
1985 - 2007
59. Majaribu
Rais Nixon wa Marekani aliitwa kusimama lakini akaanguka kwenye jaribu
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika Biblia Yako Soma
1Tim 6:3-21; Dan 4:28-37; 1Fal 19
Mstari wa Kukariri
Ushiriki taabu pamoja nami, kama
askari mwema wa Kristo Yesu. Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za
dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari. Hata mtu akishindana katika
machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali (2Tim 2:3-5).
Baadaye Fanyeni Haya
Gawanyikeni katika makundi mawili
na kisha ulizaneni maswali yahusuyo uadilifu na uaminifu.
Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana
Tena
Kama nyumbani kwako kuna vitu
visivyostahili kuwapo, kwa mfano majarida, vitabu, video na sanamu; vilete na
kwa pamoja mvichome moto kwa jina la Yesu.
Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika taarifa ya ukurasa mmoja
ukielezea jinsi majaribu yanavyoweza kukuathiri.
Tafakari Andiko Hili Neno Kwa Neno
2Tim 2:20,21
Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Uingereza. Idadi ya watu ni 46,000,000; wengi ni watu wa kawaida waliopotea kiroho. Wengi wanatazamia uamsho mwingine; makanisa mengi yamehuishwa.
Mpango wa Mungu sikuzote ni kuinua viongozi watakaomtumikia kwa uaminifu maisha yao yote; lakini mpango wa Shetani ni kumpiga mchungaji ili kwamba kondoo wa kundi lake watawanyike. Sisi hatukosi kuzijua fikira zake zinazoweza kutuletea hatari kama hizo (Zek 13:7) (2Kor 2:11).
Majaribu
Kule nyikani Shetani alimjaribu Yesu kwa kumshawishi atumie vibaya nafasi yake na uweza wake wa kiroho ili kujipatia riziki; kisha akamshawishi achukue njia ya mkato ili kuepuka mateso; na hatimaye Shetani akapendekeza kujikweza. KiIa wakati Yesu alisema, Hapana! Uamuzi utakaoufanya sasa unaweza kuokoa maisha yako baadaye.
Majaribu mengine yanayowakumba viongozi yanaitwa ‘wasichana, madaraka na dhahabu’.
Wasichana (Wavulana !), Matumizi Mabaya Ya Ngono
Ukiruhusu sikio lako kusikia maneno ya mapenzi au jicho lako kuona picha za mapenzi, kunaweza kukusukuma kufanya ngono nje ya ndoa, na hasa unapokuwa mpweke, unapokuwa kwenye mawazo mazito, au unapokuwa safarini. Anguko litaathiri huduma, ndoa na heshima yako; na wengi hawatakuamini tena (Mit 6:20-35; 5:7-14).
Madaraka, Matumizi Mabaya Ya Nafasi
Utaweza kusikia majivuno ya watu kama vile, ‘mimi’ ndiye niliyefanya hili na lile, badala ya kumtukuza Mungu. Kiburi kilisababisha anguko la Shetani na tangu hapo amedanganya viongozi wengi (Dan 4:28-37) (Mit 16:18; 29:23).
Dhahabu, Matumizi Mabaya Ya Fedha
Wivu na tamaa ya kuwa na nyumba kubwa, magari ya kifahari, saa za dhahabu, mavazi ya kifahari, na usafiri wa daraja la kwanza; yote hayo bila shaka yatamsababishia mtu madeni na kuathiri utoaji wa sadaka na kusababisha matatizo makubwa ya fedha (1Tim 6:6-10).
Lililo Bora Kuliko Yote- Usianguke!
Uwe mwangalifu na udanganyifu wa moyo wako mwenyewe (Yer 17:9)
Macho yako yasiondoke kwa Yesu (Ebr 12:2)
Nyenyekea mbele za Mungu, Shetani asije akakudhili (1Pet 5:5,6)
Mkaribie Mungu (Ayu 33:14)
Watu husema, “Ni kwa neema ya Mungu tu…”. Ipo neema kutoka kwa Mungu, kwahiyo hakikisha unaipokea hiyo (2Tim 2:1). Mtafute rafiki aliye mwaminifu, kisha mwongee. Mruhusu akuulize maswali saba yafuatayo:
Maswali Ya Uadilifu
Baraka Au Fadhaa?
Baada ya Shetani, adui mkubwa wa kiongozi anayefuata, ni kiongozi mwenyewe. Mfano mzuri ni Eliya. Katika Wafalme wa Kwanza mlango wa 19 alizuia mvua isinyeshe na kusababisha matatizo ya kiuchumi kwa taifa; alimfufua mtoto; aliita moto kutoka mbinguni; aliua manabii wa uongo 400; aliruhusu mvua inyeshe, na kisha akakimbia sana. Mtu wa namna gani huyu! Lakini sasa Jezebeli anapomtishia, Eliya anaishiwa nguvu kabisa na kuchoka. Hawezi kukabiliana na cho chote wala kufanya tendo lo lote la kinabii. Hana nguvu hata za kumtafuta tena Mungu kwa ajili ya neno lake.
Eliya Alishakata Tamaa
Anamwacha mtumwa wake, analikimbia tatizo, anaishia mahali pakame na kumwomba Mungu autwae uhai wake. Musa naye aliomba maombi kama hayo (Hes 11:15), na hilo linaweza kumtokea mtu ye yote. Kiongozi anapojishughulisha na masuala ya kifamilia, matatizo ya kifedha, kanisa na mipango ya baadaye, mzigo unaweza kuwa mzito sana na kumsababishia uchovu mkubwa na hata kushindwa (1Fal 19:3-5).
Majibu Ya Mungu Yalikuwa Nini?
Mungu hakukemea, badala yake alionesha huruma; alimpa chakula kizuri, kinywaji na pumziko. Mungu anamwondolea Eliya kutokuamini na kujihurumia kwake na kisha anamwongoza kwenye tukio jingine jipya (1Fal 19:5-9). Baada ya ule upepo, tetemeko na moto, Mungu anamnong’oneza Eliya na kumwambia kazi haijaisha bado. Kisha anamrejesha kwa njia aliyoijia ili kuwapaka mafuta viongozi wapya wawili na kujipatia waamini wengine 7,000! Anamtii Bwana na huduma yake inasonga mbele kwa uweza (2Fal 1&2).
Kuushinda Uchovu
Spiringi ikiwa imevutwa sana inabidi iyeyushwe na kutengenezwa upya. Halikadhalika na sisi tunapofanya kazi kupita uwezo wetu. Kuushinda uchovu sasa kunahitaji miezi kadhaa ya kutengenezwa upya.
Namna Ya Kuulinda Moyo Na Nia
Fadhaa inahusika na mioyo ambayo hugandamizwa na nguvu moja zaidi, na akili huufanya mzigo kuwa mkubwa kupita kiasi, na zisiweze kufanya maamuzi mazuri.
Paulo katika Flp 4:2-9 anasema kwamba Mungu wa amani na amani ya Mungu itawalinda mioyo yenu na nia zenu wakati ~
Mnaposhughulikia mahusiano yenye matatizo kwa unyenyekevu na toba.
Mnapoendelea kufurahi katika Bwana, kama jambo la hiari kwenu.
Mnapokuwa wapole, bila maudhi, kwa kuwa Bwana yu karibu, na tumaini lipo.
Mnapokuwa hamjisumbui kwa neno lo lote, bali ni kumwambia Mungu na kushukuru.
Mnapoamua kutafakari juu ya mambo yaliyo ya kweli, na si yaliyo tishio.
Mnapoamua kutafakari kuhusu mambo yaliyo mema na ya kupendeza, na si ya kinyume na ya giza.
Kwa kila jaribu Mungu anaahidi njia ya kutokea (1Kor 10:13). Na hii inaweza kuhusisha hata mambo ya kiutendaji ya usimamizi wa muda, fedha na madeni; na kusema, Hapana kwa baadhi ya watu, miradi na taarifa za maandishi.
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina
| Qatar | ||
|
Jina la watu |
Lugha yao |
Idadi yao |
|
Waajemi (Irani) |
Farsi, Eastern |
65,600 |
|
Wanaosema Kiurdu |
Kiurdu |
28,000 |

1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya
for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk