1985 - 2007

 

67. Kanisa Mama

Kuleta nafsi moja kwa Yesu ni vizuri, kupanda kanisa jipya ni vizuri zaidi

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Mdo 20:17-37; Mk 1:9-45

Mstari wa Kukariri
…yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye…Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga… (Ufu 3:7,8).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Ni wapi unapopafahamu ambapo hapana kanisa la kiinjili. Huenda ikawa ni mahali au pengine ni kikundi cha watu wanaoishi jirani na wewe. Je, unadhani ungeweza kufanya kitu fulani?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Nenda katafute watu jirani jirani na mahali unapoishi, pengine ni watu kutoka nchi nyingine iliyo tajiri zaidi au maskini zaidi kuliko yako, ambao hawana kanisa. Waulize kama watapenda kuanzishiwa kanisa ili wapate mahali pa kuabudia na kupatia msaada wa kiroho na mahitaji ya kijamii.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika uchambuzi usiozidi kurasa mbili kuhusu watu waliopo wilayani kwako ambao hawana kanisa.

Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Mt 16:18

Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Laos. Idadi ya watu ni 5,000,000. Ni watu maskini. Asilimia

2% ni Wakristo; wengi ni Mabudha. Kanisa liliteseka chini ya Ukomunisti.

 

Kuipata nafsi moja ni jambo la kufurahisha sana, lakini haitoshi ukilinganisha na ongezeko kubwa la watu. Kuanzisha makanisa mapya na kuyaunganisha pamoja katika mtandao wa kitume ni jambo bora zaidi.

Lakini Baadhi Ya Watu Wana Haya Ya Kusema ~

"Sisi hatuhitaji makanisa zaidi"

"Kanisa moja kubwa ni bora zaidi"

"Ni vema kuyategemeza makanisa yaliyopo sasa"

"Acha tu watu waje kwenye mikutano yetu"

Kama unavyoona hakuna sababu yo yote ya Kibiblia iliyotolewa. Sababu zilizotolewa zina namna ya ubinafsi na kujiangalia wenyewe, na hilo halimpendezi Bwana, na watu hawa hawataweza kuwa na kanisa la kuvutia, lenye makusudi ambayo watu watataka kuwa sehemu yake.

Ya Nini Kuanzisha Makanisa Mapya?

Je, Ni Kutimiza Hitaji La Jamii?
Hapana, huo unaweza kuwa ni mwitikio wa kimsisimko kwa ukweli kwamba inaonekana kama vile watu wana hitaji kubwa la kiroho na kimaadili kila mwaka unaopita. Lakini ukweli wenyewe ni kwamba Mungu hakutani na hitaji moja kwa moja la sivyo ulimwengu ungekuwa ni mahali pa tofauti kabisa.

Anakutana Na Imani

Ikiwa kweli uhitaji na mateso huleta uamsho, basi bara la Ulaya lilipaswa kuwa limepiga hatua kubwa sana kiroho kuliko bara lingine hapa duniani baada ya karne moja ya vita kali. Lakini kwa kweli ni bara lililoko kwenye giza kubwa kuliko bara lingine lo lote, na halipendi injili. Kupanda makanisa ni kuenea kwa uinjilisti ambao ni sehemu ya Agizo Kuu la Kristo.

Mkakati wa kuwa na makanisa mapya katika eneo ni maono yanayotoa nafasi kwa karama za watu wote wa Mungu, vijana kwa wazee, badala ya kuwategemea tu wainjilisti wageni. Kila mmoja anaweza kufanya kitu fulani na akasaidia kufikiwa watu wa rika lake kwa ajili ya Yesu. Wanapenda kufanya hivyo!

Utaratibu wa kuanzisha makanisa unaleta afya kwa sababu kanisa linaloishi kwa ajili ya watu walioko nje lina muda mchache sana wa malumbano ya ndani. Na ya nini kusubiri? Nimesikia habari za kanisa lenye watu 17 tu na ambalo lina malengo ya kuanzisha makanisa mengine matatu katika mji wao.

Je, Makanisa Mapya Si Migawanyiko Ya Siri?

Ni wazi kwamba wapo watu walalamishi na waasi ambao wanapenda ukubwa na kukaa mbele, na hao hawawezi kamwe kuanzisha kanisa lenye afya njema. Kwa kweli watakachofanya ni kuambukiza tabia yao ya kutokuridhika, na pengine kutokuelewana na wenzao na hatimaye kusababisha hilo ‘kanisa’ jipya kusambaratika. Hao wanapaswa kutubu na kujirekebisha kwa msaada wa Bwana.

Je, Pendekezo La Kusambaa Linaweza Likawa Potofu Wakati Wote?

Ni nani aliyelitawanya kanisa la Yerusalemu ambalo halikutii Agizo Kuu na kufanya uinjilisti?

Ni nani anayetenganisha nuru na giza?

Ni nani aliyelitenganisha kanisa la Kiprotestanti kutoka Roma?

Ni nani aliyewaondoa Wamethodisti, Wapentekoste na Wakarismatiki kutoka kwenye ‘kanisa’ hilo na kuwastawisha?

 

Jibu ni ‘Mungu Mwenyewe’!

Edward kutoka Pakistan na mkewe Kylykke kutoka Finland ni wamishenari nchini Uingereza. Hivi karibuni wameanzisha kanisa lenye waamini wapya wenye asili ya Kiasia na watu wengine kutoka makanisa mengine. Je, huo ni mgawanyiko? Hapana. Kwa sababu watumishi tisa kutoka kwenye makanisa mengine walihudhuria sherehe za uzinduzi na kutoa baraka zao na kuwaunga mkono. Huo ulikuwa ni mwanzo mzuri.

Mungu Anatuagiza Kuanzisha Makanisa

Kanisa ni makusudi ya Baba, (Efe 3:10)

Kanisa ni ahadi ya Mwana, (Mt 16:18)

Kanisa lilikuwa ni matokeo ya ujio wa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, (Mdo 2:42-47)

Kanisa lililoanzishwa na watu wa kawaida na kuimarishwa na watu wenye karama ni mfano mzuri wa Antiokia, (Mdo 11:19-26)

Kuanzisha makanisa lilikuwa lengo mojawapo la Paulo, kwa mfano kule Efeso (Mdo 13:14; 19:1- 20:17)

 

Leo Mungu amefanya uanzishwaji wa makanisa kuwa agenda namba moja, kwa kuvuvia na kubariki mashirika ya kimataifa yaliyofanikiwa, DAWN & SEAN, yanayojishughulisha na uanzishwaji wa makanisa.

Makanisa Mapya Yanaanzishwaje?

Hapa pana viambato vya kiroho kutoka kwa mfano wa Yesu mwenyewe. Matokeo yake kama yanavyoonekana kwenye Mk 1:45 ni kwamba watu ‘waliendelea kuja’ wakiletwa na hatua hizi muhimu na bora kwa uanzishwaji wa makanisa ~

Kumkaribisha Roho Mtakatifu, na kukubali kuongozwa naye (Mk 1:9-12).

Ulazima wa kumshinda Shetani (ms 13).

Kutenda kwa kuzingatia wakati mwafaka, (Mk 1:14a,15).

Kuhubiri kunapewa umuhimu wa kwanza (ms 14).

Kuna mafanikio makubwa zaidi tunapotenda kama timu (ms 16-20).

Matumizi mazuri ya karama za kiroho, (Mk 1:23-42).

Kujitoa kwa ajili ya maombi ya dhati (ms 35).

Roho ya utangulizi inayokataa starehe (Mk 1:37-39).

Upendo kwa watu ni jambo muhimu sana, (Mk 1:23,30,40).

Kiutendaji, Unafanyaje?

Kanisa kubwa linaweza kupeleka watu 50 kwenda kuabudu na kueneza injili katika eneo jipya, wakiendelea kusaidia ili kuhakikisha kwamba huyo mtoto mchanga anakua. Waweza pia kuanzisha kanisa kwa ‘lugha’ maalum katika eneo lako kwa watu kama wahamiaji au wakimbizi. Huduma zenye wepesi wa kutafuta ni njema katika kueneza injili miongoni mwa watu wa kidunia kwa njia zisizo za kikanisa kama muziki mzuri na maigizo siku za Jumapili; waamini wanaweza kukusanyika siku nyingine katikati ya wiki.

Vipo vitabu vingi vya kukuongoza na kukutia moyo, lakini sikuzote ikumbuke theolojia ya Maria. Yeye alisema hivi, “Fanyeni lo lote atakalowaambia”. Soma pia Ufu 3:7,8.

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Syria

Jina la watu

Lugha yao

Idadi yao

Circassian

Adyghe

25,000

Dom Gypsy (Nawar, Kurbat, Barake)

Domari

10,000

Kurd, Western

Kermanji (Kurmanji)

667,800




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk