1985 - 2007
77. Habari Za Ufalme
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika Biblia Yako Soma
Mwa 1; Ufu 20:11-21:5
Mstari wa Kukariri
Naye atafuta kila chozi
katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala
maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Na yeye
aketiye juu ya kile kiti cha enzi asema, ‘Tazama nayafanya yote kuwa mapya…’
(Ufu 21:4,5).
Baadaye Zungumzieni
Jambo Hili
Unalopaswa kuwania ni
mategemeo ya baadaye yenye utukufu na yenye uhakika kutoka kwa Mungu kwa ajili
yako milele.
Jambo La Kufanya Kabla
Hatujakutana Tena
Tafuta kibali cha
kutembelea mashule, vyuo na vyuo vikuu ili kuwashirikisha mtazamo wa ulimwengu
wa Kikristo, uliopita, uliopo na ujao.
Kazi Ya Kuandika Ya
Stashahada
Andika taarifa ya
ukurasa mmoja ukielezea maana ya kile Ebr 6:4,5 inachosema ni kuonja karama na
uweza. Je, dhifa kamili inaweza kufananaje?
Tafakari Mstari Huu
Neno Kwa Neno
Ufu 20:15
Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Nepal. Idadi ya watu ni 21,000,000. Asilimia
89% ni Wahindu; Asilimia 0.5% tu ni Wakristo; mwaka 1960 kulikuwa na waamini 25, sasa wamefikia 50,000.
Chagua hapa > 77chart ili uweze kuona michoro kuhusiana na somo hili
Igundue Asili Yako
Unaweza ukadhani kwamba Ukristo ni kitu kigeni sana hapa duniani, au kwamba ni dini ya nchi za magharibi ambayo inaweza kuwa ya maana zaidi kuliko imani nyingine za kienyeji. Mawazo hayo si sahihi hata kidogo. Sasa unakaribia kuugundua ukweli kuhusu utambulisho wako na kuona kuwa wewe ni sehemu ya familia kubwa yenye historia inayoanzia kabla ya kuwepo wakati, na itakayoendelea hadi wakati ujao wa utukufu. Hapa pana maelezo mafupi:
1. Kabla Ya Historia
Kabla historia haijakuwepo ilikuwa ni umilele tu, (Zab 90:2). Si mengi yanayofahamika lakini Biblia inadokeza au kutoa nuru (Zab 2:7). Katika Eze 28:12-19 na Isa 14:12-20, Biblia inatoa maelezo kumhusu Lusifa au Shetani.
2. Zama Hizi
Zama hizi zilianza kwa Mungu kuumba mifumo ya sayari ikiwemo dunia, Adamu na Hawa, na wala si kwa mageuko yatokanayo na mlipuko mmoja mkubwa ambao wanasayansi wanadhani ndio ulioleta uumbaji. Baada ya anguko la mwanadamu, zama hizi hadi leo zinawakilishwa na orodha kwenye chati inayoitwa, kifo,dhambi na Shetani.
Matukio Ya Kwanza
Katika Historia Ya Mwanadamu ni…
Uumbaji, dhambi, anguko
la mwanadamu, kifo, ahadi ya Mungu ya kuweka mambo sawa, kuzaliwa kwa uadui
dhidi ya Shetani na mwanzo wa harakati zake za kutaka umaarufu hapa ulimwenguni.
Wanadamu wamegawanyika katika makundi mawili: Wakaini wanajulikana kwa
fujo zao na kutokumcha Mungu; na Wasethi kama Henoko ni wacha Mungu. Hata
hivyo panatokea uvamizi wa kiroho; yaani ndoa kati ya roho na wanadamu. Hali
hiyo inasababisha mgogoro mkubwa wa dhambi hapa duniani (Mwa 1-5).
Nuhu, Gharika Na Agano
Mwa 6-11:9. Hata hivyo
dhambi inakaa: Mwa 9:20-22, na mara inabadilika kuwa ibada ya sanamu na Mungu
anatoa hukumu penye mnara wa Babeli, ambapo unakuwa mwanzo wa mataifa na
tamaduni: Mwa 11:1-9.
Ibrahimu
Katika Mwa 11:27-12:1
na kuendelea, Mungu anaamua kumgeukia mtu mmoja, Ibrahimu, ambaye Mungu
amemkusudia awe baba wa kundi jipya la watu, watu wa Mungu.
Isaka Na Yakobo
Mwana wa Ibrahimu na
mjukuu wake wanarithi ahadi ileile kama alivyoipokea (Mwa 12:1-3), na
inapitishiwa kwa Yusufu hadi Misri kwenye miaka 400 ya utumwa. Soma Mwanzo 21
hadi Kutoka na kisha somo la 29.
Musa Hadi Israeli Na
Yuda
Kwa mkono wa Mungu Musa
aliwaokoa taifa zima kutoka Misri na wakakutana na Mungu pale Sinai (Kutoka 19
na 20; na somo la 29). Na ingawaje kamwe hawakuwa ufalme wa makuhani na taifa
takatifu, lakini waliwakilisha imani katika Mungu mmoja aliye hai kwa miaka
1,500 kila mara wakiutafuta ufalme ujao (Waamuzi-Malaki).
Yesu
Tangazo la jambo jipya
kutoka kwa Mungu lilimjia mwanamwali mmoja katika familia ya kikulima katika mji
wa kaskazini. Kwa wachungaji ambao wala hawakuwa na haki ya kutoa ushahidi
katika mahakama ya kisheria na pengine, la kushangaza, hata kwa mamajusi.
Wanatheolojia walikuwa wapi? Na waandishi wa habari je? Je, walikuwa wapi watu
wa dini waliokuwa na nguvu na ambao wangeweza kuhakikisha kwamba Mwana wa Mungu
anawarejesha kwa nguvu wafuasi wa dini ya Kiyahudi wamrudie Mungu na wito wake
mtakatifu? Mungu alijua kwamba nguvu za giza zinakaa ndani yao wanaoidhibiti
jamii. Kwahiyo injili hii, yaani mtoto huyu, walikabidhiwa wakulima, wachungaji
na mamajusi waliokuwa wanatafuta jambo ng’ambo ya nyota.
Yesu, Ni Wa Kwanza
Katika Kizazi Kijacho
Yohana Mbatizaji
anatangaza kwamba ufalme umekaribia, mwisho wa Agano la Kale. Yesu anahubiri
habari njema kwamba ufalme umekaribia, na anafundisha namna ya kuuingia. Yesu
anawatuma wafuasi wake kwenda kusema yayo hayo, na miujiza inathibitisha
kuwasili kwa Ufalme wa Mungu. Yesu, kwa kujiamini, anatangaza sheria za baadaye
za ufalme huo na kufundisha namna watu watakavyoishi humo, na majaliwa yao, kwa
kutumia mifano; kwamba si suala la matumani bali ndiyo kweli yenyewe. Anaahidi
kwamba ufalme wake utavuka mipaka ya kifo chake na anataka tuombe ili kwamba
ufalme wake uzidi kuja. Maana yake hapa ni kwamba Yesu anatangaza vita dhidi ya
ufalme wa Shetani. (Mt 3:2; 5:20; 7:21) (Yn 3:3) (Mt 10:7; 12:28) (Mt 5, 6 na 7)
(Mt 13:11) (Lk 22:30; 11:2) (Mt 12:26) (1Yn 3:8).
Msalaba Unasafisha Njia
Adui amenyang’anywa
silaha (Kol 2:15), lakini bado yupo na ataendelea kuwa wa hatari hadi Yesu
atakaporudi.
3. Kizazi Kipya Chaanza Kuingia
Ufufuko (Yn 20 – 21)
Shule ya kwanza ya Biblia (Mdo 1:3)
Ahadi ya Roho Mtakatifu (Mdo 1:5)
Mkakati wa muda mrefu (Mdo 1:8)
Kipindi cha Kanisa Chaanza
Kipindi cha utukufu wa Kristo uliositirika.
Sisi tunaonja tu, karamu yenyewe bado, ambayo kwenye orodha katika chati inaitwa ‘Ladha’.
Roho Mtakatifu ndiye anayetutia nguvu katika mapambano falme mbili hizi zinapokwaruzana na hali hiyo itaendelea hadi Yesu atakaporejea (Mdo 2:1-4). Shetani anapata pingamizi kubwa kila mara mgonjwa anapoponywa, kila mara pepo linapotolewa, kila mara mwenye dhambi anapookoka; kila mara watu wa rangi tofauti wanapoishi kwa pamoja kwa maelewano; kila mara ulafi unapodhihirika na kuadhibiwa; kila mara familia zinapoishi katika utakatifu na usafi. Shetani huja kuiba, kuua na kuharibu, bali Yesu hutuletea uzima tele.
Kristo Anakuja Mara Ya Pili Kama Mfalme
Kipindi cha utukufu dhahiri wa Kristo.
Ufufuko wa kwanza, (1Kor 15:35-57).
Shetani atafungwa na Yesu atatawala hapa duniani kwa miaka 1000 na baada ya hapo Shetani atafunguliwa na watu watamfuata tena wakifanyika mateka wa dhambi (Ufu 20:1-8).
Ufufuko Wa Pili
Hukumu ya mwisho na kufunguliwa kwa vitabu mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kisha kutupwa kwenye ziwa la moto; mauti, kuzimu, Shetani na wafuasi wake, na wale wote ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima (Ufu 20:11-15).
4. Ufalme Wa Mungu Unakuja Kikamilifu
Nchi mpya na mbingu mpya na utawala wa haki wa Mungu vitadumu milele. Angalia orodha ya mwisho kwenye chati kisha umshukuru Mungu kwa kukuleta kwenye ufalme wake salama.
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina
Mwungano Wa Falme Za Kiarabu | ||
Jina la Watu |
Lugha Yao |
Idadi Yao |
Pashtun, Western (Pushtun, Pathan, Afghan) |
Pashto, Western |
38,100 |
Yemeni Arab |
Arabic, Ta'izzi-Adeni |
15,000 |
1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya
for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk