1985 - 2007

 

70. Kanisa Linaloongozwa Na Roho

Kufanya urafiki na Roho Mtakatifu

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Yn 14:15-26; 15:26 - 16:15

Mstari wa Kukariri
Neema ya Bwana Yesu Kristo, na upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote (2Kor 13:13).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Wakati unapokuwa ukishuhudia, au kumwombea mgonjwa, je, unaona tofauti yo yote sasa unapojua kwamba kwa kweli huduma hiyo huifanyi ukiwa peke yako?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Anza kutafuta uhusiano mzuri na Roho Mtakatifu kwa namna ileile ambayo ungeweza kuhusiana na rafiki mpenzi. Hatupaswi kumwomba hasa lakini tunatakiwa kuzungumza naye na kumshirikisha maisha yetu. Usishangae basi ikiwa atanena nawe kama alivyofanya katika Mdo 13:2 na Mdo 16:6-10.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Biblia inazungumza habari za Roho Mtakatifu kwa kutumia picha na majina kama hua, maji, mafuta, mfariji, au uvuvio. Tafuta majina mengine unayoweza kuorodhesha, angalau yafikie kumi.

Tafakari Andiko Hili
Mdo 16:6-10

Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Cuba. Idadi ya watu ni 10,000,000. Kuna ukandamizaji, mgawo wa chakula na uhaba. Kumekuwepo pia na mateso kwa waamini ambao ni asilimia 3% tu. Watu wengi wanaabudu pepo wachafu.

 

Je, Unakifahamu Unachokiomba?

Tuna kawaida kila mwisho wa ibada ya pamoja kubarikiana kila mmoja na mwenzake kwa mistari ya Biblia tuliyoikariri, lakini je, uliwahi kujiuliza ni nini hasa tunachotakiana?

Ushirika Wa Roho Mtakatifu

Neno ushirika ni koinoñia, lenye maana ya ubia, au urafiki wa ndani na Roho Mtakatifu. Waamini wengi kila mahali wanajua uweza, karama na tunda la Roho Mtakatifu; lakini je, ni wangapi wetu wanaomjua kama rafiki wa karibu?

Roho Mtakatifu Ni Nani?

Baadhi ya watu wanadhani Roho Mtakatifu ni aina fulani ya nishati, uweza au radi. Lakini wanakosea.

Roho Mtakatifu Ni Mtu
Na kwa kweli ni ‘mtu’ muhimu sana; ni Nafsi ya Tatu katika Utatu wa Mungu (Mt 28:19) (2Kor 13:13). Yeye ni mtu roho, kama vile wewe ulivyo ila Yeye hafungwi na mwili. Twaweza kumwomba kila siku tukisema, ‘Roho Mtakatifu,  nijaze kwa uweza wako, niongoze, nipe hekima na ujasiri’ kwa sababu ni mtu kweli tunayeweza kuzungumza naye na kujihusisha naye.

Kwanini Jambo Hili Ni Muhimu?

Ina maana unaweza kujihusisha na Mungu kirahisi. Mwanadamu hawezi kamwe kuwa na uhusiano na nguvu, nishati au vitu visivyo hai, au hata rafiki mkubwa wa mwanadamu, yaani mbwa. Mungu anataka tuwe na uhusiano wa kibinafsi naye, na akijua kwamba twaweza tu kuwa na uhusiano na mtu, ametupa Roho Mtakatifu awe rafiki yetu kibinafsi, msaidizi na mfariji wetu.

Kwa wanafunzi walioishi na Yesu kwa miaka mitatu, Roho Mtakatifu alikuja na akachukua nafasi ya Yesu kwao na kwa kweli alikuwa karibu zaidi nao kwa sababu alikuwa ndani ya kila mmojawao. Na kwa sababu Roho Mtakatifu ni mtu- Roho alikuwa na uwezo wa kuwa na wanafunzi wote, wakati wote, na hakufungwa na mwili ili awe mahali pamoja kwa wakati mmoja kama Yesu alivyokuwa, kwa hiari yake mwenyewe. Na ndivyo ilivyo hata leo; Roho Mtakatifu, Mungu mwenyewe yuko pamoja nasi sote, wakati wote.

Je, Roho Mtakatifu Ni Nafsi Halisi?

Madaktari husema kwamba nafsi halisi ni sharti iwe na akili, hiari, na hisia. Na Roho Mtakatifu tunampima kwa vigezo hivyohivyo vitatu.

Je, Roho Mtakatifu Ana Akili?

Akili ni uwezo wa kujifunza, kuelewa na kufikiri. Ndiyo, ana akili sana! (Rum 8:27) (1Kor 2:10-13).

 

Je, Roho Mtakatifu Ana Hiari?

Hiari inahusiana na kusudio, uchaguzi, takwa na azimio. Ndiyo, Roho Mtakatifu ana hiari yake mwenyewe na anakubaliana na Baba na Mwana (1Kor 12:11).

 

Je, Roho Mtakatifu Ana Hisia?

Je, ana hisia na hisia kali? Anapenda na hiyo ndiyo hisia yenye nguvu sana aliyonayo, na kuna hisia kali katika kuugua kwake awapo kwenye maombezi (Rum 15:30; 8:26,27).

Mara Zote Yesu Anamtaja Kama Mtu

Katika mazungumzo ya mara moja tu Yesu ametumia kiwakilishi nomino mara kadhaa kumtaja Roho Mtakatifu kwenye jinsia ya kiume (Yn 16:7-11). Na katika Yn 14:15-17 Yesu anamwita Mshauri (Wakili), akiwa na maana ya Yeye asimamaye kando yako kama mwanasheria wako ili kukutetea. Roho Mtakatifu Ndiye anayeshikamana nasi kinyume na udhaifu wetu (Rum 8:26).

Roho Mtakatifu Ana Huduma Yake Binafsi

Ukiona kazi anayoifanya utashangaa, anaifanya vizuri, wakati wote, kila mahali~

 

Hufanya kazi, (1 Kor 12:11);

Hutafuta, (1Kor 2:10);

Hunena, (Mdo 13:2);

Hushuhudia, Yn 15:26);

Huelekeza, Neh 9:20);

 

Hutia hatiani (hushuhudia), (Yn 16:8-11);

Husali, (Rum 8:26);

Huongoza, (Mt 4:1);

Huongoza kwenye kweli, (Yn 16:13);

Humtukuza Yesu, (Yn 16:14);

 

Husababisha uzao mpya, (Yn 3:5,6);

Hutoa hoja, (Mwa 6:3);

Huelekeza huduma, (Mdo 8:29);

Hupeleka wajumbe, (Isa 48:16);

Huwaitia watu huduma, (Mdo 20:28);

Hugawa karama, (1Kor 12:7-11).

 

Roho Mtakatifu Ana Hisia Binafsi

Anaweza kuhuzunishwa,

kutukanwa,

kudanganywa,

kujaribiwa,

kukufuriwa,

kupingwa na kuzimwa.

(Efe 4:30) (Isa 63:10),

(Ebr 10:29) (Mdo 5:3) (Mt 12:31) (Mdo 7:51)(Mdo 5:9) (1The 5:19).

Hili Lina Maana Gani Kwangu?

Ikiwa sisi tunaweza tukawa na urafiki wa kina na washirika wetu au wapenzi wetu katika ndoa, si zaidi tukijenga uhusiano wa ndani kabisa na Mtu wa mbinguni anayeaminika kabisa, rafiki anayenipenda,  anayeishi ndani yangu, anayenena nami, anayetaka kutenda kazi pamoja nami na kupitia kwangu!

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu
Huu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Tanzania


 




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk