1985 - 2007

 

76. Kanisa La Uamsho

Ni siku kuu uamsho unapolikumba kanisa

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Isa 35;   Mdo 8:4-8

Mstari wa Kukariri
Tubuni basi, na kumgeukia Mungu, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kutoka kwa Bwana (Mdo 3:19,20).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, uamsho unamaanisha tu mikutano zaidi na mirefu?
Uamsho unatakiwa ulete mabadiliko gani katika jamii?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Soma maandiko katika kitabu cha Matendo na kujionea mwenyewe kilichotokea. Je, waweza kupata taarifa zaidi za ukuaji wa kanisa?
Je, harakati za uamsho zilianzaje? Je, palikuwepo na tukio lo lote maalum lililowavutia watu kama miujiza au uponyaji?

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Pata taarifa za shughuli za uamsho kwa kuuliza watu wengine au kwa kusoma vitabu. Baada ya utafiti wako andika taarifa ya kurasa mbili.

Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Zab 85:6

Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Tunisia. Idadi ya watu ni 9,000,000. Ngome kubwa ya Ukristo katika karne ya kwanza; sasa kuna hitaji kubwa la uamsho.

Asilimia 99.5% ni Waislamu, asilimia 0.25% tu ndio Wakristo.

 

Katika miaka ya karibuni Mungu amekuwa wa neema kwa watu wake kwa kutuma mawimbi mengi ya uhuisho kwa kila sehemu ya kanisa litakalompokea Roho Mtakatifu. Uhuisho huleta burudisho kwa waamini lakini si kama uamsho, ingawa unaweza kuwa kama upepo mwanana unaotangulia upepo wenye nguvu wa Roho unaoleta uamsho wa kweli.

Uamsho Ni Nini?

Vyo vyote unavyoanza na uhuisho wo wote unaoletwa kwa waamini na wale waliorudi nyuma, uamsho unasemekana kwamba umekuja wakati watu, wake kwa waume, ambao hapo mwanzo hawakuamini, wanapomgeukia Kristo kwa wingi na kumtukuza Mungu.

Soma Habari Za Uamsho Katika Matendo

Watu elfu tatu wakaongezeka.

Bwana akaongeza idadi yao kila siku.

Idadi ya watu ikaongezeka hadi kufikia 5000.

Idadi ya wanafunzi ikaongezeka kwa kasi.

Makutano wakamsikia Filipo, wakaona miujiza, pepo wachafu wakatoka, viwete wakaponywa, kukawa na furaha kuu mjini.

Kanisa likatiwa nguvu na moyo na Roho Mtakatifu, likakua kwa idadi, na watu wakaishi kwa kumcha Mungu.

Idadi kubwa ya watu wakaamini.

Wote wakashikwa na hofu, jina la Yesu likatukuzwa, watu wakaungama matendo yao maovu, vitabu vya uchawi vikachomwa.

Ona ni watu elfu ngapi walioamini.

Katika karne iliyopita kulionekana milipuko ya uamsho Afrika Mashariki, Indonesia, Uchina, Wales, Scotland, Argentina na Marekani. Ona Mdo 2:41;  2:47;   4:4;  6:7;  8: 4-8;  9:31;  11:21;  19:17-20;  21:20.

Kwanini Uamsho Huja?

Hakuna shaka kwamba uhuru na haki ya Mungu ya kuchagua nyakati na mahali pa kuzuru kumekuwa ni sababu ya nyakati za uamsho wa nguvu.

Ni nani aliyemwongoza roho wa Bwana au kumpa maelekezo kama mshauri wake? (Isa 40:13); …nikisema, kusudi langu litasimama, nami nitatenda lile nitakalo (Isa 46:10).

Kwa upande mwingine Biblia inatutia moyo kwamba Mungu ataitikia kilio cha mioyo ya watu, katika maombezi, mwaliko na maandalizi.

 

Itengezeni nyikani njia ya Bwana,

Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu (Isa 40:3).

 

…Itengenezeni njia ya watu;

Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake;

Twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu (Isa 62:10).

Je, Tunawezaje Kuiandaa Njia?

Kwa Kumpenda Mungu Kuliko Kitu Kingine Cho Chote

Zaidi kuliko hewa tunayovuta ni lazima tuwe na hamu ya utukufu wake, njia zake na haki yake. Hii ni hali inayojaza mioyo yetu, nafsi zetu, akili na nguvu zetu.

Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji, vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu (Zab 42:1).

 

Kwa Kumpa Roho Mtakatifu Uhuru Kamili

Hapakuwepo na mji mwingine duniani uliokuwa mgumu zaidi kupita Yerusalemu; na ni katika mji huohuo walipomwulia Yesu. Hata hivyo Roho Mtakatifu alichagua kushukia hapohapo siku ya Pentekoste, na akafanya mambo ambayo hakuwahi mtu ye yote kuyaona kabla. Kama tukithubutu kusisitiza kwamba uamsho unaweza kuja tu kwa namna tunayodhani sisi kuwa ni sahihi, Roho Mtakatifu anaweza akatupita hivihivi (Mdo 2:1-12).

 

Kuwa Na Uchungu Na Nafsi Zilizopetea

Wakati mapigo ya mioyo yetu yanapolandana na mapigo ya moyo wa Mungu, na inapokuwa kwamba kitu kinachomhuzunisha Mungu ndicho hichohicho kinachotuhuzunisha sisi, tutafanya bidii katika maisha ya kawaida ya kanisa. Kwa vyo vyote vile hatima ya nafsi zilizopotea itatawala maombi yetu.

Bwana Mwenyezi anasema, “Nami nitawatafuta waliopotea, nitawarudisha waliofukuzwa, nitawafunga waliovunjika, nitawatia nguvu wagonjwa; nao wanono na wenye nguvu nitawaharibu; nitawalisha hukumu” (Eze 34:16).

 

Kwa Kupendana Sisi Kwa Sisi

Yesu alisema kwamba tukipendana, watu wote watajua ya kwamba sisi tu wafuasi wake, na akaomba ili sisi sote tuwe wamoja ili kwamba ulimwengu upate kuamini (Yn 13:35; 17:21-23).

 

Kwa Kuishughulikia Dhambi Ipasavyo

Watu hukwepa jambo hili lakini tunapaswa kuomba msamaha kwa maumivu tunayomsababishia Mungu, maumivu tunayosababishiana sisi kwa sisi, na tunayojisababishia wenyewe kwa kuishi maisha yasiyo matakatifu. Toba ya dhati na marejesho mbele za Mungu Mtakatifu ni ishara ya uamsho wa kweli. Siku nyingi zilizopita wakati Jonathan Edwards alipohubiri, watu walijishika na nguzo za jengo la kanisa kwa hofu ya kutumbukia  kuzimu wakiwa hai. Wakati George Whitfield alipohubiri machozi mengi yalitiririka mashavuni mwa nyuso nyeusi za wachimba migodi.

 

Kwa Kuishi Katika Hofu Ya Mungu Mtakatifu

Asije akatujia kinyume kama alivyofanya si mara moja katika Biblia. Waamini wanapaswa kuwa ni watu waliotengwa kwa usafi wa maisha na ulimi usiolaani wala kumlaumu mtu mwingine na hasa mwamini (Zab 51:10-13).

 

Kwa Kudumu Katika Maombi Kwa Mungu Anayejibu Kwa Moto

Ikiwa watu wangu, wanaoitwa kwa jina langu, watanyenyekea na kuomba na kuutafuta uso wangu, na kuziacha njia zao ovu, basi nitasikia kutoka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao (2Nya 7:14) (1Fal 18:37-39).

Maombi Ya Nabii Habakuki

Ee Bwana nimesikia habari zako; nami naogopa matendo yako, Ee Bwana. Yafufue katika siku zetu, katika nyakati zetu yafanye yajulikane; katika ghadhabu kumbuka rehema (Hab 3:2).

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Mwungano Wa Falme Za Kiarabu

Jina la watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Baluch, Southern

Baluchi, Southern

100,000

Pashtun, Eastern (Pushtun, Pathan, Afghan)

Pashto, Eastern

100,000

 




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk