1985 - 2007

 

62. Kuutunza Muda Wako

Muda uliopotea umepotea milele

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Mhubiri 3

Mstari wa Kukariri
Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana; usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi (Yn 9:4).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Uwe mwaminifu kwa wenzio. Je, unasimamiaje muda wako na Yesu, na familia, na mwajiri wako, na katika mapumziko? Ni nani anayepata muda mwingi zaidi?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Fanya jitihada za kuandaa muda mzuri wa kukaa na familia yako, au wazazi kama uliwasahau. Fanya jambo maalum kwa pamoja, si lazima lihusishe matumizi ya fedha, lakini ni matumizi ya muda kufurahiana.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika kwa uaminifu kumbukumbu za kila siku kwa wiki nzima namna unavyotumia muda wako kila baada ya nusu saa, ikiwa ni kwa ajili ya Mungu, familia, kazi, mapumziko, mambo mengine, au kama umepotea bure.
Fanya tathmini na kupendekeza mabadiliko.

Tafakari Mistari Hii Neno Kwa Neno
Gal 6:9,10

Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Yemen. Idadi ya watu ni 16,000,000. (Waarabu). Asilimia 99.9% ni Waislamu.

Kuna wakati Yemen ilikuwa na Wakristo wengi

 

Muda ni kitu cha kipekee. Nyumba yako ikiungua unaweza kujenga nyingine. Ukikosa fedha benki unaweza kutafuta zingine. Mnyama wako akifa unaweza kununua mwingine.

Ukipoteza Muda, Huo Umepotea Moja Kwa Moja

Sulemani aliandika kwamba kuna muda kwa ajili ya kila jambo linalofanywa na mwanadamu na akasema pia kwamba mtu mwenye hekima hujua wakati sahihi na namna ya kushughulikia kila jambo (Mhu 8:5).

Ni Nani Walio Washindi Maishani?

Mbio si kwa wale walio wepesi, au vita kwa walio na nguvu; wala chakula hakiji kwa wenye hekima, au utajiri kwa wenye akili; wala hisani haiji kwa wasomi; lakini muda na fursa huwatokea wote pia (Mhu 9:11).

Kipaji Cha Muda

Mungu humpa kila mtu kwa usawa masaa 24 kila siku. Mshindi wa mbio za maisha si yule aliye mwepesi, au aliye na hekima bali ni yule anayeutumia muda wake vizuri.

Komboa, Ununue Tena Muda Wako

Ukomboe muda,

Kwa sababu zama hizi ni za uovu.

(Efe 5:16).

 

Ili kumaliza mbio hatupaswi kupoteza muda wa thamani wala kubanwa na shughuli nyingi na kutufanya watu wa kuendeshwa. Waamini wanapaswa kuwa wataratibu, waishi maisha ya kumtukuza Mungu na kuwa katika mazingira ya kipekee ya amani na umilele hata wanapokuwa wametingwa na shughuli nyingi.

Natumaini Huyu Siye Wewe

Kwa kawaida mtu anayeendeshwa ana chumba kisicho na mpangilio, gari chafu, hajiheshimu, anaogopa kugundulika, anasahau ahadi, hutoa ahadi ya huduma moja kwa watu wawili kwa wakati mmoja, harudishi majibu, hafanikishi mambo kufikia tarehe ya mwisho, anavunja ahadi, hujisikia vibaya kuhusu kazi zake, muda wake wa karibu sana na Mungu ni mdogo, uhusiano wake na wenzake si mzuri, analala vibaya na msongo.

Ni Nani Anayeuhitaji Muda Wako?

Mungu anauhitaji muda wako na familia yako pia, wewe mwenyewe na mwajiri wako pia, ingawa si lazima kwa mtiririko huo.

Muda Wa Thamani Kwa Mungu Una Maana Ya

Ukimya na kujitenga.

Kumsikiliza Mungu.

Kutafakari.

Hali hii inaruhusu umilele kuingia moyoni mwako na kukuepusha na kuendeshwa.

 

Muda Wa Thamani Kwa Familia Yako Una Maana Ya

Wakati wa waume, wake na watoto kufurahiana.

Wakati mzuri wa kumheshimu baba na mama bila kujali umri wako (Mt 15:4).

Kwa namna hii upendo utaingia maishani mwako na kukuepusha na kuendeshwa.

 

Mapumziko Na Burdani Yenye Thamani Ina Maana Ya

Ile kanuni ya 1 kati ya 7 iliyoko katika Kut 34:21.

Kanuni ya kujitenga faragha pamoja au kusambaratika, iliyoko katika Marko 6:31.

Je, siku za mapumziko yako ni takatifu?

Ukifanya mambo haya amani itaingia maishani mwako na kukuepusha na kuendeshwa.

 

Matumizi Bora Ya Muda Kazini Ina Maana Ya

 

Namna Ya Kuifanya Kazi Iwe Nyepesi Zaidi

Shughulikia Nyaraka Vizuri

Zigawe nyaraka zinazoingia katika mafungu manne:

Za kushughulikiwa sasa.

Taarifa kwa utekelezaji wa baadaye.

Taarifa za nyuma kwa ajili ya kusoma.

Takataka – tupa kwenye chombo cha taka.

Shughulikia faili 1 sasa, mengine utayaona baadaye utakapopata muda zaidi.

 

Kumbuka kwamba kutunza nyaraka kwenye mafaili ni ili uweze kuzipata tena baadaye unapozihitaji, kwa hiyo faili linapokuwa na unene wa sm 3, ligawe.

 

Washughulikie Watu Wa Thamani Kwa Ustahimilivu

Wakati mwingine makaratasi yanatushughulisha na kutuchanganya kiasi kwamba tunatoa huduma ya daraja la pili kwa watu ambao ndio sababu ya kuwepo kwetu mahali pa kazi. Hata kabla hujazungumza kumbuka kwamba lugha ya mwili wako huzungumza kwa sauti kubwa zaidi kuliko maneno ya kinywa, na sauti yako inaeleza hisia zako hata kabla hujasema lo lote. Hapa kuna njia sita za kukomboa wakati mahali pa kazi kwa kupokea watu vizuri.

 

Wasalimie tu. Endelea kufanya kazi.

Wapokee kwa upole. Usikae chini, dakika 15 zinaweza kupotea hivihivi.

Wasindikize kwenda kwa mtu mhusika.

Ongea nao. Wape muda wako wa thamani sana, uliowekwa kwa miadi.

Kaa nao. Kwa masuala yaliyo muhimu sana sahau shajara yako.

Agana nao ikiwa ni watu wanaokupotezea muda, na kamwe usiwasikilize.

Daftari Na Shajara

Hivi vitakusaidia kupangilia shughuli zote unazopaswa kuzifanya. Isome shajara yako kabla hujaanza kazi. Jiulize maswali yafuatayo kuhusiana na kazi unazoenda kuzifanya:

Je, ni ya Haraka na Muhimu? Ifanye. Ifanyike leo.

Je, si ya Haraka na Muhimu? Icheleweshe. Ishughulikie baadaye.

Je, ni ya Haraka na Si Muhimu? Kasimisha. Mwache na mwingine ajifunze.

Je, si Muhimu na Si ya Haraka? Iweke kapuni. Ina haja gani kuifanya?

Usiogope kupanga kwa wakati na Bwana, wewe mwenyewe na familia yako. Muda usiopangiliwa utapokonywa na ama watu wenye nguvu zaidi yako, au maeneo yako yenye utovu wa nidhamu na yasiyo na kiasi, au cho chote chenye sauti ya juu kuliko vyote. Kazi yenye mpangilio mzuri inakuepusha na kuendeshwa, na kukupa muda zaidi na nguvu kwa ajili ya Yesu, familia na wewe mwenyewe.

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Saudi Arabia

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Mahra (South Arabic)

Mahri

17,000

Persian (Irani)

Farsi, Western

120,000

Turk

Turkish

17,000




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk