1985 - 2007

 

72. Kanisa La Kitume

Mitume kama walivyo wavuvi wazuri wanajua jinsi ya kuziweka nyavu zao katika hali nzuri

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
2Kor 10 & 11

Mstari Wa Kukariri
Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni (Efe 2:19,20).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, makanisa ya leo yanaweza kurejeshwa na kufuata mfumo wa huduma ya kitume ya Agano Jipya?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Fanyeni huduma ya kitume, mwondoke kama timu na kwenda mahali kama kijijini, shuleni au gerezani pale ambako injili haijapenya, na kuwasilisha mpango wa Mungu wa wokovu.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Tafuta ujue jinsi makanisa mengine na madhehebu yanavyosimamiwa leo na kisha andika mifano na misingi ya Biblia.

Tafakari Andiko Hili Neno Kwa Neno
1The 1:7,8

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Uzbekistan. Idadi ya watu ni 24,000,000 katika makabila mengi.

Asilimia 68% ni Waislamu na asilimia 4% ni Orthodox. Ni makao makuu ya Uislamu ya Asia ya Kati.

 

Katika Agano Jipya tunaona mitume wakitajwa kama mara 80 hivi, kwahiyo kwa vyo vyote katika kanisa la kwanza walikuwa ni watu muhimu, na kwa kweli ~

Mitume ni ‘wa kwanza’ kanisani (1Kor 12:28).

Kanisa limejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii (Efe 2:20).

Mitume na manabii wana ufunuo maalum na uwezo wa kuelewa mambo kutoka kwa Mungu (Efe 3:5) (Yud 1:17). Makanisa yanapaswa kuwa na mitume wao (2Pet 3:2).

Lakini je, mitume ni kwa ajili ya siku zetu pia au walikuwepo mwanzo kwa kazi ya kuanzisha Ukristo? Kama hata sasa wanatakiwa, ni akina nani hao na wanafanya nini?

Sisi Tunafanya Nini?

Leo hii tunaongozwa mara kwa mara na watawala au wachungaji wenye karama, lakini kama mitume bado ni ‘wa kwanza’ wa Mungu katika kanisa na moja ya  misingi yake, tunapaswa kufanya nini?

Mtume Ni Nani?

Neno Mtume lina maana ya mtu anayetumwa, na kupewa uweza wa kufanya umisheni kutoka kwa Mungu. Utume si cheo, ni wito, ni karama na shughuli kama shughuli nyingine yo yote ndani ya kanisa.

Mitume Katika Agano Jipya

Yesu, yu juu ya wote, (Ebr 3:1).

Wale mitume thenashara wa Mwanakondoo (Mk 3:14-16) (Mdo 1:26) (Ufu 21:14).

Karama ya mtume (Efe 4:11); watu kama Paulo, Yakobo, Barnaba, Timotheo, Sila, Andronika na Yunia.

Biblia haijatuambia kwamba hawa walikuwepo kwa ajili ya karne ya kwanza peke yake. Kutokana na ukweli kwamba Kristo aliweka wengine kanisani kuwa mitume  ili kutenda kazi ambayo bado haijakamilika (Efe 4:12-14) ni ushahidi tosha kwamba mitume wanahitajika sana hata leo kama karama nyingine zilizozoeleka zaidi (Efe 4:11).

Ni Nini Kazi Za Mtume?

Si kila mtume anayetenda kila kazi kama inavyoonekana katika Agano Jipya lakini kazi za kitume ni pamoja na ~

Kueneza injili, kwa mfano safari nyingi za Paulo, na ziara ya Petro kwenye eneo lile ambalo halikuwahi kufikiwa kabla katika nyumba ya Mmataifa (Mdo 10).

Kuwafikia watu ambao hawajafikiwa (Rum 15:20).

Kusababisha uinjilisti mpya kufanyika (Mdo 19:10).

Kusababisha makanisa mengi mapya kuanzishwa, kama alivyofanya Paulo kusini mwa bara la Ulaya.

Kuwa mjenzi mkuu mwenye hekima, anayejua la kufanya (1Kor 3:10; 5:3; 6:4; 7:1; 8:1).

 

Mitume Huweka Misingi Imara
Ya Kristo (1Kor 3:11)

Ya maisha katika Roho (Mdo 19:1; 8:14-17).

Ya utii mbele za Mungu (Rum 1:5).

Ya fundisho la kweli (Efe 3:2-21)

Ya viongozi wazuri (Mdo 14:23) (Tit 1:5).

 

Kuwa baba au mama wa makanisa machanga, kuyatia moyo kwa nyaraka na ziara, na kamwe si kuyadhibiti (2Kor 11:28) (1The 2:7,11).

Kukabiliana na tamaduni zisizo na maana, kama Paulo alivyopingana nazo hata kwa Petro (Gal 2:11-14).

Safari za kuuunganisha Mwili kama alivyofanya Paulo akiunganisha Yerusalemu, Antiokia na makanisa  mapya kwa mahusiano yake.  

Alionesha urafiki wa muda mrefu na uaminifu, akitenda kazi katika mahusiano na si katika mifumo na vyeo (1The 1: 5-7; 2:8) (Flp 1:8; 4:10,14,15) (Mdo 20:31; 18:11).

Utamtambuaje Mtume?

Mitume huitwa na Mungu, na wakajua, na watu wote pia. Wanaweza wakakubali wito wao, lakini hawana haja ya kutangaza nafasi yao kama cheo, na haipaswi kuwa hivyo, badala yake ni nafasi yenye majukumu makubwa. Angalia salamu za Paulo anavyoanza kuandika nyingi ya nyaraka zake; na pia angalia uone kwamba mitume ~

Mitume Pia Wanahitaji Makwao

Mitume katika Agano Jipya wanaonekana sikuzote wakitenda kazi katika timu ya umisheni au pamoja na wazee wa kanisa nyumbani ambako ni kituo cha kitume Angalia Matendo 15 na somo la 12.

Ni Nini Kituo Cha Kitume?

Ni kanisa la mfano, ambako mitume, timu mbalimbali na watu wanakusanyika pamoja kwa ajili ya Yesu na kwa ajili yao wenyewe kwa wenyewe. Ni mahali pa kuanzia na kituo cha kupatia watu, fedha na vifaa kwa ajili ya umisheni. Ni mahali pa ushirika, pa kuhuishwa, pa kuwajibika na kuwategemeza wale wanaofanya huduma za kitume, na kamwe isiwe piramidi ya huduma yenye ‘mtume aliyewazidi wenzake’ akiwa kwenye nafasi ya juu akitoa amri tu. Ni pale tu timu ya Paulo ilipokuwa nje ya kituo huko Antiokia ndipo walipojitawala na kujitegemea (Mdo 14:26-28).

Vituo Vya Kitume Katika Biblia

Makanisa ya Yerusalemu, Antiokia, Efeso na Thesalonike yalikuwa ni zaidi ya makanisa ya maeneo tu. Haya yalikuwa na huduma katika Roho Mtakatifu yakifanya maombi, uinjilisti, unabii, mikutano ya mafundisho na ibada. Kulikuwa na viongozi kadhaa, kanisa lililo hai na ushirika. Walikabiliana na changamoto za kisheria, mateso, mkakati na kupeleka timu za kitume na kuusaidia ulimwengu wa Wayahudi, na kuendelea hadi Samaria na hatimaye kwa mataifa.

 

Ni muhimu kwamba mitume wajifunze nyumbani na kisha wawapelekee wengine hayo masomo. Ni lazima vituo vya kitume vifaulu mtihani wo wote, na pawe ni mahali ambapo timu za kitume zinaona fahari kuelekeza watu na kuwakaribisha kuja kujifunza.

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Uturuki

Jina la Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Balkan Rom Gypsy

Romani, Balkan

55,000

Circassian

Adyghe

71,000

Karakalpak

Karakalpak

62,000

Mingrelian (Laz, Zan)

Laz

30,000

 




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk