1985 - 2007

 

39. Kashfa Ya Matumizi Kwa Mkristo

Nyumba unayojenga ni ya nani?

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Hagai 1 na 2

Mstari wa Kukariri
Nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema BWANA wa majeshi (Hag 2:7).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, ni kiasi gani unachotoa kwa ajili ya kazi ya Mungu katika uinjilisti, umisheni, na katika kuwatunza maskini, ukilinganisha na kile unachobakiwa nacho?

Jambo la Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Katika kikundi, tambulishaneni kila mmoja ujuzi alionao, na kisha fanyeni utaratibu wa kulifanyia ukarabati jengo la kanisa lenu, au jengo la kanisa maskini zaidi jirani na kwenu.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika taarifa ya ukurasa mmoja kuelezea Hagai 1:6; inaweza kumaanisha nini katika maisha ya kiutendaji ya kila siku katika siku zetu.

Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Zekaria 4:6

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Benin. Idadi ya watu ni 5,500,000. Asilimia

55% ni wafuasi wa dini za kichawi kama vile voodoo. Makanisa yanakua vizuri.

 

Kitabu cha kinabii cha Hagai kinatoa maelekezo ya Mungu kuhusu ujenzi wa Ufalme wake, na hasa kwa siku zetu.

Historia Kufikia Wakati Wa Hagai
Katika mwaka wa 538 KK Koreshi, mfalme wa Uajemi aliwaruhusu watu wa Mungu waliokuwa uhamishoni kwenda Yerusalemu na kulijenga tena Hekalu lao. Unaweza kusoma habari hizi katika kitabu cha Ezra. Zerubabeli akiwa na watu 50,000 walirejea na katika kipindi cha miaka miwili wakakamilisha kazi ya kuweka msingi. Kulikuwa na shangwe kubwa, lakini Wasamaria waliokuwa wameingia Yerusalemu wakati wa uhamisho, sasa wakahofia usalama wao na kwa kweli wakasitisha shughuli za ujenzi wa hekalu mpaka Dario alipoingia madarakani mwaka wa 522 KK. Mfalme Dario alikuwa mtu mpenda dini. Baada ya hapo watu wa Mungu walipaswa kubeba lawama kwa ‘kulala usingizi’. Ndipo Hagai na Zekaria walipoanza mahubiri ya ‘kuwaamsha watu usingizini’, na mpaka kufikia mwaka wa 516 KK kazi ya ujenzi wa hekalu ikawa imekamilika.

Leo hii amri ya kuujenga Ufalme wa Mungu ulimwenguni kote inaitwa Agizo Kuu. Na masomo ni yaleyale.

1. Je, Ni Wakati Wa Mungu?

Watu wale wakaendelea kusema, “Wakati bado haujawadia”. Kuna maneno mawili kwenye Biblia yenye maana ya wakati, nayo ni chronos na kairos. Chronos ni majira unayosoma kwenye saa yako, lakini kairos, neno analolitumia Bwana, lina maana ya majira ya fursa ya kimbingu. Wakati ule watu walikuwa wakisema, na hata leo kuna baadhi wanasema, “...hakuna kinachoendelea, tuishi tu tupendavyo” (Hag 1:2).

Ni Nini Kinachoendelea Leo?

Tatizo Ni Nini?
Mungu huweka kidole chake penye tatizo halisi. Wale watu walitumia rasilmali za Mungu kujijengea nyumba nzuri, wakati nyumba ya Bwana ikiwa katika hali mbaya. Siku zile kilichotakiwa ni miti kwa ajili ya ujenzi; leo kinachotakiwa ni fedha na watendakazi kwa ajili ya kueneza injili (Hag 1:4,9).

Je, Waweza Kuamini Haya?
Ni ukweli uliofanyiwa utafiti kwamba wakristo wa ulimwengu wa Magharibi wana matumizi yafuatayo:

Asilimia 99.9% ya mapato yao yote wanayatumia wenyewe.

Asilimia 0.09% tu huchangia uinjilisti.

Asilimia 0.01% pekee ndio inayotengwa kwa ajili ya umisheni.

Bwana anasema kwamba watu wajapotumia fedha kwa ubinafsi, hata hivyo hawatosheki (Hag 1:6). Aliwaambia mara nne watafakari juu ya umaskini wao licha ya kujitwalia mafanikio yote peke yao. Mungu akawaambia wakomeshe kashfa hiyo na kumjengea nyumba (Hag 1:8 -11).

2. Waliisikia Sauti Ya Bwana

Kusikia mara zote ni pamoja na kutii (Yak 1:22-25). Katika siku za Hagai viongozi walitii, na watu wote pia (Hag 1:12). Biblia inatuambia katika Mdo 5:32 kwamba Mungu huwapa Roho Mtakatifu hao wanaomtii, na ndivyo ilivyokuwa hapa (Hag 2:5).

3. Mungu Aliifanya Kazi Yake Mwenyewe Pia

Mungu alisema, “Mimi nipo pamoja nanyi”, na akafanya kile ambacho ni Mungu pekee awezaye kukifanya kwa sababu utii wetu humsababisha Yeye atende. Aliiamsha roho ya mtawala wa nchi ile kiutendaji, akamhamasisha kuhani mkuu na watu wote, nao wakaanza kazi ya ukarabati wa nyumba ya Bwana (Hag 1:13-15) (Zek 4:6). Mungu alimwambia yule mtawala, na yule kuhani mkuu, na watu wote, kwamba wasiogope, bali wawe hodari na wafanye kazi kwa sababu yeye yuko pamoja nao (Hag 2:1-5).

Ahadi Ya Kinabii
Kisha Mungu akaahidi jambo ambalo kamwe halijawahi kuwa dhahiri zaidi kama lilivyo katika siku zetu leo, akisema kwamba atazitikisa mbingu na nchi. Na Mungu anapozitikisa mbingu na kuzitetemesha nguvu za giza zinazotawala, haichukui muda mrefu kabla dunia haijahisi mabadiliko (Hag 2:6). Tumekuwa na karne nzima ya mtikisiko hapa duniani, na tumeshuhudia wenyewe serikali na mataifa yasiyoshindwa, mabenki na hata ukomunisti vikiporomoka, na hata sasa mtikisiko unaendelea.

4. Tazama Ni Nani Wanaokuja!

Kisha kinachosubiriwa na mataifa yote kitakuja. Wengi wanachukulia kitu hicho kuwa ni Yesu kwa sababu ndiye anayesubiriwa na watu wake katika kila taifa, na hakika atarudi, lakini kitenzi kilichotumika hapa ni cha wingi.

Wanaosubiriwa Kwa Hamu Watakuja
Hii ina maana ya wale watu ambao Yesu anataka waje kwa mfano watu bilioni 1.2 kutoka Uchina, watu kutoka India, Uarabuni, watu wenye kiburi kutoka nchi za Magharibi, na kutoka katika makabila ya watu wanaohamahama ambao hawajafikiwa bado. Hao wote watakuja katika majira ya Mungu, yaani, kairos.

Na ujumbe wa mwisho na mgumu wa Hagai ni kwamba, kugusa kitu kitakatifu hakukufanyi wewe kuwa mtakatifu, ni dhambi pekee inayoambukizwa namna hiyo. Halikadhalika kujua kila kitu kuhusu Agizo Kuu hakukufanyi wewe kuwa mjenzi wa Ufalme, kwa kuwa uweza haupo katika kujua bali katika kwenda (Hag 1:10 -18).

5. Je, Imebakia Mbegu Yo Yote Ghalani?

Iwapo umekuwa ukiishi maisha ya kutokutosheka, tafakari njia zako na uijenge nyumba ya Mungu leo kwa kuomba, kwa kwenda, kwa kupeleka, na kwa kutoa. Yawezekana hujamzalia Yesu tunda hata sasa, lakini ukilifanya tupu ghala lako, Mungu ameahidi, “…kuanzia leo nitakubariki” (Hag 2:19).

Kwa Kumalizia Omba Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Iraq

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Herki

Herki

22,000

Luri (Lur)

Luri

67,000

Persian (Irani)

Farsi, ya Magharibi

250,000

Shikaki

Shikaki

22,000

Surchi

Surchi

11,000

 






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk