1985 - 2007
74 (sehemu ya 1) Kanisa La Kimishenari
Wakiwa na Yesu maishani mwao watu walio mbali watapata tumaini, heshima na kusudi
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika Biblia Yako Soma
Mdo 11:19-30; 20:1-6
Mstari wa Kukariri
Basi hawa walipokuwa wakimfanyia
Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa
kazi ile niliyowaitia” (Mdo 13:2).
Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Kama una maono kutoka kwa Mungu,
ni watu wachache tu wanaoweza kuangamia. Je, miongoni mwenu kuna maono kwa ajili
ya waliopotea?
Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana
Tena
Undeni timu na kuchagua kiongozi,
na kisha andaeni tukio litakalosababisha kutumika kwa karama na vipawa vilivyoko
miongoni mwenu. Fanyeni maombi, wekeni mkakati, na kisha tokeni kwa utekelezaji.
Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Jifikirie kwamba wewe ni mchungaji
na una kanisa la watu 80 na kwamba unataka kuona huduma ya ulimwengu
inaanzishwa. Andika malengo yako na kila moja aya yake.
Tafakari Mistari Hii Neno Kwa Neno
Mdo 8:4-8
Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Pakistan. Idadi ya watu ni 145,000,000. Asilimia
97% ni Waislamu wenye siasa kali. Kuna matatizo makubwa ya kijamii na ya kiuchumi.
Kuna mateso kwa Wakristo ambao ni asilimia 2-3%. Watu wengi sana hawajafikiwa na Injili
Yafaa sana shirika la kimishenari likazaliwa ndani ya kanisa la eneo moja, likitegemezwa na ushirika wenye maono, na kisha likapita likianzisha makanisa kila liendako. Kanisa lako la eneo moja linaweza likawa kanisa lenye kuubadilisha ulimwengu kwa huduma ya kimataifa, kwa namna ifuatayo:
Kanisa Hilo Ni Nini?
Timotheo Cheni ndiye mchungaji
ambaye katika somo la kwanza alifundisha watu 15 kila baada ya miezi miwili na
kwa pamoja wamepatikana waamini wapya zaidi ya 100,000. Anasema makanisa yake
huko nchini Uchina ni “akiba wa watu walio katika maandalizi kwa ajili ya Agizo
Kuu”.
Unahitaji Kufanya Nini Ili Kuanzisha Huduma Kwa Ulimwengu Kanisani Kwako?
Kanisa Linahitaji Maono
Ya Mit 29:18
kwa sababu bila
maono watu wataangamia. Zaidi ya hayo kiongozi mwandamizi anatakiwa kuutwaa moyo
wa Mungu kwa ajili ya ulimwengu wa watu wasiofanana, aende na kujionea mwenyewe,
kila mwaka. Litakalomfurahisha yeye litaathiri kanisa lote.
Unahitaji Uongozi Na
Umiliki
Watambue wale Mungu
anaowainua kwa ajili ya huduma ya ulimwengu katika maombi, matoleo na katika
kwenda. Wape majukumu na kuwaweka huru na shughuli za kanisani kwako. Na hilo
ndilo lenye maana ya "kuwaacha waende zao" katika Mdo 13:1-3.
Unahitaji Hekima Kwa
Ajili Ya Huduma Kwa Ulimwengu
Omba kama Paulo
katika Kol 1:9 ili upewe uwezo wa Kimungu wa kuelewa mambo na maarifa.
Ushirika Ni Hekima
Kushirikisha mwili
wote kwa upande mmoja, na kufanya kazi kwa ushirikiano na makanisa na misheni
nyingine ni jambo jema kwa sababu baraka zimeamriwa kunako umoja. Hakuna kanisa
moja peke yake lenye uwezo wa kuubadilisha ulimwengu au hata taifa moja la watu
ambao hawajafikiwa.
Unahitaji Kuweka Malengo Na Tarehe
Malengo yanaachilia nguvu na mwelekeo. Kama ukilenga hewa utaipiga hiyohiyo kila mara, na maamuzi yasiyokuwa na tarehe hakika yatachelewa. Unahitaji kuweka malengo ya ~
Unahitaji Mkakati Unaoongozwa na Roho
Katika 1Kor 3:10, Paulo anajitaja kuwa Mjenzi Mkuu, sophos architekton, yaani msanifu mwenye hekima au bwana mipango anayepokea hekima kutoka kwa Mungu kupitia Neno lake na Roho. Hiyo hekima ilikuwa ni nini?
Mkakati Wa Paulo Wa Umisheni
Mkakati wa kimishenari wa Paulo
ulikuwa ni kwenda katika njia kuu ziendazo kwenye miji ya watu waabudu sanamu,
na kugundua lile kundi la watu ambalo Mungu amelikusudia na kufanya kila
linalowezekana kuhakikisha kwamba wameokolewa, wamekomaa na wanawahudumia
wengine. Msingi wa misheni aliouweka ulikuwa na sehemu kuu mbili ~
Makanisa Mama
Katika Biblia tofauti pekee
tunazoziona kati ya makanisa ni zile za kijiografia kama vile makanisa ya
Yerusalemu, Antiokia, Filipi, na Efeso ambayo yalizaa makanisa mengine na
kuyategemeza. Aidha yalijihusisha na shughuli za kimishenari katika kueneza
injili. Antiokia lilikuwa ndilo kanisa mama la Paulo. Alipelekwa kutokea pale na
kurejea tena pale pale katika huduma yake ya kimishenari.
Timu Za Kitume
Neno “kitume” hapa lina maana ya
kutumwa na Mungu, na si lazima kuongozwa na mtume kama ambavyo hata Paulo
hakutambuliwa hivyo kwa wakati ule. Mungu alipomwita kwenye umisheni aliunda
timu ndogo ya kitume ya watu watatu ikiwa na mkakati wa wazi wa kuwaendea
wasiofikiwa bado, Mdo 13:1. Kuanzia hapo huo ukawa ndio utendaji wake, na katika
Mdo 20:4 watu kutoka makanisa mbalimbali wanashirikiana naye katika shughuli za
umishenari.
Kanisa Na Umisheni Ni Mapacha
Kanisa lilikuwa ni kanisa na umisheni ulikuwa ni umisheni tangu mwanzo. Timu ya kimishenari ilikuwa na mamlaka ya kanisa la eneo moja; na kwa hakika lilikuwa ni kanisa linalosafiri. Paulo alipoondoka alijisimamia mwenyewe, akitegemezwa, na wala si kudhibitiwa na kanisa la Antiokia, Yerusalemu au Filipi. Timu ilijitosheleza kiuchumi. Walipokuwa barabarani, walijitawala, walijitafutia fedha kwa mahitaji yao, na walijizaa wenyewe kwa maana ya kuanzisha makanisa mapya, shule na timu za kimishenari. Lengo ni moja, lakini njia za utekelezaji ni mbili.
Hatua Zilizopendekezwa Pamoja Na Uongozi Wa Mungu
Angalia pia somo la 64; na la 74 sehemu ya 2
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina
Uganda | ||
Jina la Watu |
Lugha Yao |
Idadi Yao |
Lulba |
Luluba |
15,000 |
1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya
for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk