1985 - 2007

 

45. Kuupiga Vita Umaskini

Katika Yesu utapata njia za kuupiga vita umaskini

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
2 Wakorintho 8 na 9.

Mstari wa Kukariri
Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake (2Kor 8:9).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Mwe waaminifu ninyi kwa ninyi. Je, umekuwa ukiukubali umaskini kama kitu cha lazima na kwamba hujafanya juhudi yo yote ya kupigana vita vya kiroho dhidi ya nguvu za giza zinazohusika kukuletea huo umaskini?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Tafuteni kila sababu ya kulitoa kasoro somo hili. Kama hamwezi kupata kasoro yo yote basi kaeni pamoja na kutubu mbele za Mungu kwa kuikubali laana kama kitu cha kawaida, na katika maombi kwa jina la Yesu, mkisimamia kwenye neno la Mungu, mpeni Shetani notisi ya kuanza kwa mapambano dhidi ya umaskini wake.

Kazi ya Kuandika ya Stashahada
Andika taarifa ya ukurasa mmoja ukieleza mfano wa ‘ngamia wa nundu tatu’ unaweza kuwa na maana gani katika maisha.

Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Zab 23:1

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Kuwait. Idadi ya watu ni 1,300,000. Ni Waarabu na wahamiaji. Ni nchi yenye mafuta mengi. Wananchi wake ni Waislamu; wahamiaji wanaweza kuwa Wakristo.

 

Kumpanda Ngamia Mwenye Nundu Tatu

Watu husema kwamba kuna taabu kusafiri juu ya ngamia mwenye nundu moja au mbili; sasa hebu fikiria safari ndefu juu ya ngamia mwenye nundu tatu! Lakini hilo ndilo hasa tunaloitiwa katika maisha ya huduma ya Kikristo. Msikilize Paulo anavyozungumzia mtindo wa maisha yake ya kifedha katika Mdo 20:33-35.

Sijatamani fedha waIa

dhahabu ya mtu…mnajua kuwa

mikono yangu hii imenipatia-

 

Mahitaji yangu mwenyewe,

Mahitaji ya wenzangu,

Na mahitaji ya walio dhaifu…

Kwa sababu kuna baraka zaidi katika kutoa kuliko katika kupokea.

Nundu ya kwanza – kupata mahitaji yako mwenyewe.

Nundu ya pili – kuwa na fedha za kutosha hata kuwasaidia wenzako.

Nundu ya tatu – kuwa na fedha za kutosha kuwasaidia maskini pia. Lengo ni kuwa na fedha za kukutosha wewe na ziada ya kuwagawia wengine. Pengine unapata taabu katika kulipa bili zako, utawezaje basi kuwa na wazo la kutoa kwa ajili ya wengine?

Imani Ya Kuupiga Vita Umaskini

Haiwezekani kumpendeza Mungu bila imani, na imani huja kwa kusikia na kuliamini neno la Bwana. Kwa hiyo Bwana ana nini la kusema?

(Ebr 11:6) (Rum 10:17).

Mungu Ndiye Atupaye Uwezo Wa Kuzalisha Mali

Kum 8:18 inasema waziwazi kwamba Mungu ndiye atupaye uwezo wa kuzalisha mali. Mungu hakupi utajiri, ila anakupa uwezo wa kupata utajiri. Je, umemwomba Mungu akupe huo uwezo?

Mungu Anaweza

Je, ni nini anachoweza kufanya?

 

Anaweza -

Kuwajaza kila neema kwa wingi,

ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna sikuzote,

mpate kuzidi sana katika kila tendo jema.

Ufunguo ni kupanda kwa ukarimu ili upate mavuno. Ukifanya hivyo, neno la Mungu linaahidi kuwa utatajirishwa kwa kila namna. Kwanini Mungu afanye hivyo? Ni kwa kuwa anataka uwe mkarimu nyakati zote, kwa wenzako na kwa maskini, na ukarimu wako utasababisha Mungu apewe shukrani (2Kor 9:6-11).

Karama Ya Mungu Isiyoelezeka

Paulo huhitimisha maelezo yake yanayohusiana na uhuru wa fedha kwa kumshukuru Mungu kwa karama yake isiyoelezeka. Karama hiyo ni nini?

Karama Hiyo Ni Bwana Yesu Kristo

Ni kwa sababu ya Yesu tu, mateso yake na kazi aliyoifanya pale Msalabani kwamba tunapokea baraka za Mungu maishani mwetu.

Ni Nini Kilichofanyika Pale Msalabani?

Yesu alitwaa kutoka kwetu vitu vyote vilivyokuwa vinatuharibu, na mahali pake akatupa baraka za Mungu. Kulifanyika mabadilishano ya kimbingu.

Yeye alisulibishwa kwa ajili ya maovu yetu.

Yeye alijeruhiwa kwa makosa yetu.

Yeye aliadhibiwa ili sisi tupate amani.

Yeye aliumizwa ili sisi tupone.

(Isa 53:5,6) (1Pet 2:24).

Hebu Twendeni Hatua Moja Zaidi

Kwa kuwa mnaijua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba ingawa alikuwa tajiri, lakini kwa ajili yenu alikuwa maskini, ili kwamba ninyi kwa kupitia umaskini wake, mpate kuwa matajiri (2Kor 8:9).

Yesu alikuwa tajiri mbinguni pamoja na baraka zote za Mungu. Kwa ajili yako akawa maskini. Mtu maskini hana cho chote na hawezi kujitegemeza mwenyewe. Pale Msalabani Yesu akawa huyo mtu maskini. Kwanini? Ni ili kwamba wewe, kwa kupitia umaskini wake upate kuwa tajiri. Ukichunguza kwa makini maneno ya asili ya ‘tajiri’ yaani plousios na plouteo yana maana ya utajiri wa mali; na ‘maskini’ yaani ptocheuo lina maana ya umaskini wa kina.

Paulo Hakumaanisha Utajiri Wa Kiroho

Yesu aliyekuwa tajiri aliutwaa umaskini na ufukara wako, na badala yake akakupa wewe utajiri wa mali unaopokelewa kwa imani.

Je, Utayaamini Haya?
Unaamini kwamba umeokoka na unapinga vikali juhudi yo yote ya Shetani ya kutaka kukuibia wokovu wako. Unaamini kwamba uliponywa pale Msalabani na unampinga Shetani anapojaribu kukuibia afya yako. Unaamini kwamba uliwekwa huru na laana pale Msalabani na unavunja kila moja ambayo Shetani anajaribu kuileta kwako; lakini je, unaupiga vita umaskini kwa kwa juhudi iyo hiyo?

Au je, unaafikiana na adui, ukikubaliana na uongo wake na hoja zake kwamba kwa vile watu wanaokuzunguka ni maskini, basi ni wazi kwamba njaa na kutindikiwa katika kazi ya Mungu ni vitu vya lazima na vya kukubalika, ingawa Biblia inasema umaskini ni laana? Ukweli wa hali ya juu kuliko ukweli mwingine wo wote ni kwamba kwa sababu ya Yesu na Msalaba wewe umeokolewa, umeponywa, unapendwa, umewekwa huru, na mahitaji yako yanashughulikiwa na Mungu aliyekuchagulia nafasi katika maisha na anakupa vitu vya kukuwezesha kuishi katika nafasi hiyo. Kwanini upokee baraka moja tu na si nyingine pia? Linapokuja suala la matumizi ya vile anavyokupa Mungu, swali ni kwamba, unafanya nini na vile anavyokupa – je, unavitumia vyote peke yako, au unafanyika mikono Yake ya ukarimu na huruma kwa wengine?

Angalia pia kitabu cha Jonathan Frusher kiitwacho God Wants His Money Back, yaani, Mungu Anataka Arudishiwe Fedha Zake, kinachoweza kusomwa bila malipo kwenye anwani ifuatayo http://www.dci.org.uk/main/library.htm.

Yesu Alisema, “Imekwisha”

Kazi yake pale Msalabani haikubakiza cho chote ambacho kinaweza kufanywa na mwanadamu mbali na kuamini (Yn 19:30). Kama unakosa kipaji cho chote kutoka kwa Mungu, ni nani anayekuibia? Utafanyaje sasa? Kama utauweka msingi wa imani mahali pake, na kupambana na laana ya umaskini kwa kustahimili katika imani, kwa kuomba na kutenda, hali itaanza kubadilika na hatimaye itaanza kwenda sawasawa na neno la Mungu.

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

 

Malaysia

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Banjar (Banjar Melau)

Banjar

221,000

Brunei

Brunei

54,000

Butonese (Wolio)

Wolio

12,000

Orang Negeri

Negeri Sembilan Malay

300,000

Sama, Central (Sinama)

Sama, Central

40,000




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk