1985 - 2007

 

48. Funguo Za Ufalme

Kusema na milima si jambo la ajabu kama unavyofikiria

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Kum 14:22 -15:11

Mstari wa Kukariri
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu ndani, ya Kristo Yesu (Flp 4:19).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, umewahi kujikamata mwenyewe ukiongea na gari lililokutangulia, au taa za kuongoza magari, au basi lililochelewa, au hata kikangio chako kikiwa juu ya jiko? Sasa itakuwaje ajabu kwako kuzungumza na milima, mito au miamba?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Hebu pitia tena kwa uangalifu utoaji wako ili kuhakikisha kwamba unakubaliana na viwango vya Mungu. Unaweza pia ukapanga kuongeza matoleo yako mwezi hadi mwezi ukawagawia maskini.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Elezea kwenye ukurasa mmoja jinsi mpango wa Mungu wa akiba ulioko katika Kum 14:22-29 unavyoweza kutekelezwa leo kwa kutenga fedha.

Tafakari Mstari Ufuatao Neno Kwa Neno
Mhu 7:12

Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Oman. Idadi ya watu ni 1,800,000, Waarabu na wahamiaji. Asilimia 95.5% ni Waislamu wa Ibadi. Pengine wapo wakristo 20 tu kutoka Oman.

 

Sisi tunajielewa kuwa ni watendakazi wa saa ya kumi-na-moja katika shamba la Bwana la siku za mwisho, na kwamba ingawa mishahara yetu haijulikani na mapema, lakini hatuna mashaka kwa sababu Bwana wetu ni mkarimu. Tumeshaona namna Yesu na Paulo walivyoishi na tumegundua msingi wa imani ya mambo ya fedha katika kazi iliyomalizika pale Msalabani. Isaka ametuonesha namna ya kuwa na msimamo sahihi wa uvumilivu katika majaribu kabla hatujapata mafanikio; si kama ilivyo leo kwa mtu kutaja tu baraka anayotaka, kuidai na kusubiri mtu ajitokeze na kumpa! Tumejifunza pia kuhusu sarafu ya imani kutoka kwa Isaya. Je, hilo tutalifanyiaje kazi?

1. Mwamini Bwana

Jihadharini na tabia ya kupenda fedha, na toshekeni na mlivyonavyo kwa sababu Mungu mwenyewe alisema,

 “Kwa vyo vyote sitakupungukia kabisa, wala sitakutelekeza na kukuacha bila msaada. Kamwe, kamwe, sitakuacha hata kwa kiwango kidogo, kukuacha bila msaada, au kukuacha, au kukuangusha, au kulegeza mkono wangu kwako. Hakika sitafanya hivyo! Kwahiyo tunafarijika na kutiwa moyo, na kwa uhakika na ujasiri twathubutu kusema, ‘Bwana ndiye anisaidiaye’”(Ebr 13:5, 6) (Tafsiri mojawapo ya Biblia ya Amplified).

Ng’ang’ania neno lake katika mazingira yanayokuja kinyume, ustahimili, na muda si mrefu yatajitokeza mazingira yale yasiyopingana na kweli ya neno la Mungu.

2. Uwe Na Imani Katika Mungu

Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na hivi vitu vingine vyote mtapewa. Vitu, vitu halisi. Kama ukivikosa ‘vitu’ unavyovihitaji ni lazima ujihoji kama kweli unautafuta utawala wa Mfalme, na njia yake ya haki ya kufanya mambo.

Theolojia Ya Maria Ya Kupata Riziki
Maria, mama wa Yesu alikuwa na theolojia inayotenda kazi. Alisema, “…Lo lote atakalowaambia, fanyeni” (Yn 2:5).

Imani ya Paulo Katika Kupata Riziki
Paulo aliwaambia rafiki zake kule Filipi, “Na Mungu wangu atawajazeni na kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu (Flp 4:19). Na huu ni ushuhuda wake baada ya miaka ya ugumu wa maisha na safari za kuhubiri injili. Angalia orodha ya mikasa aliyokumbana nayo Paulo katika 2Kor 11:23-29.

Baada ya uzoefu mwingi ambapo Mungu ndiye aliyekuwa mfadhili wake pekee, Paulo anasema kwamba, ‘ni Mungu wangu pekee, si taifa langu au dini yangu itakayowatimizia mahitaji yenu yote’. Paulo aliposema ‘yote’ alimaanisha yote na akadokeza kwamba kujazwa kwenyewe kutakuwa ‘kwa kadiri ya utajiri wake’, na hapo akitaka kutuhakikishia kwamba mbinguni hakuna upungufu. Paulo akaongezea, ‘…katika Kristo Yesu’, akitupa anwani ya chanzo cha mahitaji yetu.

3. Ishi Maisha Yanayompendeza Bwana

Kanisa la kule Laodikia lilikuwa mbali sana na Mungu kiasi kwamba ilibidi Yesu aligongee mlango kwa nje akitazamia kwamba atakuwepo mtu ndani atakayemsikia (Ufu 3:20). Lakini maisha yetu yanapaswa kuwa safi, mahali ambapo Mungu atapenda kuishi ndani yake na kunena nasi mara kwa mara. Paulo aliwaambia Wafilipi la kufanya:

  1. Uhusiano mzuri baina yao huleta utulivu wa ndani wa kuweza kumsikia.
  2. Maisha ya sifa na shukrani humfanya Mungu ajisikie nyumbani.
  3. Maisha ya maombi na ushirika na Mungu huleta majibu yake.
  4. Kuna thamani kubwa sana kuweka nia yako safi, kwa sababu itakuwa wazi kwa Roho apate kukunong’oneza.
  5. Jifunze kutosheka katika mafanikio na katika umaskini. Utoshelevu si kitu rahisi. Ni siri unayopaswa kujifunza.
  6. Jifunze kutoa na kupokea. Kwa baadhi ya watu kutoa ni jambo gumu; lakini kwa wenye kiburi kupokea kwaweza kuwa kugumu zaidi. Mungu ana namna ya kuwapanga wajane na watoto kuudhili moyo mwenye kiburi sana.

Kwa sababu anajua kwamba wale Wafilipi wanalenga kuishi namna hiyo anaweza kuwaambia kwa kujiamini kwamba, ‘Na Mungu wangu atawajazeni na kila mnachokihitaji…’ (Flp 4:2-20).

4. Zishinde Hisia Zinazokuwa Kinyume

Tubu kwa msimamo wo wote usiostahili ndani mwako. Kwa kule kukuita tu, tayari Mungu amekwisha azimia kwamba wewe unastahili kutegemezwa na Yeye na wanadamu pia. Usihofie udhaifu, na wala usitishwe na nguvu za watu wengine. Kumbuka kwamba Mungu huwachagua, huwatumia na kuwabadilisha watu dhaifu. Vunja tabia ya kupenda kujitegemea na kiburi ambayo Mungu anaichukia, na uchague kuishi maisha ya kutegemeana, umtegemee Mungu na watu wake pia (Mhu 4:9-12).

5. Pigana Vita Vya Kiroho Dhidi Ya Umaskini

Vunja kila laana ya umaskini, ya kale na ya sasa, na kila nguvu za kipepo kwa maombi katika jina la Yesu. Itia damu ya Kristo kinyume na mapepo yanayotawala eneo na yanayojaribu kuzuia injili isienee kwa kuwatia umaskini watumwa wa Kristo.

6. Sema Na Milima, Mito Na Miamba

Mara kwa mara sema na kila mlima wa kutindikiwa na umaskini, na kuuamuru kuondoka kwa jina la Yesu. Ustahimili mpaka yatokee (Mk 11:22,23).

Sema na mto unaoleta furaha katika mji wa Mungu, yaani Yerusalemu, ambayo haina mto wa asili. Amuru mto wa Mungu utiririke kupitia katika maisha yako ili upate kuwagawia wengine maji (Zab 46:4).

Sema na mwamba, ambao kanisa limejengwa juu yake (Mt 16:8), na maji yatatiririka. Kamwe usimpige Kristo wala kanisa katika kufadhaika kwako (Hes 20:8-11).

Vita vya kiroho maana yake ni kuwa mtu yuleyule unapokuwa hadharani na unapokuwa faraghani. Lipa bili zako kwa wakati wake na kutunza kumbukumbu za kweli (2Kor 8:21).

7. Sasa Achilia Mavuno Yako

Fanya hivyo kwa kutoa kwa ukarimu na kwa furaha katika jina la Yesu (2Kor 9:6-8).

Usimwibie Mungu, kila mara lipa zaka zako (Mal 3:8-12) (Kum 14:22-29).

Malimbuko (Kum 18:4) (Mit 3:9).

Panda mbegu za sadaka (2Kor 9:6).

Usiwasahau maskini (Kum 15:7-10).

 

"Mungu hatakosa kuwajazi wale wote wanaoifanya kazi yake sawasawa na mapenzi yake".

Hudson Taylor, China.

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina.

Moldova

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Jat (Jati, Jatu)

Jakati

156,000




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk