1985 - 2007

 

66. Kanisa La Ushuhudiaji

Uwezo katika watu kuzungumza

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Mt 28:19; Lk 9:1-6; Lk 10:1-24

Mstari wa Kukariri
Ndipo wakaambiana, “Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; tukingoja hata kutakapopambazuka madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme” (2Fal 7:9).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Ni watu wa aina gani mtakaowatafuta ili kuunda kikundi kidogo cha kuwashirikisha yale mliyojifunza.

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Chagua watu wasiopungua watatu na wasiozidi 12 ambao watakubali kukutana nawe mara kwa mara nyumbani kwako au ukumbini. Utakuwa na fursa nzuri ya kuwafundisha yale uliyojifunza na mwalimu wako katika masomo haya. Waagize nao wakawafundishe wengine yale utakayowafundisha.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika kurasa zisizozidi mbili, hatua tatu kama zinavyoonekana katika 2Tim 2:2 na uelezee ukuaji kwa njia ya kuzidisha.

Tafakari Maandiko Haya
Lk 10:1-4, 17-21

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Uturuki. Uturuki ni daraja kati ya Ulaya na Asia. Idadi ya watu ni

62,000,000. Asilimia 99.8% ni Waislamu. Wapo Waturuki wapatao 600 ambao ni wanafunzi wa Kristo.

Hii ndio ‘Galatia’ ya kwenye Biblia inayohitaji sana maombi yako.

 

 

Katika mpira wa miguu wachezaji wapya hujifunza kutoka kwa kocha wao; ambaye pengine naye aliwahi kuwa nyota wa timu yake. Katika karakana utawakuta vijana wakijifunza kazi kutoka kwa mwalimu mtaalamu mwenye ujuzi wa kutosha. Kujifunza kutoka kwa Bwana wetu, Yesu, ndiyo hasa maana ya ufuasi, na una nguvu. Yeye ni Mwalimu, na sisi tu wanafunzi wake, yaani wanaume na wanawake ambao kwa pendo lake wanafundishwa na kuadibishwa.

 

Chagua hapa > 66chart ili upate kuona mchoro kuhusiana na somo hili

 

1. Uweza Wa Ajabu Wa Ufuasi

Mchungaji mmoja kutoka Taiwan alisafiri mara moja kila baada ya miezi miwili kwa muda wa miaka miwili kwenda katikati ya Uchina ili kuwafundisha kwa siri watu 15 yale aliyokuwa anayafahamu kumhusu Yesu na ushuhudiaji. Watu hao nao kila mmoja aliwafundisha watu wengine 12 na hao pia wakawaeleza watu wengi zaidi habari za Yesu.

Mwaka 1993 walikuwa na mwezi wa uinjilisti ambapo watu wapatao 1,500 watumishi walioandaliwa vizuri walisafiri kwa miguu, kwa baiskeli, kwa mabasi, kwa matreni, na kwenda sehemu mbalimbali za Uchina kuwashuhudia watu wengine habari za Yesu. Waliporudi na kutoa taarifa, yule mchungaji kutoka Taiwan alipiga mahesabu na kugundua kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja tu cha kuyafanyia kazi mafundisho yake zaidi ya watu 100,000 waliokoka na kubatizwa.

Hebu Turejee Kuangalia Yale Yaliyotokea ~

Hatua 1
Mtu mmoja alifundisha watu 15, kwahiyo watu 15 walikaa chini na kufundishwa.

Hatua 2
Halafu wale 15 kila mmoja alifundisha watu wengine 12 wake kwa waume. Na idadi yao sasa ikawa imefikia 195 watu waliosikia na kujifunza hilo somo.

Hatua 3
Wale watu 195 walirejea makwao na kila mmoja akafundisha watu wengine kati ya 6 na 12 na mwishowe idadi yao ikafikia 1,500; watu waliopokea mafunzo kutoka kwa mtu mmoja katika hatua ya kwanza.

Huo Ndio Uweza Wa Ufuasi Ukitenda Kazi
Kumbuka kwamba shughuli yote hiyo ilifanyikia nyumbani, chini ya mti na maeneo mengine yenye utulivu ili kuepuka bughudha za polisi na mateso. Hapakuhitajika majengo ya gharama kubwa, wala vifaa au vitabu. Ni maneno tu ya kimyakimya, kujifunza pamoja na maombi kama ilivyofanyika katika karne ya kwanza, baada ya agizo la Yesu la kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi.

2. Je, Ni Lazima Shule Ya Biblia Iwe Na Jengo?

Je, kuhudhuria Shule ya Biblia kwa mwaka mmoja au miwili ndiyo njia pekee ya kujifunza njia za Mungu? Lakini inakuwaje watu kwa maelfu wanapomjia Yesu, na wote wanataka kujua zaidi habari za Bwana na kumtumikia?

Watapata wapi fedha na muda wa kuwa mbali na familia zao, kazini na hata kanisani? Utapata wapi walimu, majengo, vitanda na vyakula? Hata kuwaleta pamoja watu 500 kwa wiki moja kunahitaji nauli 1,000 za basi, mikeka 500 ya kulalia, nafasi za choo kwa ajili ya watu 500, madaftari 500 na kalamu, na milo 10,500 pamoja na maji!

3. Je, Hakuna Njia Nyingine?

Marabi nao walikuwa na shule lakini Yesu alichagua njia tofauti kabisa. Ni njia iliyo rahisi kupanga, sio ya gharama kubwa, na ipo nafasi kwa kila mmoja kuhudhuria.

Je,Yesu Aliwaandaaje Wafusi Wake?
Yesu alitumia muda wake mrefu kuandaa vikundi vidogovidogo vya watu 3, 12 na 72. Walikuwa marafiki. Aliwafundisha wakiwa faragha, na mengine walijifunza katika mikutano ya hadhara. Walipelekwa ili kujaribu kufanyia kazi kila walilojifunza. Na waliporejea walimwambia Yesu mambo yote (Mt 10:1) (Lk 9:1-10; 10:1-24).

Unatahadharishwa na mapema
Ufuasi huachilia neno la Mungu na Roho wake na hili husababisha jambo jema sana na ovu sana ndani yako. Ufuasi husababisha hasara ya kidunia lakini ukuu wa ndani, faida ya milele. Wakati fulani wafuasi walisafiri kwa kukatiza ziwani, ndipo walipopigwa na dhoruba. Walikuwa katikati ya mapenzi ya Mungu, lakini hata hivyo walitota kwa maji na hofu iliwapata pia! (Mt 8:23-27).

4. Paulo Alikuwa Na Wanafunzi Pia

Wakati akiwa kwenye safari zake Paulo aliondoka na timu ya watu ambao walijifunza kwa kuona na kuiga yale aliyoyafanya (Mdo 20:4,5). Wakati Paulo akiwa Efeso, ambayo ni Izmir iliyoko katika Uturuki ya leo, alikutana na waamini ambao walikuwa hawajasikia hata habari za Roho Mtakatifu. Kwahiyo Paulo akawafundisha, akawaombea na akaendelea kukutana nao kila siku kwa zaidi ya miaka miwili. Walikaa miguuni pa mzee Paulo na kujifunza kama wanafunzi.

Unafikiri Kulitokea Nini?
Kulikuwepo na uinjilisti wa dhati kwa sababu katika kipindi cha miaka miwili jimbo lote walisikia neno la Mungu.

Kulikuwa na miujiza mikubwa,

Mji ulijawa na hofu ya Mungu.

Watu walichoma vitabu vyao vya uchawi.

Neno la Mungu lilienea na kukua katika uweza.

Wale waamini waliokuwa wajinga hapo awali, wamekuwa wazee wa makanisa ya Efeso (Mdo 19:1-21; 20:17,18).

5. Je, Ni Kuongezwa Au Ni Kuzidishwa?

Kwa kawaida makanisa hukua kwa kuongezeka mtu mmoja au wawili au zaidi wanapokuja kuisikia injili. Lakini ukuaji kwa kuzidishwa huwa hivi; wengi husikia ujumbe wa Biblia, na kuupokea upendo wa Mungu, na kanisa la nyumbani huanza pale wanapoishi.

Hili linaweza kutokea kijijini kwako kwa kuachilia uweza wa ufuasi. Maana yake unatakiwa kukumbuka au kuandika yale yote uliyofundishwa na kuandaa utaratibu wa kufundisha kikundi cha rafiki zako, ambao nao watakwenda kuwafundisha wengine. Paulo alimpa kijana Timotheo, mwanafunzi wake, hatua tatu:

  1. Mambo yale uliyoyasikia kwangu . .
  2. Hayo uwakabidhi watu waaminifu . .
  3. Watakaofaa kuwafundisha na wengine.

Chagua wanafunzi wako. Kutana nao, pengine nyumbani kwako ili kuwaambia yale uliyojifunza katika somo hili na kuwaambia kitu watakachoweza kujifunza kama watarudi tena. Kisha wapange hao rafiki zako ili nao waweze kuwafikia wengine kwa neno la Mungu (2Tim 2:2) (2Fal 7:9). 

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Sudan

Jina la Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Sungor (Assagori)

Sungor

15,000

Tulishi

Tulishi

10,000




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk