1985 - 2007

 

69. Kanisa Lililo Hai

Je, Kanisa Ni Jengo Au Ni Watu?

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
1Kor 12 hadi 14

Mstari Wa Kukariri
 “…nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Mt 16:18,19).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Baadaye utakapokwenda kanisani unafuata nini hasa, unatazamia nini?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Baadaye utakapokwenda kanisani hakikisha unamtafuta Mungu ili akupe zawadi ya kumpelekea mtu mwingine atakayekuwa humo kanisani, na hakikisha wameipokea kabla hujarejea nyumbani.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika ukurasa mmoja na kwa heshima utoe mawazo yako kuhusu mabadiliko yanayoweza kuleta maendeleo katika maisha ya kanisa.

Tafakari Mistari hii Neno Kwa Neno
2Tim 1:6,7

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Omba Kwa Ajili Ya Wahindi Wenye Asili Ya Marekani. Idadi yao ni 2,000,000 na makabila 266.

Tatizo lao kubwa ni umaskini, magonjwa na kukosa ajira. Kuna idadi ndogo lakini inayokua ya watu wanaompokea Yesu.

 

1. Kwanini Nini Unakwenda Kanisani?

Baadhi ya watu huenda kanisani kwa sababu wanaona kama ni wajibu wao kufanya hivyo au kwa sababu ni siku ya Jumapili asubuhi. Kwa baadhi ni mahali pazuri pa kupatia taarifa za biashara au wanajisikia furaha kuwepo kanisani. Wengine wanakwenda kanisani kwa sababu tu marafiki zao nao wanakwenda kwa hiyo ni mahali pa kukutanikia. Watu huenda kanisani kupata burudani siku za Jumapili au kupata ufahamu wa mambo fulanifulani, au kuwasikiliza wahubiri maarufu. Wengine wanakwenda kanisani ili kuwaridhisha waume/wake zao; wengine wanakwenda kutafuta wachumba; na wengine wanakwenda ili kuwakimbia wake/waume zao. Matumaini ni kwamba wengine huenda ili wapate kujifunza Biblia.

2. Kanisa Ni Nini?

Iwe ni kanisa la ulimwengu mzima ambalo ni jumla ya mamilioni ya waamini au ni kanisa la eneo moja, kanisa sikuzote ni watu na kamwe si jengo. Sisi ndilo Kanisa, ‘Nyumba ya Bwana’.

Jamii Mpya

Kanisa ni jamii mbadala ambayo kuweko kwake kunawezeshwa na Roho Mtakatifu kwa njia zisizo za kawaida. Ni jamii iliyounganishwa na imani, ambapo wanajamii hubebeana mizigo yao, na wanaishi maisha yenye nidhamu na ushirika wa karibu, uwajibikaji na matendo.

 

Watu Wanaomwelekea Mungu

Kanisa lina maana ya furaha, maombi na ibada katika kumwadhimisha Baba yetu wa Mbinguni kwa wema wake wa kila siku. Neema zaidi inapokelewa kupitia ubatizo, Sakramenti ya Meza ya Bwana, na uwepo wa Mungu.

 

Hatima Yao Ni Ushindi

Yesu aliahidi kulijenga kanisa lake na kwamba milango ya kuzimu haitalishinda hata kanisa linaposonga mbele kinyume nayo (Mt 16:18).

 

Tafakari kuhusu picha hizi pia kutoka kwenye Biblia. Kanisa ni familia ya Mungu; ni jengo ambalo Yesu ndiye Mjenzi na Jiwe la Pembeni; ni mwili ulio hai na Yesu ndiye Kichwa cha mwili huo; ni kundi na Yesu ndiye Mchungaji; ni bibi arusi na Yesu ni Bwana arusi; ni sanduku la thamani kubwa lenye kuhifadhi vito vya thamani; ni matawi ya Mzabibu; ni hekalu ambalo Yesu ndiye Kuhani Mkuu; ni jeshi na nyumba ya sala.

 

Unataka Kujua Zaidi?

Tumia itifaki yako ili kupata mistari ya Biblia inayohusiana na kanisa kama ilivyotajwa hapo juu.

3. Ni Nini Kinachotokea Kanisani?

Tunakutana Na Yesu

Yesu yupo wanapokutanika wawili au watatu kwa jina lake, akitoa msamaha, kukubalika na uzima wa milele (Mt 18:20).

 

Tunamsikia Yesu

Kupitia Neno lake na Roho wake.

 

Tunaponywa Na Yesu

Yesu, ni yeye yule jana, na leo na hata milele, bado ni mponyaji wetu.

 

Tunamwabu Mungu Kwa Pamoja

Mungu anakaa katika sifa za watu wake.

 

Tunaimarishana

Paulo anafundisha katika 1Kor 14:26 kwamba kanisa linapokusanyika, kila mmoja na aje na karama kutoka kwa Mungu kwa ajili ya mtu mwingine. Paulo anazitaja karama tano hapa, lakini zipo nyingi zaidi ya hizo kwa ajili ya mahitaji ya watu kanisani.

4. Hebu Na Tuzifungue Karama Za Mungu

Katika 1Kor 12-14 Biblia inatoa maelezo kuhusu karama za Mungu na kuonesha namna ya kuzitumia kwa usahihi (1Kor 12:4).

Karama Za Mawasiliano

Ndimi, hukuwezesha kunena kwa lugha ambazo hukuwahi kujifunza.

Tafsiri, kujua kile kilichonenwa.

Unabii, sikuzote ni lazima unabii upokelewe, upitiwe na kujaribiwa.

 

Karama Za Ufunuo

Maneno ya maarifa, kutoka kwenye hazina ya Mungu ya habari.

Neno la hekima, hukuwezesha kujua la kufanya.

Utambuzi wa pepo wabaya (sio wanadamu).

 

Karama Za Uweza

Imani yake, huhamisha milima.

Uponyaji ni karama ya Mungu kwa ajili ya wagonjwa.

Miujiza, kwa maana ya, matendo ya uweza.

 

Karama Za Uongozi

(Efe 4:11) (1Kor 12:27-31)

 

Karama Kwa Ajili Ya Watu Wote Wa Mungu

(Rum 12:6-8) (1Pet 4:8-11)

Kutoa unabii, sio kuwa Nabii, bali kulileta neno la Mungu ili kuwaimarisha watu, kuwafariji na kuwatia moyo (1Kor 14:3).

Kuhudumu, ina maana ya kuwasaidia wengine kwa furaha!

Kufundisha, lakini hii haina maana kwamba ni lazima uwe na karama ya Mwalimu.

Kutia moyo, kama Barnaba, (Mdo 11:23).

 

Kufadhili, kuwa tayari kushiriki baraka za Mungu na watu wengine, ni karama kuu.

Kusimamia, ni karama ya wazee.

Huruma, inakusaidia wewe kuwasaidia walio dhaifu.

Utawala, ni karama muhimu inayowezesha shughuli za kanisa kwenda kwa mpangilio mzuri.

 

Karama nyingine ni pamoja na mwanamaombezi, mzee, shemasi, mwimbaji, mwalimu wa nyimbo, mngoja mlango, na kuhani. Hatushangai basi Paulo anaposema habari ya kuchochea karama ndani mwetu (2Tim 1:6) (1Tim 4:14). Yapo mambo tofauti ya kufanya na karama hizo, na njia mbalimbali za kutendea kazi karama hiyohiyo moja, lakini Mungu anahusika katika zote. Zote hutolewa na Roho Mtakatifu kama apendavyo. Hatuwezi ama kuchagua karama zetu wenyewe, au kuzitumia au kutozitumia kama tupendavyo; na badala yake tunazitumia kwa upendo (1Kor 12:5,6; na mlango wote wa 13).

5. Je, Kuna Vyeo?

Biblia inasema kwamba mitume na manabii wanaongoza kisha wanafuatia walimu ili kutuweka kwenye mstari ulionyooka. Baada ya hapo karama zote ni muhimu, kwahiyo igundue karama Mungu aliyokupa na kuichochea kwa kuwahudumia wengine.

Filipo alianza kama mtawala lakini baadaye akawa mwinjilisti, na Paulo alianza kama mwalimu na akaishia kuwa mtume (Efe 2:20) (1Kor 12:28).

Akiwepo ndugu au dada mwenye karama zaidi yetu katika eneo fulani, basi na tumletee watu ambao sisi tumeshindwa kuwasaidia ili awahudumie. Sisi sote kwa pamoja tu timu ya Mungu, mwili mkamilifu wa Yesu katika ulimwengu huu (1Kor 12:12-27).

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Tajikistan

Jina la Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Parsee

Parsi (Parsee)

50,000

Shughni (Shugnan-Rush)

Shugni

35,000

Tatar

Tatar

75,000

Turkmen (Turkoman)

Turkmen

14,000

 




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk