1985 - 2007

 

71. Kanisa Linalotumia Nguvu

Shetani alitupwa chini kutoka mbinguni, sasa mtupe nje kutoka kanisani!

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Ufu 12:7-12    Dan 10

Mstari wa Kukariri
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa (Ufu 12:11).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Hebu angalieni tabia za yule mwizi na mjadiliane jinsi kila mmojawenu alivyoziona katika maisha  na katika Jamii. Hitimisha kwa kumshukuru Mungu kwa kukukomboa.

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Andaa muda maalum wa maombi ukiwashirikisha wachungaji na wanamaombezi wazoefu na kumwomba Roho Mtakatifu akuwezeshe kupokea huduma itakayokuhakikishia kwamba uko huru na Poneria.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika ukurasa mmoja ukibainisha aina ya pepo linalotawala juu ya mji wako, na uelezee udhihirisho wa pepo hilo katika maisha ya wakazi wa mji huo.

Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Kol 1:13

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Ireland. Idadi ya watu ni 4,000,000. Asilimia 92% ni Wakatoliki; idadi ya Waprotestanti inazidi kupungua; ni taifa maarufu kwa kutuma wamishenari.

 

Falme Mbili Na Mipango Miwili

Biblia inafundisha waziwazi kuhusu kuwepo kwa falme mbili na watawala wawili. Ufalme wa Mungu ni ulimwengu wa mamlaka ya Mungu na serikali yake, na asili yake kwa ujumla ni nzuri. Ufalme mwingine unatawaliwa na Shetani na majeshi yake ya giza ambayo asili yake ni uovu mtupu. Ufalme wa Mungu ni mahali pa baraka kama inavyoonekana, kwa mfano, katika Yer 29:10-14.

Nitawajia na kuitimiza ahadi yangu ya neema kwenu, (ms 10).

Nina mipango ya kuwastawisha na wala si ya kuwadhuru, (ms 11).

Mipango yangu itawapa ninyi tumaini na maisha bora baadaye, (ms 11).

Nitawasikiliza, nanyi mtanipata.

Nitawarejesha kutoka utumwani, (ms 12,14).

Lakini mwizi haji ila aibe, aue na kuharibu (Yn 10:10). Ufalme wa Shetani ni:

Ufalme wa mashaka, kutokuamini, kuchanganyikiwa, kukata tamaa, huzuni, kukataliwa, mchepuko, majaribu, ulaghai na unajisi, udanganyifu, uongo, lawama na wizi, kutawala, kudhibiti,  uasi, ibada ya sanamu, uchawi na utumwa, uharibifu, mauaji, umezaji, mateso, hofu na mgawanyiko. Haya yote ni maelezo ya Biblia.

Upinzani Usioonekana

Ni wajibu wa Kanisa sasa, baada ya kuokolewa (Kol 1:13,14) kunyenyekea kwa Mungu, na kumpinga ibilisi kwa mapambano, na werevu katika vita vya kiroho.

Vita Na Tahadhari

Ni vema wanaopigana vita hivi wawe ni kanisa, au vikundi vya wanamaombi wa dhati, badala ya waamini mmojammoja (Yak 4:7) (Rum 12:21) (1Pet 5:9). Mada hii, na somo hili limejawa na ubishani wa kisomi na bahatisho kidogo, lakini tutajaribu kutoka Efe 6:12 kuainisha ngazi tatu za majeshi ya adui, na kupendekeza miitikio sahihi.

Watawala wa ulimwengu, kwa ujumla wake, kilimwengu.

Roho za nchi, nguvu za kipepo katika mataifa mbalimbali.

Majeshi ya pepo wachafu, hupangiwa kushambulia vikundi na mtu mmojammoja.

Msomi maarufu Dk. Peter Wagner, anaona uovu wa ngazi ya chini - wa kufanana hasa na ule uliotokea kule Samaria (Mdo 8:7); uovu ngazi ya kishirikina - mfano halisi ni Simoni Mchawi, au Elima, (Mdo 8:9; 13:6); na uovu ngazi ya kimkakati - kama ule wa Artemi wa Efeso, yule mkuu wa anga (Mdo 19:27).

Jinsi Ya Kuwashinda Watawala Wa Ulimwengu Wasioonekana

Neno kosmokrator, lina maana ya mtawala au nguvu za giza katika kizazi hiki. Mtawala wa ulimwengu huwakamata watu katika uongo mkubwa wa kiroho. Kosmokrators wanaweza kukuza roho ya mpinga-Kristo ya Uislamu, au uyakinifu, Uhindu, Ubudha, na Kizazi Kipya. Mtawala mkuu wa ulimwengu ni Shetani mwenyewe, mtu mwenye nguvu anayetajwa katika Lk 11:21, na yeye ni mfano wa hao wakuu wengine walio chini yake.

Maamuzi Ni Vita Vya Kiroho

Katika Mt 4:1-11, Yesu alimshinda Shetani katika vita vya kiroho kwa maamuzi yake ya kusimama kwenye kweli ya neno la Mungu.

Alikataa jaribu la kutumia uweza wake kujibariki mwenyewe, badala yake akachagua kujikana na kujitoa mhanga (ms 3,4).

Alikataa ufidhuli uliochanganyika na hekima za kibinadamu/kishetani, na akachagua kufanya maamuzi yatakayompa Baba yake heshima (ms 5-7).

Alikataa kuchukua njia ya mkato ya kuukwepa Msalaba wa Kalvari, na badala yake akachagua kuyafanya mapenzi ya Mungu ikiwa ni pamoja na  kuteseka, ili kuwakomboa wengine (ms 8-10).

 

Shetani aliondoka zake na hatimaye Yesu akashindwa pale Msalabani kwa kutumia silaha ileile ya kufanya maamuzi sahihi ya kutobadili msimamo wa kweli ya neno la Mungu.

Jinsi Ya Kuwashinda Arche Na Exousia

Hizi ndizo falme na mamlaka zilizotajwa katika Efe 6:12; wakuu wa giza na watawala juu ya mataifa,mikoa na miji.

Kwa mfano ‘pepo’ mchafu wa Amsterdam. ‘Mamlaka’ ya Japan inakuza ibada ya jua. Moja ya ‘mapepo’ yaliyoko San Francisco ni la ulawiti. Hispania kuna ‘pepo’ la muda mrefu la dini, kuchanganyikiwa, na mgawanyiko. Na Afrika ‘pepo’ la uchawi linashirikiana na ‘pepo’ la umaskini. (Ayu 38:7) (Ufu 12:7-9,4) (Mwa 6:1-6; 11:1-9; 10:5) (Kum 32:8) (Zab 82) (Dan 10:13,20).

Katika kitabu cha Danieli mlango wa 10 tunapata ufunuo kuhusu mapambano dhidi ya mamlaka na nguvu za giza na jinsi ambavyo maombi ya mfululizo yanavyoweza kuleta huo ufunuo muhimu na msaada wa malaika.

Jinsi Ya Kuushinda Uovu Dhidi Yako

Yesu alipinga uovu katika jamii na pia mara kwa mara alitoa pepo wachafu kutoka kwa watu walioonesha tabia isiyokuwa ya kawaida. Neno la Biblia, poneria, lina maana ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Paulo katika Efe 6:10-14 anatupa njia ya uhakika ya kuupata na kuulinda ushindi wetu:

  1. Mwe hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
  2. Vaeni silaha zote za Mungu, kwa mfano kwa kusema kweli ambayo kwa vyo vyote itakulinda na  wakati huohuo kumwudhi Shetani.
  3. Mpingeni Shetani.
  4. Salini katika Roho Mtakatifu.

Omba katika jina la Yesu na mamlaka ya jina hilo yatavunja nguvu za uovu za poneria; lakini mapambano yanaweza yakawa mafupi na marahisi iwapo mtu anayetaka kuwekwa huru atafanya haya yafuatayo:

Atambue kwamba chanzo ni cha kiroho.

Atubu dhambi zake, na kuziacha kwa msaada wa Mungu, na kuchagua kumfuata Yesu awe Mwokozi na Bwana.

Apokee msamaha katika jina la Yesu, na kumsamehe kwa jina la Yesu kila aliyemkosea na kumwumiza.

Amkatae Shetani na kazi zake zote.

Sasa mkumbushe Shetani kuhusu damu ya Kristo na jinsi Yesu alivyomshinda pale Msalabani.

Kisha mkemee kila pepo mchafu na  kumwamuru aondoke, halafu vunja kila laana kwa jina la Yesu.

Mwekee mikono mtu huyo ili ajazwe maisha yake na Roho Mtakatifu. Mwelekeze amtukuze, na kuishi katika Roho na neno la Mungu.

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Thailand

Jina la Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Nyong

Yong

12,000

 




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk