1985 - 2007
65. Kanisa La Utumishi
Gandhi aliliongoza taifa la India kwa huduma na bila kutumia mabavu
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika
Biblia Yako Soma
1Pet 5:1-4; Eze
34:1-17
Mstari wa
Kukariri
Kwa maana Mwana wa
Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya
wengi (Mk 10:45).
Baadaye
Zungumzieni
Jambo Hili
Linganisha mifumo ya
uongozi mahali pa kazi na katika taasisi mbalimbali nchini mwako, na jinsi
inavyopaswa kuwa ndani ya Kanisa.
Jambo La
Kufanya
Kabla Hatujakutana Tena
Enenda ukaoneshe
moyo wa mtumishi wa Kristo, ukiwategemeza watu wa chini kabisa kama watoto, watu
wa mitaani, waromani, na wasioguswa. Waache jirani na Mungu.
Kazi Ya Kuandika Ya
Stashahada
Andika ukurasa mmoja
ukielezea tofauti zilizopo kati ya kanisa linaloongozwa na mchungaji, na lingine
linaloongozwa na ‘mchinjaji’.
Tafakari Mistari Hii Neno Kwa Neno
Mit 27:23-27
Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Hong Kong. Umiliki wake umerudi mikononi mwa Uchina mwaka 1997.
Ni eneo lenye nguvu kibiashara katika Asia; na lina Wachina na wahamiaji wengine wapatao 6,000,000.
Asilimia 66% ni Tao & Mabudha, asilimia 14% ni Wakristo, ni lango la kimishenari la kuingilia Uchina.
Ni Uongozi Au Ubwana?
Kiongozi
wa kanisa au umisheni ni tofauti kabisa na viongozi wengine kama wa kisiasa, wa
kijeshi, wa biashara au wa kidini. Katika ulimwengu huu mtu mmoja aliyeko juu
anadhibiti kila mtu aliyeko chini yake kwa kutumia cheo, shinikizo au hofu ya
kupoteza ajira. Yeye, au wabia wake wanapata manufaa makubwa wakati ambapo
wafanyakazi wanaweza kuishi katika hali ngumu. Hatushangai kuwepo kwa mapinduzi
na migomo. Ni huzuni kwamba baadhi ya makanisa nayo yanatawaliwa kwa mfumo huo.
Hali hiyo inasababisha kutokuridhika.
Ni Wachungaji Au Wachinjaji?
Mzee mmoja wa busara aliwahi kusema, "Ni watu wa aina mbili tu wanaojishughulisha na kondoo – wachungaji na wachinjaji!
Ni Yupi Mtu Huyu?
Anapenda kuwa wa kwanza.
Anawakwepa watumishi wa kweli wa Mungu. Anawasemea wengine maneno maovu na ya
chuki. Huwadhibiti watu kanisani, akionesha ubwana wake, ambayo ni namna ya
uchawi. Yeye ni Diotrefe, (3Yoh 3-10). Wapo pia wachungaji waovu kwelikweli
katika Eze 34:1-6 na Zek 11:15-17.
Utawajuaje Wale Wabaya?
Katika
mabenki watumishi hujifunza kuzitambua noti bandia kwa kuendelea kushughulika na
noti halali. Noti bandia inapowafikia wanaitambua mara moja. Sisi nasi tutaweza
kujiepusha na udanganyifu wa viongozi wabaya kwa kujihusisha na viongozi wema.
Yesu,
Mchungaji Mwema
Yesu, Simba jasiri
wa kabila la Yuda yeye pia ni Kondoo wa Mungu aliye mpole. Kiongozi wa leo
anaweza akanguruma kama simba dhidi ya dhambi, na wakati huohuo akawa
mnyenyekevu na mpole kwa watu kama mwanakondoo.
Njia Ya
Mwokozi
Wanadamu kwa kawaida
hutawala kwa njia ya uwezo wa jeshi, siasa, fedha au dini; lakini Yesu alichagua
namna nyingine kabisa ya uwezo, ambao wengi hawaujui na mara nyingi
unadharaulika. Uweza wa ajabu wa unyenyekevu, na huduma ya kujitoa kuwa sadaka.
Katika Mk
8:31, Yesu anatangaza mpango wake mzuri sana wa kuwapata watu wa ulimwengu, kwa
kukubali usumbufu; kwa kustahimili dhihaka, fedheha na mateso bila ubishi, na
kwa kukubali kukataliwa, kusalitiwa na hata mauti bila malalamiko (Flp 2:6-11)
(Yn 12:32). Yesu anazungumza habari ya kufufuka, wanafunzi wake hawaelewi lakini
Shetani anaelewa na mara anapinga mpango huo kupitia kwa Petro (Mk 8:32,33).
Yesu Ameweka Kiwango
Katika Mk
8:34,35, Yesu anasema kumfuata kuna maana ya mtu kujikana mwenyewe, kukubali
mateso ya msalaba na kupoteza maisha kwa ajili ya Bwana. Thawabu ya upotevu kama
huo kwa ajili ya Yesu na injili ni uzima halisi!
Je, Naweza Kuwa Huyo Kiongozi?
Katika Mk 9:31-39 Yesu anarudia tena mkakati wake wa unyenyekevu na huduma ya kujitoa. La kushangaza ni kwamba wale wafuasi wake walilipokea hilo kwa kuanza kubishana wao kwa wao kuhusu safu ya uongozi miongoni mwao na ni nani atakayekuwa kiongozi wao. Yesu akajibu na kusema kwamba ili uwe wa kwanza ni lazima ujiweke kwenye nafasi ya mwisho na kuwa mtumishi wa wote, hata na watoto na watu wengine walio tofauti.
Je, Naweza Bwana?
Katika Mk 10:32-45, Yesu
anaelezea kwa mara ya tatu mkakati wake wa unyenyekevu, na huduma ya kujitoa, na
safari hii Yakobo na Yohana wanawania cheo na uweza wa ubwana badala ya huduma.
Yesu anajibu na kusema kwamba ni viongozi wa Mataifa pekee ndio wanaowatawala
watu, na kwamba haipasi kuwa hivyo miongoni mwa wafuasi wake; hata Mwana wa
Mungu hakuja kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake.
Njia Pekee Ya Kwenda Juu Ni Kushuka
Yesu
alishuka hadi kwenye mauti na akafufuka. Mkakati wake ulifanya kazi na leo
anaongoza mamilioni ya wafuasi wa rangi zote na tamaduni zote, wanaomtii,
wanaompenda na kumshukuru. Yesu, akiwa Simba mkamilifu na Mwanakondoo mkamilifu,
alitupa sisi mfano mmoja pekee wa uongozi, unyenyekevu na huduma ya kujitoa.
Bila kujali wasifu na utamaduni wa kiongozi, atakuwa amefanya vema kunyenyekea,
na kuhudumu kwa kujitoa kama alivyofanya Kristo.
Je, Linatekelezeka?
Waraka wa kwanza wa Paulo kwa Wathesalonike mlango wa pili, mistari 13 ya kwanza, unaonesha ushuhuda wa uongozi wa kihuduma ukitenda kazi. Paulo alivumilia mateso na matusi, na hakuwa na nia mbaya wala hila. Aliishi kwa kumpendeza Mungu na si wanadamu, hakumfurahisha ye yote na hakuwa na tamaa ya fedha na wala hakuwa mzigo kwa mtu ye yote; lakini alikuwa mpole na mwenye kujali, na kwa kweli akiwa na shauku ya kuishi na wale watu. Alionekana kuwa mtakatifu, asiye na lawama na mwenye haki. Sasa ni nani asiyempenda mtumishi kama huyo?
Na la
kufurahisha ni kwamba hata watu wa ulimwengu huu wanatambua uzuri wa uongozi wa
kihuduma katika ulimwengu mbaya wa ubwana. Gazeti la TIME la tarehe 9 Mei, 1994
liliripoti kwamba, “Kura huko Ufaransa zinaonesha kwamba kasisi wa watu
wasiokuwa na makazi Abbé Pierre ni mtu anayeheshimika sana katika taifa hilo”.
Je, Linafanyaje Kazi Siku Hizi?
Andiko la
Efe 4:11 linatuambia kwamba Mungu amewaweka mitume, manabii, wainjilisti,
wachungaji na walimu kuliongoza kanisa, na ms 12 unatuambia kwamba jukumu lao ni
kuwaandaa watu kwa ajili ya huduma, na si kwamba waifanye hiyo huduma peke yao.
Lakini kwa vipi?
Chagua hapa > 65chart ili uweze kuona mchoro kuhusu somo hili
Umbo La Pembetatu
Katika
ulimwengu umbile la pembetatu yule mtu hukaa pale juu. Amri zinatoka juu kwenda
chini, na mali kutoka chini kwenda juu. Hata hivyo, katika Ufalme wa Mungu
pembetatu ya ulimwengu ni lazima ifanywe kinyume; watu wenye karama sana na
wenye uwezo, katika ujumla wao katika uongozi, wakae chini kwenye magoti wakiwa
wanategemeza ngazi ya uongozi inayofuata, na ngazi hiyo kutegemeza ngazi
nyingine inayofuata, mpaka watu wote wawe wametegemezwa na kuinuliwa karibu
zaidi na Mungu.
Kwanini Mitume Wakae Chini?
Mitume ni wa kwanza kanisani,
sikuzote wakiwa kwenye timu pamoja na wazee, na ni wa kwanza pia katika makanisa
ya maeneo (1Kor 12:28) (Mdo 15:2,4,6,22,24) (Mdo 13:1). Yesu alisema nini? Wa
kwanza na awe mtumwa wa wote. Na iwe hivyo.
Kwa
Kumalizia Omba kwa Ajili Ya Watu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa
Majina
Somalia |
||
Jina la Watu |
Lugha Yao |
Idadi Yao |
Shambaara (Gosha) |
Mushungulu |
84,000 |
Waswahili (Baraawe) |
Kiswahili |
40,000 |
Tunni |
Tunni |
20,000 |
1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya
for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk