1985 - 2007
38. Mrejeshe Mfalme
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika Biblia Yako Soma
Yeremia 8:20; Mathayo 13.
Mstari wa Kukariri
“…Ufalme wa dunia umekwisha kuwa
ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele”
(Ufu 11:15).
Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Ni ishara gani za nyakati
unazoweza kuziona hapa duniani? Ni matukio gani unayoyaona kwenye magazeti na
kwenye TV ambayo yametabiriwa kwenye Biblia?
Jambo La Kufanya Kabla
Hatujakutana Tena
Je, umebarikiwa na mafunzo haya?
Kama umebarikiwa basi omba nafasi makanisani na kuwafundisha watu kile
ulichokipata. Wakaribishe katika vipindi utakavyoandaa au waelekeze jinsi ya
kuanzisha vikundi vyao.
Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Chunguza andiko hili, 2Pet
3:10-17, na kisha andaa orodha ya majibu kumi kwa swali lifuatalo kwa kuzingatia
kwamba Bwana anakaribia kurudi. “Sisi tunapaswa kuwa watu wa aina gani?
Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Ufunuo 22: 20.
Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Kongo (DRC). Idadi ya watu: 42,000,000 katika makabila 450.
Asilimia 21% ni madhehebu ya Kiinjili; asilimia 42% ni Wakatoliki
Wakati huu Mfalme wetu Yesu hayupo pamoja nasi, yupo mbinguni na anasubiri wakati wa Mungu ufike ili arejee kuja kuutawala ulimwengu kwa haki. Kila mmoja anataka kujua ni lini. Katika Mdo 1:7 Yesu alisema, “…Si kazi yenu kujua nyakati wala majira…”, lakini ametupa viashiria vingi vinavyotufanya tuelewe majira ambayo Bwana anatazamiwa kurejea.
1. Kuna Ishara Duniani
Awali ya yote, nabii zote zinazomhusu Mfalme ni lazima zitimilizwe. Yesu alituambia habari za matukio ya ulimwengu yatakayopelekea kurudi kwake, na kwa kadiri siku za mwisho zinavyozidi kupungua ni lazima tutazamie kuona ishara hizo kwa kiwango kikubwa (Mt 24:3-51) (Mk 13:1-37) (Lk 21:5-36).
Taifa Litainuka Juu Ya Taifa Jingine
Neno taifa ni ethnos lenye
maana ya kundi la watu. Na ingawaje vita vya ulimwengu vimemalizika, lakini vita
baina ya vikundi vya kikabila vinaendelea katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa
mfano Bosnia, Chechenya, Afghanistan, na Rwanda.
Maafa Yataongezeka
Kuongezeka kwa njaa, magonjwa,
matetemeko ya ardhi na vimbunga ni ishara za ule mwisho.
Matukio Ya Kutisha Na Ishara Kuu
Madhara hayatakosa kuja, pengine
yatasababishwa na uchafuzi wa mazingira unaotokana na milipuko, uharibifu wa
misitu, ajali za nyuklia, au tofauti kubwa iliyopo kati ya maskini na matajiri.
Baadhi ya manabii wanadhani kwamba matajiri wa Magharibi wanakaribia mwisho wa
miaka ya ng’ombe wanono wa Yusufu (Mwa 41:17-40) na kwamba miaka ya ng’ombe
waliokonda imekaribia. Wale ng’ombe waliokonda waliwameza wale walionona na hili
linawakilisha hazina za kitaifa, lakini walikuwa wamekonda. Na kama ilivyokuwa
wakati wa Yusufu, watu wanaweza kujikuta kwenye utumwa wa madeni bila fedha,
bidhaa za kununua na kuuza, au ardhi, na ni lazima aje Mwokozi kama Yusufu.
Matukio Makuu Ya Kiroho
Yapo matukio ya kweli ya uamsho
yanayoendelea kadiri Roho wa Mungu anavyotembea katika juhudi za kuleta mavuno
kwa ajili ya Yesu. Yapo pia matukio ya uamsho usiokuwa wa kweli yanayoendeshwa
na mapepo wachafu katika juhudi za kuvuruga kazi ya Mungu.
Israeli Ni Ishara Dhahiri Hapa Duniani
Baada ya miaka 1,900 ya
kutawanyika duniani bila makazi, watu wa Mungu, Wayahudi, ambao pia
hawakupendwa, wamerudi kwenye nchi yao kama ilivyotabiriwa (Amo 9:8-15).
Mihuri, Tarumbeta, Magojwa Na Bakuli
Saba kwa kila moja ya haya
yanapatikana katika Ufunuo mlango wa 6 hadi wa 16, ambako tunaelezwa kuhusu
matukio ya ghafla na ya ajabu hapa duniani. Lakini usijali, tazama juu! Hayo
yote yanaashiria kurudi kwa Yesu ambako kutakuwa utatuzi wa masuala mengi, na
jibu la maombi ya mamilioni wa watu ulimwengu mzima (Lk 21:25,26).
2. Kuna Ishara Katika Ufalme
Ufalme ni pale Mfalme anapotawala. Tunamwomba Mungu, “Ufalme wako uje”, na vitendawili vya Ufalme kwa mfano Mathayo 13 inatuonesha namna mambo haya yanavyotokea. Kutoka kwa marafiki wachache waliokuwa katika eneo la Msalaba, leo mamilioni ya watu kwa uaminifu na kwa furaha wamemfanya Yesu kuwa Mfalme wao.
Mfalme Anakuja
Kanisa Linajengwa
Yesu aliahidi kwa upendo mkuu
akisema, “Nitalijenga kanisa langu” (Mt 16:18) (Efe 5:27), na ndicho kitu hasa
anachokifanya siku hizi. Zaidi ya asilimia 50% ya watu waliowahi kuokoka,
wameokolewa tangu mwaka 1900 na wengi wa hao ni kuanzia mwaka 1950. Watu 70,000
humpa Yesu maisha yao kila siku duniani kote. Mikutano mikubwa ya injili
imewaleta kwa Yesu mamilioni ya watu kutoka Amerika Kusini, Afrika kusini mwa
jangwa la Sahara, na sehemu za Russia, Uchina na Korea ya Kusini.
Inafanyika Toba Ya Kitaifa
Watu wanapotubu kwa ajili ya
dhambi za taifa lao wanahimiza kurudi kwa Mfalme. Kwanini? Katika Mdo 3:13 Petro
anawatuhumu watu wake kwa kumwua Yesu. Lakini kwa ukweli sio wao hasa waliotenda
jambo hilo, bali viongozi wao. Petro akasema kwamba kama tutajihusisha na dhambi
za mataifa yetu, na kutubu kwa niaba yao, na kumgeukia Mungu kwa niaba yao,
Mungu atafanya yafuatayo (Mdo 3:19,20):
Utekelezaji wa Agizo Kuu Unasonga Mbele
Katika Mt 24:14 Yesu anasema
kwamba ule mwisho hautakuja hadi injili hii itakapokuwa imehubiriwa katika
mataifa yote. Neno mataifa hapa, ethnos, halina maana ya mataifa ya
kisiasa mathalani India, lakini makundi ya kikabila, ambayo watu wake
wameunganishwa na lugha moja na utamaduni mmoja. Miaka 200 iliyopita makumi ya
maelfu ya mataifa yalikuwa hayajafikiwa kabisa; hata kufikia mwaka 1900, idadi
ilikuwa bado ni ndogo. Leo hii wasomi wa masuala ya Umisheni wanajua idadi ya
mataifa yaliyobakia ni kama 7,000 tu. Wanayajua mataifa hayo kwa majina na
mahali yalipo. Mipango ipo na maombi yanafanyika ili kuwafikia wote.
3. Kwahiyo Sisi Tunapaswa Kuwa Watu Wa Namna Gani?
Katika 2Pet 3:10 -18 tunaambiwa kwamba kwa kuzingatia ujio wa siku ya Bwana, tunapaswa kuwa watakatifu, bila doa, bila lawama, tukihimiza kurudi kwake, tukikesha, tukisimama imara bila kuchukuliwa na mafundisho potofu, tukikua katika neema na katika kumjua Yesu.
Je, Tunaharakishaje Ujio Wa Siku Hiyo?
Kwa kuomba na kuutumikia Ufalme
kwa njia ya kulijenga Kanisa, tukiziungama dhambi za taifa letu, na kukamilisha
utekelezaji wa Agizo Kuu.
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina
Iraq | ||
Jina la watu |
Lugha yao |
Idadi yao |
Anatolian Turk |
Turkish |
22,000 |
Bajelan (Shabak, Gura) |
Bajelan |
20,000 |
Circassian (Cherkess) |
Adyghe |
10,000 |
Dom Gypsy |
Domari |
50,000 |
Hawrami (Gurani) |
Hawrami |
22,000 |
1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya
for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk