1985 - 2007
44. Yesu Aliishije?
Fundi seremala anaweza kuubadili ulimwengu!
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika Biblia Yako Soma
Wafilipi 4:2-20
Mstari wa Kukariri
Na Mungu wangu atawajazeni kila
mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu
(Flp 4:19).
Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Zungumzieni kuhusu kanuni
mlizoziona katika maisha ya Yesu na Paulo. Je, wewe huwezi kuishi kama wao?
Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana
Tena
Andaa bajeti ya familia yako ya
kila mwezi ukionesha mapato na matumizi. Weka orodha ya mapato yanayotarajiwa
upande mmoja na matumizi yanayotarajiwa upande mwingine. Je, pande mbili
zinalingana? Mapato yakizidi matumizi ni baraka, kinyume chake ni matatizo!
Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Soma Kumbukumbu La Torati mlango
wa 28 na kisha orodhesha yote yaliyosemwa kuhusu mafanikio na umaskini. Andika
kwenye ukurasa mmoja ukionesha kila mojawapo linavyokuja.
Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Kum 28:47
Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Djibouti. Idadi ya ni 473,000. Huko kuna Waislamu Wasomali na Waarabu. Wakristo ni wachache katika taifa hilo lililoko katika pembe ya Afrika. Ni jangwa na joto.
Mungu Alikuwa Na Mtoto Mmoja, Naye Alikuwa Mmishenari
Yesu aliishije? Kwa namna gani aliweza kujinunulia chakula na kulipa bili zake nyingine? Je, alibadili mawe kuwa mkate, na uwezo alikuwa nao, au alihudumu kama mtu mwenye uwezo wa Roho Mtakatifu? Maandiko yanatuonesha kwamba hilo la pili ndilo sahihi (Flp 2:6-8) (Mdo 1:2).
Hatujui majibu yote, lakini Biblia inatoa nuru ingawa haioneshi waziwazi ni njia ipi mojawapo iliyotumika. Hebu kwanza tushughulikie swali moja muhimu.
Je, Yesu Alikuwa Mtu Maskini?
Watu wengi na wachungaji watajibu, “Ndiyo”. Watu wanaonekana kuwa na mawazo kwamba kuna namna ya utakatifu au unyenyekevu katika umaskini, ingawa Biblia inasema ni laana (Kum 28:47).
Ya Nini Mtu Maskini Kuwa Na Mweka Hazina?
Je, katika maskini unaowafahamu kuna mmojawapo aliye na mweka hazina wa kuangalia mahesabu ya fedha zinazoingia na kutoka? Jambo moja ni wazi, kwamba Yesu alikuwa na namna ya kupata fedha kwa ajili yake, kwa ajili ya watu 12, na kwa ajili ya kutoa sadaka. Maskini hawezi kuwa na mweka hazina, lakini Yesu alikuwa naye. Kwahiyo kulikuwa na fedha; lakini zilitoka wapi?
Yesu Alichagua Udhaifu
Siku hizi kila mmoja anatafuta kuwa na nguvu lakini Yesu alichagua kwa dhaifu, na wepesi wa kushambuliwa na kudhurika; na kumtegemea Baba yake na rafiki zake.
Ni Wa Kawaida Tu!
Kitu Mungu anachotaka kutuonesha kupitia kwa habari za Yesu ni kwamba kuna upatikanaji wa riziki kwa njia za miujiza wakati tunapohitaji, lakini kwa kawaida riziki kwa watendakazi wa saa ya kumi-na-moja hutoka kwa Mungu na kuwajia kwa matukio ya kawaida ya kila siku na kwa kupitia kwa watu wa kawaida ambao Mungu anawaleta kwako. Kaza mwendo kuenenda katika utakatifu, katika upole na kwa kuishi kwa ajili ya wengine, nawe utaona jinsi Mungu atakavyojenga daraja imara chini ya miguu yako unapotembea juu ya mwujiza wa imani kwake na kwa neno lake (Yn 6:35).
Paulo Aliishije?
Na sasa, vipi kuhusu Paulo, mtu
aliyepeleka injili Ulaya, na kuandika nyaraka zilizo nyingi katika Agano Jipya.
Ni Nani Aliyemtegemeza Paulo Katika
Huduma Yake?
Hakutegemezwa na kanisa la
Antiokia kwa sababu isingewezekana katika siku hizo. Katika matukio yote Paulo
alipelekwa na Roho. Makanisa yalimtegemeza, lakini pia makanisa yalisitisha
misaada yao. Mara moja tu kanisa moja lilimtegemeza (Flp 4:16).
Theolojia Ya Paulo Ya Kuishi
Paulo, mwanatheolojia mkuu wa wakati wake alielezea namna ya kuishi kwa kusema, “Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami” (1Kor 15:10).
Umeshaona ya kwamba huhitaji kuwa mtu mwenye imani kubwa ili uweze kuitikia wito wa Mungu. Watu wakuu sana katika Agano Jipya wametuonesha jinsi lilivyo jambo la moja kwa moja kuishi katika neema na riziki za Mungu.
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina
Libya | ||
Jina la watu |
Lugha yao |
Idadi yao |
Zuara (Zwara, Zuraa) |
Zuara |
33,000 |
1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya
for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk