1985 - 2007
40. Kwanini Watu Maskini Wawe Maskini Kiasi Hicho?
Nelson Mandela aliuelewa ubaguzi wa rangi na umaskini
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Mstari wa Kukariri
"Fumbua kinywa chako
kwa ajili yake aliye bubu; uwatetee watu wote walioachwa peke yao; fumbua
kinywa chako, uhukumu kwa haki; uwapatie maskini na wahitaji haki yao” (Mit
31:8,9).
Baaadaye Zungumzieni Jambo
Hili
Ni kwa jinsi gani
unavyoweza kuwa mikono ya Yesu, miguu yake na moyo wake kwenye mji unamoishi?
Jambo La Kufanya Kabla
Hatujakutana Tena
Kama kikundi mwendeeni
wakala anayefanya kazi miongoni mwa watu maskini na mjitolee kufanya kazi kwa
ajili yao. Msijali kama wakala huyo ni Mkristo au la.
Kazi Ya Kuandika Ya
Stashahada
Andika maelezo ya
ukurasa mmoja ukiainisha jambo unalodhani limewapata watu na kuwafanya
maskini.
Tafakari Mstari Huu Neno
Kwa Neno
Yeremia 22:16
Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Bangladesh. Idadi ya watu ni 132,000,000. Ni maskini sana.
Asilimia 87% ni Waislamu; asilimia 10% ni Wahindu; na asilimia 0.08% ni wafuasi wa madhehebu ya Kianjili.
Watu ni wengi kupita kiasi, na nchi inakumbwa na mafuriko.
Siku moja Yesu alipokuwa akizungumza na umati wa watu ambao wengi wao walikuwa wanavijiji walioishi chini ya utawala wa kimabavu wa Warumi na viongozi wa kidini matajiri, aliwaambia, “Heri yenu ninyi mlio maskini, …” (Lk 6:17-20). Mara nyingi sisi tunapenda kufasiri maneno Yesu anayozungumza kuhusu maskini kumaanisha ni umaskiniwa kiroho, lakini neno Yesu analotumia hapa ni ptochos, lenye maana ya maskini anayetetemeka.
Biblia inataja maskini zaidi ya mara 245 na hii inaonesha jinsi Mungu alivyo na mengi ya kusema kuhusu umaskini. Suala hili lipo karibu na moyo wake na kamwe hautaji umaskani kama baraka, wala utukufu, au jambo la kufurahiwa, kinyume chake Biblia inasema ni laana.
1. Kwanini Watu Maskini Ni Maskini?
Baadhi ya watu ni maskini lakini si kosa lao; lakini ni kutokana na kunyonywa na kukandamizwa na watu wengine, dhambi za watu matajiri, viongozi wala rushwa, au mataifa yanayovamia na kutawala. Maneno ya Kiebrania ni rush na ani.
Maskini Wanyenyekevu Wa
Bwana
Baadhi ya watu wa
Mungu waliodhilika kwa umaskini na kukandamizwa wanaitwa maskini wanyenyekevu
wa Bwana, na wanamlilia Bwana wao na kumtegemea yeye kwa unyenyekevu (Kut
1:11,12). (Neno ani ni la Kiebrania, na ptochos ni la Kigiriki).
Waathirika Wa Maafa
Watu wanaweza kuwa
maskini pia kutokana na maafa yanayosababishwa na matukio ya asili, ajali,
uchumi mbaya kitaifa, au wamezaliwa wakiwa vilema, na kwa kweli hawana kosa
katika yote hayo. Wanaweza wakawa ni watu wadogo, au wasio na ulinzi wala
msaada wo wote kama vile wajane na yatima. (Maneno ya Kiebrania ni ebyon,
dallah, na dal).
Dhambi Ya Mtu Binafsi
Watu wengine wengi ni
maskini kutokana na dhambi zao wenyewe na hilo ni kosa lao wenyewe (Ayu 33:3)
(Mit 13:25; 24:30; 21:5; 22:16; 21:17; 28:22) (Kum 28:48)(Neno la Kiebrania ni
chaser). Dhambi binafsi inasababisha umaskini, lakini machungu ya
umaskini huo yanasababisha dhambi nyingine binafsi kama vile wizi na ulevi
unaosababisha uovu, magonjwa, na vurugu (Mit 30:9; 30:7).
2. Kwa Namna Gani Wanaweza Kubarikiwa?
Yesu anawaita maskini heri kwa sababu anajua wamebarikiwa na Mungu, Mungu wa haki yote, Mungu anayerekebisha mambo yote kuwa sawa. Watu wengi walio maskini hawajawahi hata kusikia habari hizi, licha ya kufungua mioyo yao na maisha yao ili kupokea hiyo baraka.
Ni Nini Jibu La Mungu?
Katika Mithali 31:9 waamini
wanaelekezwa jambo la kufanya. “Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki;
uwapatie maskini na wahitaji haki yao”. Hatima ya watu maskini ipo mikononi
mwetu, ingawa zoezi hili linaweza likawa hatari kwetu kama lilivyokuwa kwa
watu waliowatetea maskini kama vile Amy Carmichael, William Wilberforce na
William Booth.
Mungu Anawaona Watu Maskini Kuwa Wa
Thamani
Soma kutoka Ayubu 36:15, Zaburi
34:6; 35:10; 113:7, 8; ili upate kujua kwamba habari njema za Mungu kwa
maskini ebyon, dal
na dallah ni Yesu mwenyewe (Lk 7:22).
Sisi Ni Mikono Ya Yesu
Wengine wananukuu 1Yoh 3:17 au
Yak 2:15; 1:27 na kusema kwamba tunapaswa kuwasaidia ndugu zetu kwanza. Ni
sawa kwa sababu wapo wengi sana wanaopambana katika udhaifu wao, lakini hata
hivyo maskini, chaser, ambaye pengine hapendwi au pengine hana
shukrani, ana huruma na neema kwa Mungu.
Mungu anasema nao kipekee katika
Zab 23:1, Zab 34:9,10. Soma pia Ayu 29:15,16.
3. Maskini Wanabarikiwaje Basi?
Yesu aliposema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini,...” alikuwa akiwatazama wafuasi wake (Lk 6:20). Hao ni maskini ambao pia ni wafuasi wa Yesu ndio wanaobarikiwa kupitia imani yao kwa Mungu.
Kubarikiwa Na Mungu Anayejali
Mungu anaelewa machungu ya umaskini kuliko mtu mwingine ye yote, kwa sababu pale msalabani Mungu mwenyewe kama Yesu alipata mateso ya kusalitiwa, kunyimwa haki, kukandamizwa na kukosa vitu vyote.
§ Ayubu anawatetea maskini, (Ayu 1:16).
§ Zaburi za Daudi zinawapa maskini tumaini.
§ Isaya anatabiri msaada kwa watu wanaowapenda maskini, (Isa 58:6-12).
§ Hosea anatujulisha jinsi Mungu anavyofanya watu wampende, (Hos 11:4).
§ Yeremia anauliza kama kweli unamfahamu Bwana, (Yer 22:16).
§ Yesu alipakwa mafuta na Mungu ili awahudumie akina ptochos, ambao ni wanyenyekevu wa Mungu walio maskini (Lk 4:18,19).
§ Paulo anaweka fundisho katika matendo, (Gal 2:10; 6:10) (2Kor 8:13).
§ Yakobo analipa kanisa changamoto, (Yak 2:5, 14-16).
§ Kanisa la Petro lilijali, (Mdo 4:34,35).
§ Neno la mwisho la Yohana, (1Yoh 3:17,18).
Kubarikiwa Kwa Kupokea Msamaha
Katika Yesu kuna msamaha wa
Mungu kwa dhambi zote binafsi zinazosababisha umaskini. Safari ya kwenda
Jehanum iliyo halisi inaweza kusitishwa na mwelekeo wake kugeuzwa kabisa.
Kubarikiwa Kwa Neema Ya Mungu
Yesu anawapa watu maskini uwezo
dhidi ya majaribu. Mikono iliyotumika katika wizi sasa inamtumikia Mungu,
familia na watu wengine (Efe 4:28).
Kubarikiwa Na Watu Wa Mungu
Mungu anaamuru waamini wenye
mali na uhuru kuwafadhili watu maskini na kusimama kinyume na vitendo vyote
vya uonevu vinavyowashikilia mamilioni ya watu kwenye umaskini wa rush.
Katika Mt 25:35 Yesu anaelekeza la kufanya.
Katika mazingira hayahaya ya umaskini, wafuasi wanaagizwa kuwapenda adui zao, ambao wanaweza kuwa ndio haohao maskini wanaokuibia, na sio kuwapenda wale tu wanaowapenda ninyi. Tunapaswa kufanya wema wetu si kwa wale wanaotufanyia wema tu, tusiwahukumu, na tusiwakopeshe wale tu watakaoturudishia. Utakapowapa maskini, na wewe utapewa (Lk 6:27-38). Hawataweza kukulipa lakini Mungu atakulipa (Mit 19:17).
Injili inawabariki maskini wanaomkimbilia Kristo, na Injili hiyohiyo inawabariki matajiri wanaomkimbilia Kristo. Lakini kama tajiri atakuwa ni sababu ya watu wengine kuteseka kwa umaskini, Yakobo anatoa tahadhari (Yak 5:1-6).
Kwa Kumalizia Omba kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina
Japan | ||
Jina la watu |
Lugha yao |
Idadi yao |
Amami-Oshima |
Amami-Oshima |
16,000 |
1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya
for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk