1985 - 2007

 

53. Hatima

Martin Luther King alifanya maisha yake yawe na maana kwa msaada wa Mungu

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Yeremia 1

Mstari Wa Kukariri
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” (Yer 1:5).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Kuishi ni mara moja, na maisha yanapita haraka, lakini yale yaliyofanywa kwa ajili ya Yesu yatadumu. Ikiwa kauli hiyo ni ya kweli, ni mabadiliko gani ya dhati utakayoyafanya?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Andika maono yako kutoka kwa Mungu, ya familia yako, na ya huduma yako ya Kikristo. Weka malengo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kwa kila eneo, na kuhakikisha kwamba yote yanakubaliana na kanuni kama inavyoelekezwa katika somo hili.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika taarifa ya kweli au ya kubuni kuhusu mpango wa kuandaa mkutano wa injili. Tumia yale maswali saba vizuri.

Tafakari Mistari Hii Neno Kwa Neno
Yeremia 29:11-14

Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Brazil. Idadi ya watu ni 165,000,000. Watu wa rangi zote. Wengi ni maskini na hawajafikiwa. Inatisha kwamba asilimia 22% pekee ni wafuasi wa madhehebu ya Kiinjili. Wengi wanaabudu mapepo.

 

Chagua hapa > 53chart upate kuona mchoro kwa ajili ya somo hili

 

Uislamu na baadhi ya dini nyingine hufundisha kwamba wanadamu ni kama majani yanayoanguka wakati wa msimu wa kuanguka majani na kuchukuliwa na mto wa maisha kutupeleka unakotaka, na kutuacha kwenye ukingo wa mto au kutumwaga kwenye bahari ya umilele.

Kinyume chake, tukiwa ndani ya Kristo, kwa imani na maombi, ambayo huleta ufunuo, tunaweza kujua mpango wa Mungu katika maisha yetu. Lakini tusipokuwa watiifu katika maisha yetu ufunuo huo utabaki kuwa wa kimaono tu na hautatufaidia cho chote sisi wala ulimwengu huu kwa kipindi cha kuishi kwetu.

Kugundua Mpango Wa Mungu Kwa Maisha Yako

Maisha yaliyofanikiwa yana mizizi imara katika Mungu, na yanashamiri kwa utukufu wake. Kupata mwelekeo sahihi, ambao utafanya maisha yako yawe ya faida, kwa kuubadilisha ulimwengu huu uwe bora, si ndoto ya siku moja; bali ni mwunganiko wa umilele, wakati uliopita, wakati uliopo na ufunuo wa kinabii wa Mungu aliouchagua kwa ajili yako.

1. Ulijulikana Katika Umilele Uliopita

Kabla ya kuwako kwa nyakati kulikuwa na mazungumzo mbinguni kuhusu maisha yako (Yer 1:5) (Gal 1:15) (Zab 139:15,16).

Mungu Alikuchagulia:
Tarehe ya kuzaliwa na mahali pa kuzaliwa; rangi na wajihi wako; wazazi wako na historia ya familia yako, ikiwa ni tajiri au maskini. Kwahiyo unaweza ukachukulia kwamba bado ana mpango wa maisha yako yaliyobaki.

Siku Za Nyuma Uliandaliwa
Tangu ulipozaliwa mikono ya Bwana iliyojeruhiwa imekuwa ikikuandaa kwa namna ya kipekee.

Umefinyangwa Na Mfinyanzi Mkuu
kupitia uzoefu mzuri au mchungu, ndani ya familia au kwenye mazingira mbalimbali, mafundisho ya shuleni au kwenye dini hata kama si ya Kikristo. Je, waweza kuona alama za vidole vya Yesu katika maisha yako yaliyopita akikupa neema ya maisha yote na ulinzi dhidi ya ajali na uovu katika shule ya maisha? Unaishi wakati wengine wamekufa!

2. Kisha Maisha Yakaanza Kweli

Alikuleta na kukufikisha mahali ambapo ulianza kuhisi utakatifu wake, na ukajisikia kuhukumiwa kwa habari ya dhambi zako, ukikabiliana na umilele wa waliopotea. Roho wake alimdhihirisha Mwokozi wako, Yesu, na akakupa imani ya kumwamini na kufanyika mfuasi wa Mwana wa Mungu.

Kipindi Cha Fungate Cha Mungu
Waamini wapya huonekana kufurahia na Bwana kipindi cha mwanzo kabisa cha wokovu wao ambapo Baba humimina upendo wake na furaha kwa familia yake mpya. Ni wakati wa kuponywa na kuwekwa huru kutokana na kushikiliwa na Shetani kwa muda mrefu. Halafu neema na furaha ya ubatizo wa maji na wa Roho (Efe 2:1-10).

3. Wito Wa Wakati Huu

Haichukui muda mrefu kabla hatujagundua kwamba Mungu ana mipango kwa ajili yetu, na hamu yetu ya kutaka kujua mambo inaamshwa (Yer 29:11).

Kwanini Tuko Hapa?
Katika Yn 13:3 tulijifunza kwamba, kama ilivyokuwa kwa Yesu, tumetoka kwa Mungu, na tuko hapa kwa ajili ya Mungu, na siku moja tutarejea nyumbani kwa Mungu. Kwa kulijua hilo, Yesu, aliye Mwumbaji wa ulimwengu na Bwana wa yote, alikuwa na furaha na kujiona salama, na aliweza kuhudumu hata kwa kuwatawadha miguu wanafunzi wake.

Mwombe Mungu Akuoneshe Mpango Wenyewe
Katika Efe 2:10 tunaambiwa kwamba Mungu tayari ameandaa kazi kwa ajili yetu ili tuzifanye. Kwahiyo tafuta kutoka kwa Bwana upate kujua ni kwanini ulizaliwa na kisha ukazaliwa mara ya pili. Yajue makusudi ya Mungu na kazi Yesu aliyokuandalia (Yn 15:16).

Andika Maono Hayo Kwenye Karatasi
Soma (Kut 31:18) (1Nya 28:19) na (Ufu 1:19).

4. Sasa Panda Maono Ya Siku Zijazo

Kama mbegu katika maombi, iache mikononi mwa Mungu, ikisubiri siku maisha mapya na mavuno yatakapotokea (Yn 12:24).

5. Weka Malengo Yanayoeleweka Kuupa Sura Wito Wako Na Siku Za Baadaye

Malengo yaliyo wazi yatakurahisishia mawazo yako, maombi yako, kumbukumbu zako, rasilmali, na zinaachiliwa nguvu kubwa kuliko unavyoweza kufikiria.

Sifa Za Malengo Yanayotekelezeka:

Yanaonekana waziwazi, hayana utata.

Yanapimika, kuona maendeleo.

        Yanaweza kufikiwa, hakuna shaka.

Zoezi hilo liko wazi, linaweza kurudiwa na watu wengine.

Lengo linaweza kupangiwa muda wa kuanza na muda wa kukamilika.

Waweza kuwa na malengo ya muda mfupi, kwa mfano miezi mitatu; malengo ya muda wa kati, kwa mfano miaka miwili; na malengo ya muda mrefu, kwa mfano miaka kumi.

6. Pangilia Kwa Kuweka Kipaumbele

Hakuna mtu awezaye kutekeleza mambo sita kwa wakati mmoja, kwahiyo andaa orodha ya mambo mengi unayotaka kuyafanya katika familia yako na katika huduma ya Kikristo. Kisha jiulize swali hili: Iwapo Mungu ataruhusu malengo sita tu kati ya haya niliyoorodhesha, yatakuwa ni yapi, na orodha yake kwa kipaumbele itakuwaje? Kupanga malengo yako kwa kipaumbele kunakupa uwezo zaidi.

7. Majibu Mazuri Huleta Mipango Mikamilifu

Ili kuweza kuandaa mipango mikamilifu hata kwa mradi mdogo wa kanisa jiulize maswali saba yafuatayo. Majibu yake yatakupa wewe mpango mkamilifu.

Ni nini hasa ninachotaka kufanya?

Ni kwanini ninataka kufanya jambo hili?

Ni wapi hasa ninakotaka kufanyia jambo hili?

Ni lini nitakapoanza na ni lini nitakapomaliza?

Ni nani atakayenisimamia, kufanya kazi pamoja na mimi; na ni nani atakayenufaika na mpango wangu?

Ni kwa namna gani nitatekeleza kazi hiyo? Hatua ya kwanza, ya pili, n.k.

Ni nini gharama yake? (Lk 14:28,29).

8. Sasa Anza Kutekeleza Mpango Wako

Kwa sababu imani bila matendo imekufa. Uwe tayari kutumia muda wako, nguvu zako, maombi, fedha, hadhi, na heshima ukijua kwamba utendaji kazi kwa bidii huleta faida (Mit 14:23). Usisahau kupokea ushauri mwingi na kujifunza kutoka kwa wengine. Fanya tathmini ya maendeleo kila baada ya miezi mitatu na mwaka mmoja na kufanya mabadiliko yo yote ya lazima.

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina 

Niger

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Iberogen

Iberogen

20,000

Igdalen

Igdalen

15,000

Maure (Moor)

Arabic, Hasaaniya

127,400




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk