani Na Nyumba Yako?

Kufuatana na neno alilolitumia Yesu alimaanisha ni pamoja na mtu mwingine ye yote bila kujali taifa lake au dini yake, iwe tunaishi jirani au hata kama tumekutana tu. Soma habari kamili za yale yaliyotokea kwenye Barabara ya Yeriko katika Lk 10:25-37.

5. Kumpenda Mungu Maana Yake Ni Kujipenda Mwenyewe

Yesu alisema ni lazima ujipende, lakini ni vigumu sana kwa baadhi ya watu wanaojisikia kwamba hawakuwahi kupendwa katika utoto wao. Pengine inawezekana walipendwa sana lakini hawakuhisi kupendwa. Kama hujifikirii sana mwenyewe hebu jitazame tena mwenyewe kutoka juu, kwa mtazamo wa Mungu. Angalia ni kiasi gani Mungu anachokupenda, kiasi cha kutosha kumtuma Mwanaye afe badala yako ili wewe udumu katika pendo lake milele.

Amekubariki.

Amekuchagua.

Anakupenda.

Amekukubali na kukufanya wake.

Amekununua kwa bei kubwa sana.

Amekusamehe.

Amekukirimia utajiri wa neema yake, hekima, uelewa na maarifa, na Roho Mtakatifu pia (Efe 1:3-14).

Ndiyo, wewe huna thamani yo yote, lakini mbele za Mungu una thamani kubwa. Ukijua kwamba Mungu anakupenda kiasi hicho, itakusaidia wewe kujipenda mwenyewe. Wewe ni muhimu kiasi hicho.

6. Na Washirika Wa Ndoa

Waume wanapaswa kuwapenda wake zao, na wake wanaweza kufundishwa kuwapenda waume zao (Efe 5:25) (Tito 2:4).

Je, Ni ‘Lugha’ Gani Ya Upendo Unayotumia?
Je, ulijua kwamba waume na wake wana mahitaji tofauti ya upendo, na kwamba wana miitikio tofauti kwa ‘lugha’ za upendo? Mke anapokosa kuisikia ‘lugha’ yake, ndipo hapo anapojisikia kutokupendwa, ingawa kwa kweli anapendwa. Halikadhalika kwa waume. Kama unaijua ‘lugha’ anayoielewa vizuri zaidi mshirika wako inene hiyo mara kwa mara.

‘Lugha’ Tano Za Upendo Ziko Hapa:

Maneno ya kusisitiza – Yanatamkwa kila mara.

Muda mwafaka – Uliokuwa unangojewa kwa hamu kubwa na wengi.

Kupokea zawadi – Kunasema mengi kwa baadhi ya watu.

Matendo ya huduma – yanaonesha upendo wako.

Kuguswa – Wengine wanapenda kuguswa miili yao.

7. Na Kuwapenda Ndugu

Soma tena andiko lenye uweza, mstari wako wa kukariri katika Yn 13:35. Soma pia Ebr 13:1 na 1Yoh 4:7.

Usimpe Ibilisi Nafasi

Tofauti zinaweza kujitokeza miongoni mwa watu lakini msimruhusu Shetani kutumia nafasi hiyo. Kila mara hakikisha mmepatana kabla hakujakuchwa (Efe 4:26). Mungu ametuwekea njia rahisi ya kutatua migogoro na kushughulikia suala la dhambi bila kusababisha kashfa. Katika utaratibu wa mapatano ulioko katika Mt 18:15 -18, Mungu amelenga kuzuia kusambaa kwa habari ya dhambi na kumpata ndugu yako, na wala si kujipatia alama za ushidi dhidi yake.

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Iran

Punjabi

Panjabi, ya Mashariki

24,000

Shikaki

Shikaki

24,000

Tat, Mussulman

Tat, Mussulman

31,000

WaUrdu (Islami, Undri)

Urdu

60,000

Vafsi

Vafsi

18,000

 






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk