1985 - 2007
54. Ustahimilivu
Bi. Cory Aquino alistahimili hata kuwaletea Wafilipino mapinduzi ya amani
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika
Biblia Yako Soma
Danieli 10
Mstari
Wa Kukariri
Basi mtiini Mungu.
Mpingeni Shetani, naye atawakimbia (Yak 4:7).
Baadaye
Zungumzieni Jambo Hili
Katika Mdo 16:6-10
Roho Mtakatifu alimzuia Paulo, katika 1The 2:18
Shetani alimzuia, na katika 1Kor 16:12 Apolo mwenyewe alikuwa hataki. Unasemaje
kwa nafsi yako; ni nani anayekuzuia?
Jambo
La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Kila mmoja wenu
atafute waamini wawili wapya kutoka kwenye kanisa lo lote. Watembelee na kuwatia
moyo. Huenda ikawa wanakabiliwa na upinzani wa kila namna.
Kazi Ya
Kuandika Ya Stashahada
Shetani alimzuia
askari mzoefu kama Paulo. Wewe unafikiri alimudu vipi kumzuia? Andika maelezo ya
ukurasa mmoja.
Tafakari Mistari Hii Neno Kwa Neno
1Pet 5:6-11
Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Yordani. Idadi ya watu ni 4,000,000; ni Waarabu. Asilimia 94% ni Waislamu; na watu 7,000 ni wafuasi wa madhehebu ya Kiinjili.
Je, umewahi kuona ni nini kinachotokea mtu anapoamua kumfuata Yesu? Wanafamilia ghafla wanakuwa wataalamu wa mambo ya kidini, na malumbano yanaendelea. Ukitaka kuona jinsi tabasamu linavyotoweka haraka katika nyuso za watu, taja mambo kama ubatizo wa maji, kujazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha.
1. Mtu Anachukia!
Katika Efe 6:12 tunaambiwa kwamba vita vyetu si dhidi ya nyama na damu; kwahiyo ni Shetani na mtandao wake mwovu ndiye anayepinga:
Wokovu Wetu
Ni pale Shetani anapolazimika kuachia, na mbaya zaidi kwake, ni pale Mungu anapoingia ndani mwako.
Ubatizo wa Maji
Ni pale utu wa kale wa dhambi unapokatiliwa mbali.
Ubatizo wa Roho
Ni pale utu mpya unapowezeshwa.
Shetani anaposhindwa, hatua inayofuata ni kujaribu kuwafanya wafuasi wapya wawe vipofu kwa maana ya kwenda kanisani kila Jumapili na kutoa senti kidogo kila wiki, basi.
2. Songa Mbele, Kwa Ajili Ya Yesu
Sasa ukithubutu kuombea umisheni, ni lazima uchukue tahadhari kwa milipuko ya hofu ndani yako, matatizo ya kifamilia, na hata kutokuelewana ndani ya kanisa. Hii ni kwa sababu umisheni ni kama gari la kumbebea mfuasi wa Yesu aliyezaliwa mara ya pili, anayeishi maisha ya ushindi, aliyejazwa Roho, anayeongozwa na Roho; ili kuleta mabadiliko makubwa katika ulimwengu unaomzunguka kwa ajili ya Kristo.
Biblia inatuambia kwamba watu wasiokuwa na maono huangamia (Mit 29:18), na hilo ndilo Shetani analolitaka. Kwanza anataka uangamie kwa kuchoshwa na maisha ya ukristo, na kisha anataka ulimwengu wa watu atakaoangamia nao milele. Maisha yako yakiwa mikononi mwa Roho Mtakatifu inaweza kuwa sababu ya watu wengi, wake kwa waume, kupokea uzima wa milele.
Ni Mmoja Tu Kati Ya Mia Moja
Inakuwaje kwamba ni mmoja tu kati ya waamini 100 wanaokubaliana na umisheni, ambao kweli wanashiriki shughuli za umisheni? Je, kuanza maisha ya ndoa, au ajira, au masomo, au ukata vyaweza kuwa sababu ya kweli? Au kuna mikono ya siri ambayo inakula njama kuwazuia waamini wapya, wachungaji, wazee, na hata kanisa kwa ujumla lisitekeleze Agizo Kuu?
3. Ni Nani Anayekuzuia Wewe?
Je, Ni
Roho Mtakatifu?
La kushangaza ni
kwamba ni Mungu; Roho Mtakatifu atakuwa wa kwanza kukuzuia wewe kama rafiki.
Ikiwa uko tayari kutumika unafanyika mtu wa thamani kiasi kwamba Roho Mtakatifu
atakuzuia iwapo ataona kwamba kuna kasoro katika mwelekeo wako, mbinu zako au
hata muda wako (Mdo 16:6-10) (Isa 30:21).
Je, Ni
Pepo Mchafu?
Kama kuna jambo
wasilotaka kulisikia roho za mpinga-Kristo ni habari za kuhubiriwa Injili kwa
mataifa yote na kurejea kwa Mfalme. Kutoka ndani ya ngome zao za imani
mbalimbali za ulimwengu huu kama vile Uislamu, hutukebehi kwa kusema, “Hamwezi
kuingia hapa. Angalia jinsi tulivyo jeshi kubwa; jinsi tulivyo wengi
tunaopingana na ninyi wachache mliogawanyika!”. Lakini katika 1Nya 11:4,5 kwa
msaada wa Mungu Yerusalemu ilianguka pamoja na ubishi wake; na hivi karibuni
Ukuta wa Berlin ulianguka, na tumeshuhudia pia kuporomoka kwa Ukomunisti. Wakati
mwingine tunaweza tukadhani kwamba sisi ni wadogo na wanyonge kama theluji,
lakini chembechembe za theluji zinapokusanyika pamoja huuzuia mji!
Je, ni nini kimewatokea wale mapepo wakuu wa Uyunani na Uajemi, au miungu wa siku za Elia, na wenzi wao wa Kirumi na Kiyunani katika siku za Paulo, Ziasi na Herme kwa mfano? Je, unafikiri wamefutika? La hasha! Hawa ni viumbe wasioathiriwa na muda au kifo; na mkakati wao wa kudumu ni uovu na kuwashikilia kwenye giza watu wa vizazi vyote. Kwahiyo mkuu wa anga la Mexico akijua unakuja anaweza akaandaa migomo kwa ajili yako ili kukukatisha tamaa kabla hata hujaanza safari. Kwahiyo wala usishangae ukiona mgogoro wa ghafla unazuka kwenye familia au kwenye kikundi wakati hukuutazamia kabisa.
Je, Ni
Roho Yako Mwenyewe?
Watu wengi ambao
hawajafikiwa na Injili wako tofauti sana na sisi, na si watu wengi waliookoka
ambao wako tayari kwenda kuishi nao na kuwaonesha Yesu. Tunaweza kuziona sababu
zake katika Mwa 12:1-3, pale Abramu anapoitwa na Mungu. Shetani ni bingwa wa
kutia mambo chumvi, na vilevile kutia watu hofu.
Vikwazo Vya Kijiografia
Ni kwa sababu tunalazimika kuiacha nchi yetu tuliyoizoea.
Vikwazo Vya Kitamaduni
Ni kwa sababu tunalazimika kuwaacha watu tuliowazoea na desturi zetu.
Changamoto Za Kijamii
Ni kwa sababu tunalazimika kuiacha familia na kanisa, na kuwaendea watu ambao tunawashuku na wao pia wana mashaka na sisi.
Hofu Binafsi
Mawazo hutunyima usingizi usiku tunapokuwa tukipambana na hofu ya kutokumudu mambo fulani fulani, hofu ya mabadiliko katika maisha, hofu ya kukosekana fedha au kushindwa katika lugha. Ukweli ni kwamba tumezoea starehe na urahisi wa mambo; tukienda kanisani tunakuta tumeshaandaliwa kila kitu. Tunapokwenda mahali pengine, yawezekana sisi tukawa ndio kanisa kwa ajili ya mtu mwingine!
4. Kulishinda Giza
Zishinde njama dhidi yako kwa kuchukua hatua za Kimungu:
Fuata wito wa Mungu; ukisukumwa na upendo wa Kristo (2Kor 5:14).
Ukubali kuwa mwanafunzi hadi ukomae. Ushindi hupatikana kutoka penye udhaifu kwa maombi, vita vya kiroho, hekima na kutegemezwa na ushirika wa viongozi na marafiki wanaotaka kuona mafanikio yako.
Uwe tayari kufundishwa Biblia na stadi.
Ukubali kujifunza kwa kufanya kazi.
Hatimaye, uwasaidie wengine walio wachanga.
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina
Oman |
||
Jina la watu |
Lugha yao |
Idadi yao |
Mahra |
Mahri |
109,000 |
Persian (Irani) |
Farsi, Western |
38,000 |
Shihuh |
Arabic, Shihhi Spoken |
10,000 |
1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya
for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk