1985 - 2007

 

78. Utukufu Wa Ufalme

 

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Mt 13:1-52

Mstari Wa Kukariri
... Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele (Ufu 11:15)

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Zungumzieni kuhusu mahali mnapoona utawala wa haki  na wenye huruma wa Mungu ukijitokeza katika mji wenu na taifa lenu. Je, huo utawala unakujaje?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Watafuteni hao watu ambao Ufalme wa Mungu ni wao; waendeeni kama mabalozi mkiwa na zawadi na habari njema. Wapeni mwaliko wa kuja kwenye Ufalme ulio bora.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Kutokana na mafumbo ya Ufalme ya Mathayo 13 toa maelezo ya kurasa mbili ukiainisha siri za kusonga mbele kwa huo Ufalme. Sehemu ya Ufalme ya somo la 3 inakupa mwongozo wa kufuata.

Tafakari Mistari Hii Neno Kwa Neno
Danieli 7:13,14

Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Taiwan. Idadi ya watu ni 22,000,000; ni Wachina.

Asilimia 70% ni wa dini za Kichina; kuna ukuaji wa kasi wa viwanda na utajiri.

 

Mara nyingi tunasoma habari za Ufalme wa Mungu (au wa mbinguni) lakini ni nini tunachokijua kuhusu nchi yetu, historia yetu na Mfalme wetu?

Huo Ufalme Ni Nini, Na Upo Mahali Gani?
Inawezekana kuwa ni jina lingine la kanisa? Ni akina nani wamo humo, na ni akina nani hawamo? Huo Ufalme umetoka wapi na je, mtu ye yote anaweza kuuingia? Na maisha yakoje katika Ufalme huo? Je, kuna mtu anayejali maskini? Uchumi wake ukoje? Watu hufanya shughuli gani huko? Je, Ufalme huo una maadui wo wote? Na je, huo Ufalme una mwisho? Wanafunzi pia walitaka kujua mengi kuhusu huo Ufalme. Hebu tuone tunachoweza kukikapata. (Mt 18:1; 20:21) (Lk 19:11) (Mdo 1:6).

1. Huo Ufalme Ni Nini?

Kwa maelezo rahisi, ufalme ni mahali pale mfalme anapotawala. Na ili ufalme uweze kufanya shughuli  zake vizuri, unahitaji mambo mawili. Kwanza ufalme huo unamhitaji Mfalme mwenye mamlaka na ambaye neno lake ni la mwisho. Pili, pawe na wananchi walio na furaha, na uaminifu kwa Mfalme wao.

Ufalme wa Mungu uliandaliwa kabla ya kuumbwa ulimwengu na watu wamekuwa wakiutazamia ujio wake kwa muda mrefu. Kanisa ni sehemu moja tu ya Ufalme huo. Ni mmoja kati ya falme mbili pekee kila mmoja ukiwa na mtawala wake na wananchi wake; lakini ni Ufalme wa Mungu peke yake unaoitwa ‘habari njema’ na usioweza kutikiswa. Una funguo zake, siri na hazina ambazo tunaweza kuzigundua; na kwa kweli baadhi ya watu wameuza mali zao zote ili kuvipata vitu hivyo. Si vya ulimwengu huu bali vyadumu milele na havionekani hadi pale mtu anapozaliwa mara ya pili, na halafu vinaonekana kirahisi tu.

(Mt 25:34) (Mk 11:10) (Mk 15:43) (Lk 8:1) (Ebr 12:28) (Mt 16:19) (Yn 18:36) (Mt 13:52) (Mt 13:44,45) (Lk 17:20,21) (Yn 3.3).

2. Ni Nani Aliyeko Kwenye Ufalme Wa Mungu?

Mfalme Ni Yesu Mwenyewe
Wakati wote Yesu alihubiri habari za Ufalme na kuwataka watu watubu na kuuendea. Wakati fulani Yesu alitumia siku 40 kuwafundisha wafuasi wake kuhusu huo Ufalme na hii inaonesha umuhimu wake, na bila shaka kulikuwa na mengi ya kuzungumza.  Tunajua kwamba Ufalme huu ulianzishwa kwa gharama kubwa sana ya mwili na damu ya Yesu.
(Lk 4:43) (Mt 3:2) (Mt 4:17) (Mdo 1:3) (Yn 18:36) (Lk 22:30).

Wenye Ufalme Huu Ni Akina Nani?
Ufalme huu ni wa Mungu, Baba, na tena ni wa watu maskini wa roho na watu wasiokuwa na cho chote wanaomfuata Yesu.  Unawahusu pia wanaoteswa, watoto, na watu wa mitaani. Wakati mwingine watu wanalazimika kwenda safari ya muda mrefu ili wafike mahali pa kuingilia kwenye Ufalme wa Mungu; na hata baadhi wanachagua kutokuoa/kutokuolewa ili wapate fursa nzuri zaidi ya kutumika katika Ufalme. Watu wanaweza kuwa na shauku kubwa sana ya kuingia.

Katika Ufalme wa Mungu mtu aweza kuwa mdogo au mkubwa. Nafasi yake inategemea utii wake na jinsi anavyoweza kuwa mfano kwa wengine.  Inasemekana kwamba mfuasi aliye mdogo sana ni mkuu kuliko shujaa ye yote wa Agano la Kale. Kwa bahati mbaya baadhi ya watu watatupwa nje kwa kumkataa Yesu, na baadhi ambao leo wanadhani kuwa ni ‘wa kwanza’ watakuwa ni ‘wa mwisho’ na wa mwisho wanaweza kuwa ni wa kwanza.

(Lk 11:2) (Mt 5:3) (Mt 5:10) (Mt 18:4) (Mt 21:31) (Mt 25:14) (Mt 19:12) (Mt 18:1,4) (Mt 5:19) (Mt 8:12) (Lk 7:28).

3. Ufalme Wa Mungu Unaonekana Wapi?

Wafuasi waliuona Ufalme ukiingia; na hauko mbali na mahali palipo na msamaha kutoka moyoni, uwezo wa kuleta utulivu, maisha adilifu, amani, furaha, ukarimu, na usawa; na mawazo yaliyobadilishwa ili kutenda mapenzi ya Mungu. Ufalme wa Mungu unatawala pale ambako watu wake wanamwakilisha vizuri kama makuhani na ambao wako tayari kwa kurejea kwa Mfalme. Katika Ufalme huo kunapatikana mahitaji kwa wenye njaa, walio uchi, wenye kiu, wagonjwa, na wafungwa.

(Mt 18:23) (Lk 12:32-34) (Mt 25) (Mt 25:35).

Kwa Namna Gani Mtu Anaweza Kuuingia Ufalme Huo?

Kamwe huwezi kuuingia kwa kulipa fedha ila ni kwa neema tu na upendo wa Mungu na kazi aliyoimaliza Yesu. Unaingia kwa miito ya Mungu, haki yake, kutenda mapenzi ya Baba, kumwamini Yeye kama watoto wachanga na kuwa na unyenyekevu wa moyo. Unaingia na kubakia katika Ufalme kwa kukubali vazi analokupa Mungu, kukatilia mbali shughuli zote ovu, kuzaliwa mara ya pili, kustahimili wingi wa shida, na kuwa tayari kuwajali walio wadogo.

(Mk 10:23) (Lk 18:24) (Kol 1:12,13) (1The 2:12) (Mt 5:20) (Mt 7:21) (Mt 18:3,4) (Mt 22:12) (Mk 9:47) (Yn 3:5) (Mdo 14:22) (Mt 25:34, 40).

4. Unafanya Kazi Gani Katika Ufalme?

Watu wa Ufalme huomba Ufalme wa Mungu uje na wanatafuta utawala wa Ufalme wa Mungu kwanza. Kazi ni kujitoa mhanga kwa niaba ya Ufalme, kutoa mapepo na magonjwa, kuhubiri ‘habari njema’ katika mataifa yote, na kwa kumtumaini Mungu na wala si juhudi za mwanadamu katika mahitaji, na wakati huohuo kutumia vema fedha za Mfalme. Kazi ngumu zaidi ni kupinga kila aina ya migawanyiko miharibifu, kupoa kidini na kutokuamini, na iwe mwiko kuangalia nyuma.

(Mt 6:10) (Mt 6:33) (Lk 18:29) (Mt 12:28) (Mt 10:7,8) (Lk 9:2) (Mdo 8:12) (Mdo 19:8) (Lk 12:31) (Mt 12:25) (Mt 23:13) (Lk 10:11; 9:62).

5.  Hatima Ya Huo Ufalme

Huo Ufalme unasonga mbele kwa nguvu na umepangwa kukua pamoja na falme nyingine za ulimwengu huu kwa uvumilivu. Utapenyeza jamii zote za wanadamu bila msaada wa mwanadamu, bali ukichochewa na uzima wa ndani.

Zipo ishara zinazoashiria ujio wa mwisho wa Ufalme na kurudi kwa Yesu kama Mfalme wa milele juu ya watu walio safi na watakatifu. Ufalme Wake utakuwa ni mahali pa karamu, naye atawaharibu adui zake wote na kisha atakabidhi Ufalme huo kwa Baba yake. 

Kutakuwa na falme ndogondogo ndani ya huo Ufalme lakini waovu hawatarithi sasa wala baadaye. Wafuasi wa Yesu watarithi miili mipya ya kiroho ya kuingilia kwenye Ufalme.

(Mt 11:12) (Mt 13:24) (Mt 13:31) (Mt 13:33) (Mt 24:14) (Mt 24:31) (Mt 25:10) (Lk 13:29) (1Kor 15:24) (1Kor 6:9) (Gal 5:21) (Lk 1:33) (Ufu 11:15) (1Kor 15:44).

 

Kwa kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Uzbekistan

Jina la Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Azerbaijani

Azerbaijani, North

38,000

Parsee

Parsi (Parsee)

190,000

 




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk