1985 - 2007

 

47. Fedha Ya Ufalme

Utapata wapi chakula chote hiki bila fedha au gharama?

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Isaya 55

Mstari wa Kukariri
Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu (Isa 55:8).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Hebu fikiria kuhusu kupokea. Katika maisha ya kila siku, ni kwa namna gani na ni lini unapopokea kitu cho chote. Ni nini kinachotokea?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Fanya juhudi za makusudi kabisa kukaa kimya. Tenga siku moja kwa ajili ya kumtafuta Mungu. Katika kipindi cha saa moja au zaidi utaona mambo yakikujia mawazoni mwako. Yaandike, mkabidhi Mungu halafu kaa kimya.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Elezea katika kurasa mbili ni jinsi gani na ni lini Bwana alipomtimizia Daudi baraka zote hizo alizozitaja katika 2Sam 7:8-11.

Tafakari Mistari Hii Neno Kwa Neno
Zab 37:25,26

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Kenya. Idadi ya watu ni 31,000,000 katika makabila 117. Asilimia 82% ni Wakristo, wengi wao wa majina.

Kuna uhuru mkubwa wa kuhubiri Injili; zaidi ya Wakenya 500 ni wamishenari.

 

Bwana anasikilizwa na kila mtu anapotualika kwake ili -

Kuja kununua maziwa na mvinyo

Bila fedha wala gharama.

(Isa 55:1).

Neno la Mungu katika aya hii yenye utukufu linasema kwamba bila fedha au gharama unaweza kupata maziwa ambayo ni chakula, na divai inayoashiria sherehe.

Kuna Ahadi Zaidi

Utakula kilicho chema, (Isa 55:2b).

Nafsi zenu zitajifurahisha kwa unono (Isa

55:2b). Yer 31:12 inaelezea jinsi ukarimu

wa Bwana ulivyo, na Isa 1:19 anasema

kwamba kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi.

Je, umekubali na kutii?

Kuna uzima kwa ajili ya nafsi yako (Isa 55:3).

Kuna baraka katika agano la milele la Mungu (Ebr 13:20).

Mungu Anakuahidi Uaminifu Katika Upendo Wake

Ni sawasawa na alivyomwahidi Daudi, (Isa 55:3). Hii ina maana gani? Pata jibu lake katika 2Sam 7:8-12.

Maendeleo binafsi.

Mungu atakuwa pamoja nawe.

Utapata pumziko mbali na adui zako, hata watakapoangamizwa.

Mungu anasema atalikuza jina lako (Mwa 12:2).

Utapata makazi.

Uzao unapewa ahadi.

Kwanini Mungu Alimbariki Sana Daudi?

Kwanini atake kukubariki wewe sana? Ni kwa sababu alipanga kumfanya Daudi na ufalme wake kuwa ushahidi hai kwa mataifa kuonesha wema wake na ukarimu wake uliotolewa bure (Isa 55:4). Watu waliona baraka za Mungu na kumkimbilia Daudi, ambaye ni taswira ya Yesu. Na kwa namna iyo hiyo Mungu anataka kukuonesha ukarimu wake kwa namna ambayo watu wote waliokuzunguka wataona kwa sababu mpango wake ni uleule, haujabadilika.

"Tazama utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia…” (Isa 55:5)

Aina Nyingine Ya Fedha

Ikiwa fedha hazitatumika kununulia divai yetu na maziwa, basi ni lazima pana aina nyingine ya fedha katika uchumi na biashara kwenye ufalme wa Mungu.

Hiyo fedha nyingine inaweza kuwa kitu gani?

Ufunguo Ni Neno Moja, “Kupokea”.

Mojawapo ya tafsiri za Biblia inasomeka hivi katika Isa 55:1, “Njoo, nunua, baraka zinapokelewa na yule aliyejisalimisha tu”. Kwa kawaida watu hupenda kufanya kazi, wakijitahidi ili wapate fedha na wajisikie wenye thamani. Lakini wokovu wa Mungu huja kwa imani na wala si kwa kazi zetu ili kwamba tujisikie wa maana.

Tafadhali Ni Lazima Sasa Iwe Asante

Mpango wa Mungu ni kwa sisi kupokea kila tunachokihitaji kutoka kwake. Upo wakati wa kuomba, na upo wakati wa kupokea, lakini baadhi ya watu wanadumu katika kuomba lakini hawapokei (Rum 8:32) (Yn 1:16).

Ufunguo Wa Kupokea Ni “Kusikiliza”

Sikiliza, nisikilize mimi. Tega sikio lako, njoo kwangu, nisikie mimi. Bwana anawatafadhalisha watu wenye shughuli nyingi wa ulimwengu huu wenye makelele (Isa 55:1-3). Jambo hili linaonekana kuwa ni rahisi tu, lakini linaweza kuwa ni gumu sana, kwa sababu watu wenye njaa hawataki kusubiria maneno, wanachotaka ni kula na kunywa. Tunajua kwamba Mungu amewatunza watu wake kwa miaka mingi katika miji na jangwani pia; sasa kwanini tunapendelea kuhangaikia chakula badala ya kuwa na muda na utulivu ili kumsikiliza Yehova Yire?

Kwanini Inakuwa Vigumu Kumsikiliza Mungu?
Mmishenari mmoja aliugua nchini Malaysia na madaktari wakasema angeweza kufa. Akiwa kule hospitali mawazo yake yalijawa na mambo yake, matatizo na ahadi za kukutana na watu; lakini akatambua kwamba alikuwa anakabiliwa na kifo na kwamba hakuna analoweza kufanya kati ya hayo. Akawaza kwamba muda mfupi ujao angeweza kuwa na Bwana, na mtu mwingine angechukua nafasi yake akishughulikia masuala ya tiketi, fedha, familia, na mambo mengine. Moja baada ya lingine aliyakabidhi kwa Bwana katika maombi, na akapumzika, mawazo yake yakiwa yametulia kuona ni nini kitakachotokea. Na sauti za mambo hayo zilipokoma kutawala mawazo yake, ndipo alipoweza kuhisi uwepo wa Bwana na kuisikia sauti yake vizuri. Hatimaye alipona, lakini hadi leo anajuta kwa kuruhusu tena mawazoni mwake zile sauti zilizoondoka kwanza ambazo sasa zinamzuia kuwa na uhusiano wa karibu sana na Mungu. Sauti za mambo ya kila siku, na jitihada zetu za kutatua matatizo mbalimbali kwa kutumia akili zetu, ndiyo hali inayotuzuia tusimsikie Mungu.

Je, Unaweza Kusikia Nini Kutoka Kwa Bwana?
Ukimsikia Roho akisema, “Njoo”, atakuambia uje wapi. Bibi harusi, yaani kanisa, naye anaposema, “Njoo” umepata uthibitisho thabiti. Jibu kwa Roho liwe, “Ndiyo, naja”, na mahali pale alikokuitia utapata kinywaji bure (Ufu 22:17).

Ufunguo Wa Kusikiliza Ni “Kutafuta”

Bwana anasema, “Nitafute”. Tukimtafuta tutampata na sauti yake tutaisikia (Isa 55:6-11). Lakini kama hutamtafuta na kumsikia hakika yake utatenda kosa. Kwanini? Ni kwa sababu mawazo yake na njia zake ziko juu sana kupita zetu, na ni tofauti na za kwetu. Maneno yake mwenyewe yanayotoka kinywani mwake ambayo sisi tunayarudia kwa vinywa vyetu ndiyo yanayolitimiza kusudi lake na hayamrudii bure (Isa 59:21) (Mt 6:33).

Funguo Zinazoufungua Mlango

Funguo hizi tatu, yaani, kupokea, kusikia na kutafuta, ndizo zinazoleta uhuru wa kifedha kwa watumishi wa Bwana na kazi ya injili. Agizo Kuu linakuwa ni uhusiano wa kutembea na Bwana kwa karibu, na wala si shughuli iliyokumbwa na ukata mkali.

Utakwenda Kwa Furaha Wala Si Kwa Mashaka

Kwa kuwa unajua Mungu amesema na wewe na kukupa maelekezo; kwa imani unajua kwamba ameweka mahitaji yako mbele yako.

Una amani kwa sababu hakuna hofu ya shinikizo lo lote linalosababishwa na fedha ulizokopa ili kufanyia mambo yako.

Unaweza kuiongoza milima na vilima katika kumsifu Mungu badala ya kukaa na hofu.

Utakwenda ukitazamia ukuaji katika maeneo magumu badala ya miiba na michongoma, na matunda ya kudumu kwa utukufu wa Bwana.

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili Bado, Ukiwataja Kwa Majina

Mali

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Pana

Pana

10,000

Samoa

Samoma (Kalamse)

10,000

Samogho, Duune

Duungo

83,500




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk