1985 - 2007

 

56. Kanuni Ya Matayarisho

Mwanaanga na mwamini Buzz Aldrin alikuwa ni Mkristo aliyejiandaa

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Isaya 49

Mstari Wa Kukariri
Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako (Isa 43:4).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Jadilini jinsi mlivyojisikia kuhusu stadi ya yule mfinyanzi na yule mhunzi anayetengeneza mishale maishani mwenu.

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Angalia uwezekano wa kumtembelea mfinyanzi ili kuona anavyofanya kazi zake tangu mwanzo hadi mwisho. Mtembelee pia mhunzi uone anavyotengeneza mishale.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Chunguza sifa za kiutendaji za watu wanaojitokeza katika vitabu vya Kutoka, Timotheo na Tito, kisha andika katika ukurasa mmoja ukiwaelezea katika maisha ya sasa.

Tafakari Mistari Hii Neno Kwa Neno
Yer 18:1-6

Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Ufilipino. Idadi ya watu ni 70,000,000. Kuna ukuaji mkubwa na wa ghafla wa kanisa. Idadi kubwa zaidi ya watu ni Wakatoliki; asilimia 5% ni madhehebu ya Kiinjili. Umaskini umeenea.

 

Viongozi Wanazaliwa Au Wanaandaliwa?

Je, unajua kwamba malighafi ni lazima iandaliwe ndipo iuzwe na kutumika? Kwa mfano mafundi stadi wanaweza kutumia malighafi zifuatazo kutengeneza vitu vipya ~

Waweza pia kuona kanuni ya Mungu ya maandalizi katika maisha ya asili. Kwa mfano wanyama hujiandaa kwa msimu wa baridi; ardhi huandaliwa kabla ya kupandwa mazao; na mawe yenye ncha kali hulainishwa na maji yanayotiririka.

Wakati tunapookolewa na kuitwa na Mungu tunamjia tukiwa ghafi pia; na wala hatufanani hata kidogo na namna tutakavyokuwa baada ya kutayarishwa na Mungu. Rundo la mawe haliwi nyumba mpaka limeandaliwa na kuwekwa pamoja kwa mujibu wa michoro. Halikadhalika rundo la ‘mawe yaliyo hai’ haliwezi kuwa nyumba ya kiroho au kanisa mpaka yaandaliwe (1Pet 2:5).

Mbegu Na Mmea Huja Kabla Ya Tunda

Kiongozi huzaliwa, kisha huzaliwa tena, akaitwa na kupakwa mafuta, lakini kabla hajawajibika na kumzalia Bwana matunda, kuna kipindi cha kutayarishwa. Kiongozi anaweza akakwepa hatua hiyo muhimu au akatafuta njia ya mkato, lakini jambo hilo linaweza kuwa la hatari kwake na kwa watu wa Mungu baadaye.

Kanuni Ya Matayarisho

Kwa kuwa Mungu anapenda utaratibu na ufanisi na anachukia sana mambo ya wastani, katika nyakati za Biblia ilibidi baadhi ya mambo yafanyiwe maandalizi:

Kila fundi stadi anahitaji miaka ya kujifunza kwa kufanya kazi, na viongozi hodari wa Mungu ni vivyo hivyo. Yoshua alikaa na Musa kwa miaka; Elisha naye alikaa na Eliya kwa miaka; Timotheo pia alikaa na Paulo kwa miaka.

Mungu Anawaandaaje Viongozi?

Isaya 49:1-6 ni lango la kuingilia kwenye chuo cha Mungu cha mafunzo; na kozi yenyewe itakamilika utakapoimaliza! Unaweza ukaamua kuacha chuo kikuu, lakini shule ya Mungu inakufuata na iko karibu na wewe (Zab 139:7-10). Kuhitimu kunategemea juhudi yako; ukijifunza kwa bidii utahitimu mapema. Isaya anatabiri jinsi Mungu atakavyomwandaa Yesu kwa maisha na huduma. Mchakato mzima wa maandalizi ulikuwa kweli kwa Isaya mwenyewe, na unatufaa hata sisi leo. Hebu sasa tuangalie masomo yaliyoko katika Shule ya Roho.

Masomo Kuhusu Mwelekeo Na Hatima

Viongozi ni lazima waelewe kuwa waliitwa hata kabla ya kuzaliwa kwao na kupitia kwenye mkondo wa makusudi ya Mungu ya milele (Isa 49:1) (Gal 1:15) (Yer 1:5) (Isa 9:6) (Efe 1:4).

 

Masomo Kuhusu Kunena Uzima

Mungu anatenda jambo katika ndimi zetu ili kufanya maneno yetu yawe makali kama upanga na sio butu na mabaya.

 

Masomo Kuhusu Ufinyanzi

Anatuficha katika uvuli wa mikono yake (Isa 49:2), ambayo ni picha ya Mfinyanzi Mkuu akitufinyanga sisi, tulio udongo wa mfinyanzi (Yer 18:1-4). Yesu anatumia mikono yake iliyojeruhiwa na ‘mkono’ wa duniani ambao ni wajenzi wake wakuu watano (Efe 4:11).

 

Je, ulijua kwamba udongo wa mfinyanzi huchimbwa kwanza na kutengwa? Udongo huo huoshwa na kulowekwa kwenye maji, hupondwapondwa na kushindiliwa vema na kwa kutumia waya mwembamba kuondoa mapovu ya hewa. Kisha unazungushwa tena na tena kwenye gurudumu, unanyoshwa na kuvutwa tena na tena, na baadaye huwekwa pembeni ili uwe mgumu. Halafu moto! Labda hilo litakusaidia kuelewa ni nini kilichokuwa kikikutokea?

 

Masomo Kuhusu Utengenezaji Wa Mishale

Mungu amekusudia kuwafanya viongozi wake kuwa kama mishale iliyosuguliwa (Isa 49:2). Katika zama hizo mishale ilikuwa ikitengenezwa kutokana na mti wa msonobari ambao sura yake si laini, umejisokotasokota na kuwa na makovu; sawasawa na tabia ya mwanadamu kabla hajampokea Yesu!

 

Mpini wa mshale huchongwa mara kwa mara, unapigwa msasa na kunyooshwa vizuri, unapakwa mafuta, ishara ya Roho Mtakatifu, ili kuponyesha majeraha, na hatimaye kuunganishwa kwenye kichwa cha mshale wenyewe. Lengo la matayarisho yote hayo ni kuhakikisha kwamba kila mara mshale unafika unakoelekezwa kwa usahihi.

 

Ile ncha ya mshale ni karama ya huduma, lakini ule mpini unawakilisha tabia ambayo kwayo viongozi huinuka au kuanguka, na ni sifa muhimu ya kiutendaji katika huduma (Kut 18:21) (1Tim 3) (Tito 1:5-9). Umewahi kuhisi Mungu akiwa kwenye mchakato wa kunyoosha mambo? Sasa unaelewa ni kwanini!

 

Masomo Ya Kuwa Na Subira

Baada ya maandalizi yote hayo yaliyojawa na kazi ngumu na machungu, unaweza ukadhani kwamba sasa unaweza kuongoza, lakini badala yake Mungu anakuweka kwenye podo lake pamoja na mishale mingine yote mipya. Anakuficha usiwe hadharani (Isa 49:2). Hautapita muda mrefu kabla misimamo yote mibovu ya mifadhaiko, uasi na uhuru haijakutoka. Wengine husema, “…Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida;…” (Isa 49:4), lakini subira na utiifu mtu hujifunza kwa kutenda.

Hatimaye Inakuja Siku Ya Kuhitimu

Pamoja na tuzo kwa mateso yote. Lakini Bwana anasema hivi, “…Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia” (Isa 49:5,6). Gharama za kutumiwa na Mungu ni subira katika kumruhusu yeye kukuandaa kuwa mtumishi bora wa Mungu.

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Pakistan

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Hindko, Southern

Hindko, Southern

625,000

Khetrani

Khetrani

10,000

Kolai (Kohistani-Shina)

Shina, Kohistani

200,000

Sansi Bhil

Sansi

20,000




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk