1985 - 2007

 

61. Kuushinda Upweke

Mavutano baina ya ndugu haitawafanya wasonge mbele

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Kutoka 18; Warumi 16

Mstari wa Kukariri
Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmojawao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! Tena wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto? Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi (Mhu 4:9-12).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Jadilianeni jinsi mlivyoona kwamba watu wawili kwa pamoja wanakamilisha kazi kubwa zaidi kuliko wawili kila mmoja peke yake.

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Andaa mashindano ya kuvutana kwa kamba kati ya makundi mawili; kati ya makanisa, shule, vilabu n.k. Jionee jinsi kila timu inavyoweza kuvuta kwa pamoja.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika taarifa ya ukurasa mmoja ukielezea ni kwanini Yesu alipeleka wale mitume wawiliwawili.

Tafakari Mistari Hii Neno Kwa Neno
Hes 11:14-17

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Korea Kaskazini. Idadi ya watu ni 26,000,000.Taifa lililotengwa, linalokaribia kuanguka. Asilimia 68% hawasadiki kama kuna Mungu; asilimia 30% wanajihusisha na mapepo wachafu. Kumewahi kuwako na uamsho, idadi ya waamini sasa ni 0.4%.

 

Moja ya matatizo ya kawaida kabisa katika uongozi na ambayo hayazungumzwi ni machungu ya upweke. Baadhi ya watumishi hawana marafiki au wenzao kwa sababu walifundishwa chuoni kwamba mtumishi ni lazima ajitenge na watu wengine wote. Kinyume kabisa na fundisho hilo Biblia inatupa mifano ya watu waliofanya kazi kwa pamoja kama timu.

Timu Za Kitume Za Paulo

Alianza na watu wawili tu, lakini baadaye akawa na timu kubwa ya kimataifa, na kule Rumi alikuwa na timu kubwa pia (Mdo 13:1-4; 20:4; 16:1-10) (Rum 16:10-16).

Ni Mtume Au Ni Wa Kitume?

Watu walioko kwenye timu za kitume hawalazimiki kuwa mitume, lakini wanahitajika kuwa na mwelekeo wa kitume; wakiwa wameitwa na kuandaliwa na Mungu kwa ajili ya mkakati wa kitume. Kwa Paulo hii ilikuwa na maana ya kusafiri, lakini kwa timu iliyokuwa Antiokia ilikuwa na maana ya kusambaza huduma katika mji wote.

 

Katika timu za Paulo tunakuta watu wa nyanja mbalimbali kuanzia watumishi wenye uzoefu mkubwa kama vile Barnaba na Sila, mpaka vijana kama Timotheo, Yohana Marko, Dk Luka, na wanamaombezi kama Epafra (Kol 4:12), Tikiko mhudumu mwaminifu (Efe 6:21), Zena yule mwanasheria na Apolo yule mhubiri mkimbizi (Tit 3:13). Timu zilibadilika kufuatana na jinsi watu walivyozijua hatima zao wito wao na kuwajibika. Wengine walipelekwa mbali na wengine walijiunga. Si kila mtu alikuwa anahudumu kwa mara ya kwanza! (Mdo 15:38) (2Tim 4:11).

Kanuni Za Timu

Mungu mwenyewe ni mfano mzuri kuliko yote wa timu kwa sababu ingawa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu wana majukumu tofauti lakini wanatenda kazi kwa maelewano na umoja mkamilifu ili kutimiza yale waliyokubaliana tangu awali (Mwa 1:26; 3:22; 11:7) (Isa 6:8) (Mt 3:16,17).

Yesu Aliunda Timu

Aliunda timu yake baada ya usiku wa maombi akiwasiliana na Baba yake, na kisha aliwaita na kuwapa mamlaka na karama, (Lk 6:12-15) (Mt 10:1).

Aliwafahamu kwa majina, akawafanya wanafunzi, na baadaye aliwatuma wawiliwawili (Mt 10:2,5) (Lk 10:1).

Wakati kanisa lilipoanzishwa siku ya Pentekoste wale mitume walijikuta wakifanya kazi kwa pamoja kama timu.

Kanuni Ya Mwanzo

Unaweza kuona manufaa ya kufanya kazi kwa ushirikiano katika ujenzi wa mnara wa Babeli ambao ulimfanya Mungu aingilie kati (Mwa 11:1-9). Ingawa watu hawa walikuwa wanafanya kazi isiyokuwa na kibali cha Mungu, hebu angalia uwezo wa umoja wao na katika kuzungumza lugha moja. Hii ina maana kwamba hakuna kitu ambacho kingeshindikana kwao (Mwa 11:1-6) (Zab 133).

Kanuni Ya Mhubiri

Hekima ya Sulemani inasema kwamba wawili ni bora kuliko mmoja, na kamba ya nyuzi tatu haikatiki kirahisi (Mhu 4:9-12). Zamani za kale mtu mmoja aling’amua kuwa anapowafunga farasi wawili kwa pamoja wana uwezo wa kuvuta mzigo mkubwa zaidi kuliko farasi hao wakivuta mizigo kila mmoja peke yake. Leo hii limekuwa ni jambo lilo dhahiri kwamba wawili wanaofanya kazi kwa pamoja hukamilisha kazi kubwa zaidi kuliko wawili wanaofanya kazi kila mmoja peke yake - na hii inaitwa sinaji. Wawili pamoja na Yesu wanakuwa ile kamba ya nyuzi tatu isiyokatika kirahisi.

 

Timu iliyo bora inahitaji maono ya ‘kamba ya nyuzi tatu’, au huduma ya kinabii na ya kichungaji ili kuwatunza watu wote walioko kwenye maono na uwezo wa kiutawala wa kushughulikia uongozi kama maono yanavyodai.

Kuchagua Timu Yako

Kanuni hii ilikuja wakati Musa alipokuwa na tatizo, ambalo ni la kawaida kwa viongozi, la kufanya kazi nyingi kupita uwezo wake; na alikuwa anaelekea kuchoka mpaka baba-mkwe wake Yethro alipompa ushauri mzuri.

Yethro alisema kwamba majukumu ya Musa kama kiongozi yalikuwa ni ~

 

Kuwawakilisha wale watu mbele za Mungu.

Kuwafundisha wale watu.

Kuwa mfano kwa wale watu (Kut 18:13-20)

Musa aliambiwa achague watu wenye uwezo, watu wacha Mungu, wanaoaminika, waaminifu ili afanye nao kazi kama timu, akiwagawia kazi zake wazifanye. Manufaa yake ni kwamba sasa Musa angeweza kufanya kazi kwa wepesi zaidi na watu wangekuwa na amani (Kut 18:21-26).

Musa, kama walivyokuwa baadhi ya mitume, hakuweza sikuzote kujifunza upesi, na matokeo yake ni kwamba baadaye anaendelea kufanya kazi peke yake na anakuwa amechoka kiasi kwamba anaomba afe.

Kwa mara nyingine Mungu anasema unda timu ya watu unaowafahamu na kupendezwa nao, na ambao wako tayari kusimama pamoja nawe (Hes 11:13-18).

Chagua Watu Watiifu Kwako

Kwa sababu Mungu huichukua roho ya kiongozi na kuiweka juu ya timu, ili kila mmoja aangalie kutenda sawasawa na maono ya huyo kiongozi na namna yake ya utendaji; la sivyo kutatokea mgawanyiko na matokeo yake ni maono mawili! Watu waaminifu wanakuwepo kwa ajili yako, na wala si kwa sababu zao wenyewe. Yesu alikuwa na wanafunzi watatu ambao alijua wangemwunga mkono kikamilifu. Eliya alimsikia Elisha akisema, “Sitakuacha”, na pale Hebroni Daudi aliwatafuta watu waaminifu na kuwauliza maswali matatu,

Je, mmekuja kwa amani,

Je, mmekuja kunisaidia,

Je, mmekuja kuungana nami au kunisaliti? (1Nya 12:17,18).

Maendeleo Ya Timu

Maisha ya timu huanza kwa kila mmoja kumtegemea kiongozi na maono yake. Baadaye wanaendelea kutegemeana wenyewe kwa wenyewe na kiongozi wao, lakini hatari inakuja ikiwa kiburi kitaingia na kumfanya mmojawapo kujiona kwamba sasa anaweza kujitegemea. Kuondoka mapema kwa mtu huyo kutaidhoofisha timu, yeye mwenyewe na hatima yake.

Makanisa mama ambayo ni vituo vya kitume vinavyopeleka huduma za kitume mjini na kwa mataifa ni njia ya Agano Jipya ya kueneza injili. Je, tunaweza kuboresha utaratibu huo?

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Saudi Arabia

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Fayfa

Mahri, Fayfi

20,000

Indonesian

Indonesian

37,000

Kabardian

Kabardian

17,000




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk