1985 - 2007

 

49. Uchumi Wa Ufalme

Mbinguni kuna benki pia

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Mwanzo 41

Mstari Wa Kukariri
Nami nawaambia, jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele (Lk 16:9).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Athari za madeni kwa mtu binafsi, familia, kanisa, na taifa. Linganisha manufaa yake kwa upande mmoja, na gharama na upotevu wa uhuru kwa upande mwingine.
Je, kuna njia bora zaidi ya kukopa fedha?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Soma Kum 15:6-11 na kwa pamoja andaeni mapendekezo ya kuanzisha ‘Benki ya Kikristo’. Je, mtapataje mtaji ili kuwakopesha maskini bila riba au kwa riba kidogo sana? Wakopaji watatumia fedha hizo kwa kuanzisha miradi midogo midogo ili kuwategemeza.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Tafakari wakati wa mbegu na mavuno, kupanda na kuvuna. Andika ukurasa mmoja ukionesha mifano ya asili na ya kiroho mahali ambapo kanuni hii inaweza kutumika na kuleta mavuno mengi.

Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Mithali 14:23

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Georgia. Idadi ya watu ni 5,600,000.

Kumekuwepo na mvutano na uharibifu baada ya uhuru. Asilimia 57% ni Orthodox, na asilimia 0.43% ni wafuasi wa madhehebu ya Kiinjili.

 

Hali ya uchumi wa taifa lako; ikiwa uchumi unakua, au ikiwa haukui, au pengine unaporomoka, hayo hayatokei kwa bahati mbaya. Hali hii inatokana na maamuzi yanayochukuliwa kutokana na shinikizo la masuala ya kiuchumi na imani za kisiasa ndani na nje ya nchi. Baadhi ya mataifa yamechagua ubepari, mengine yamechagua ujamaa au ukomunisti. Baadhi ya mataifa yamehifadhi soko lao na sarafu yao, mengine yanafuata mfumo wa soko la ulimwengu. Ni suala la itikadi na maamuzi ya serikali na mabenki.

Uchumi Wa Ufalme

Si jambo la ajabu kwamba hata katika Ufalme wa Mungu pia kuna sera za kiuchumi zilizobuniwa katika misingi ya upendo na hekima na mfadhili mkuu wa ulimwengu. Ukiweza kugundua kanuni za uchumi wa Ufalme wa Mungu na kuzitumia katika maisha haya utapokea baraka, amani na mafanikio. Kutokuzijua kanuni za Ufalme, au kuzijua na kutokuzitumia kunaweza kukamsababishia mtu kuongozwa na mfumo wa kidunia ambao huwafanya maskini watu walio wengi, na kuwanufaisha wachache. Je, ni zipi hizo sera za kiuchumi, utekelezaji wake, na kanuni za Ufalme wa Mungu?

1. Dunia Ni Mali Ya Bwana
Mungu ndiye Mwumbaji, na mmiliki halali. Umiliki wake una makusudi yanayoeleweka na yaliyo wazi, na hatima yake pia inajulikana. Mwumbaji huyu ametangaza, amechapisha na kuweka milele sheria za kiroho na za asili zenye manufaa kwa ulimwengu. Sheria hizi zinaweza kuvunjwa na mwanadamu kwa uharibifu wake mwenyewe (Mwanzo 1) (Zaburi 24:1, 2).

2. Dunia Amekabidhiwa Mwanadamu
Mungu akiwa mmiliki wa dunia amewapa wanadamu, wake kwa waume, dhamana ya kuiendeleza sayari hii. Tunatazamiwa kuitawala dunia kama mawakili wema, kuitunza, kugundua utajiri uliomo na kuutumia vizuri kwa manufaa ya wanadamu wote. Tunaitumia dunia vibaya na kwa kufanya hivyo kujiweka katika hatari (Mwa 1:26-31) (Zab 8:6; 115:16).

3. Majukumu Maana Yake Ni Uwajibikaji
Majukumu yote na kutegemezwa huleta moja kwa moja hitaji la kutoa hesabu kwa mmiliki kuhusu maendeleo ya majukumu hayo. Mungu anamtaka mwanadamu kutoa hesabu ya matendo yake; na mwanadamu pia anamtaka mwanadamu mwenzake kuwajibika kazini na kanisani. Mti wa uzima ulijaribu uaminifu wa mwanadamu pale Edeni na baada ya kushindwa Adamu alilazimika kutoa hesabu (Mwa 2:16; 3:4-6).

4. Kazi Ni Baraka Na Wala Si Laana
Kazi ni njia ya Mungu ya kupatia mafanikio. Adamu alipewa kazi yenye dhamana kabla ya anguko na Yesu akasema kwamba, “Baba yangu anatenda kazi, nami pia natenda kazi”. Uvivu humpeleka mtu kwenye umaskini (Mwa 1:31-2:3) (Yn 5:17) (Mit 12:24; 14:23).

5. Ufanisi Ni Kiwango Pekee Cha Mungu
Ni mfano wa Mungu mwenyewe kwetu tangu mwanzo. Tunamfanyia kazi mwanadamu kama vile Mungu ndiye mkaguzi na msimamizi wetu wa kazi anayeonekana (Mwa 1:31) (Zab 8) (Efe 6:7).

6. Familia Ni Kikundi Cha Kiuchumi Cha Mungu
Familia hufanya kazi sawasawa wakati vipaji vinapotumika kwa faida ya wote. Kuwarithisha watoto ujuzi kunawafanya wazazi kupokea tunu uzeeni. Wakuu wa kaya waliulinda uchumi wao kwa kuishi, kufanya kazi na kusafiri kwa pamoja.

7. Uaminifu Ni Kipimo Cha Mungu
Mwanadamu hutafuta mafanikio ila Mungu anatafuta uaminifu. Anatujaribu kwa vitu vidogovidogo vya kufanya, nasi pia tunawajaribu wengine kwa njia iyo hiyo. Uaminifu husababisha kupandishwa daraja (1Kor 4:2) (Lk 19:11-26) (Lk 16:9-12).

8. Fedha Zinabadilishana Na Uzima
Tunda la kufanya kazi ni kuwa na fedha mifukoni mwetu; kwahiyo si kwamba tunamrudishia tu Mungu fedha kwa njia ya zaka na dhabihu, lakini ni uhai. Kiasi tunachotoa ni kipimo cha kiasi tunachohusika kwa Yesu (Lk 16:11) (Mt 6:19-21) (Mal 3:8).

9. Mafunzo Kazini Huleta Ustawi
Kujifunza masomo ya kiroho na ya asili kutoka kwa wengine kunatuongoza katika ubunifu, maendeleo na ustawi. Njia aliyoichagua Kristo ya ufuasi, neno lingine la kujifunza kwa kufanya kazi chini ya mtu mwingine, ina maana ya kuonesha na kuachilia wengine (Lk 5:10) (Mt 28:19).

10. Kukua Maana Yake Tumtangulize Mungu Biblia inatufundisha kwamba kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake ndiyo msingi wa kupatikana kwa mahitaji ya mwanadamu. Mifumo ya kisiasa ni njia zinazopendelewa zaidi kwa kutumia hekima inayopokelewa na mwanadamu kutoka ama kwa Mungu au kwa Shetani (Mt 6:33) (Kol 2:8).

11. Utii Ndiyo Njia Pekee Kuwa mtiifu kwa njia za Mungu ndiyo ufunguo wa kuachilia mafanikio katika ulimwengu huu wenye matatizo mbalimbali (Kum 8:18, 6-10) (Kum 28:1) (Zab 1) (Yos 1:8) (Kum 28).

12. Ubia Huleta Mafanikio
Ubia huleta ‘chuma kunoa chuma’, ubunifu wa hali ya juu na wingi wa mafao. Mfanye Kristo, aliye mchumi mkuu, kuwa mbia wako mwandamizi, na kisha waamini wengine wenye mawazo kama yako (1Kor 3:9) (2Kor 6:15) (Mhu 4:9-12).

13. Ipo Sheria Ya Kudumu Ya Kupanda Na Kuvuna
Kupanda kwa ukarimu hutangulia mavuno makubwa, na matukio hayo mawili hutenganishwa na kipindi cha saburi, tumaini na imani (Mwa 8:22) (1Kor 15:42-58) (Lk 6:38) (2Kor 9:6).

14. Utajiri Ni Lazima Utunzwe
Utajiri unalindwa kwa kuwa na busara katika kuutumia, kuandaa bajeti, kubana matumizi, kuhifadhi na katika kuwekeza (Kum 6:10-16) (Mwa 41:25-40).

15. Madeni Ni Hatari
Madeni hayo mara nyingi yanatokana na kiburi au ukosefu wa subira. Yanadanganya, yanakatisha tamaa katika kipindi kigumu kiuchumi, na yanaharibu familia (Kum 28:44) (Rum 13:8).

16. Fedha Si Utajiri Wa Kweli
Utajiri wa kweli huja kutokana na matumizi sahihi ya fedha kuwaleta wenye dhambi kwa Yesu, na kuwabariki watu wenye uhitaji hapa duniani kwa uaminifu, kwa shukrani na kwa ukarimu ( Lk 12:15, 48; 16: 9-13) (Mit 11:24-26).

17. Ni Lazima Pawepo Na Uwiano Kati Ya Kazi Na Mapumziko
Kutunza afya na familia ni jambo muhimu na la kimaendeleo, na Mungu aliweka kanuni ya Sabato ili kuwepo na siku za kupumzika wanadamu wapate kumkumbuka yeye na baraka zake, na katika kuhuishwa (Kum 5:12-15) (Kut 31:12-17).

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Mongolia

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Uzbek

Uzbek, Northern

20,000




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk