1985 - 2007

 

79. Kuja Kwa Ufalme

Katiba ya Ufalme wenyewe ni mfululizo wa misimamo na wala si sheria

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
1 Korintho 15

Mstari Wa Kukariri
…akasema, “Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni…”(Mt 18:3).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, ni kweli Yesu ni Mfalme juu ya maisha yako binafsi, juu ya ndoa yako, mahali pa kazi na kanisani? Ni maeneo yapi ambako unakosa kuzitii amri zake? Katika maeneo hayo tunaweza  kutubu na kubadilika kwa msaada wa Mungu.

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Tembelea maeneo ya jirani na taasisi muhimu katika wilaya yako; kama ofisi za serikali, polisi, jeshi, vituo vya watoto yatima na mashule. Fanya maombi ili kwamba Ufalme wa Mungu uweze kupenyeza maeneo hayo na nguvu za giza zipate kushindwa.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Wewe ulikuwa ukiwaza kwamba Ufalme wa Mungu ni kitu gani? Toa taarifa ya ukurasa mmoja ukielezea jinsi unavyoufahamu kwa sasa.

Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Mathayo 6.33

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Brunei. Idadi ya watu ni 300,000; watu wenye asili ya Malaysia na Uchina.

Ni taifa lenye utajiri wa mafuta. Asilimia 71% ni Waislamu, na asilimia 8 ni Wakristo. Hairuhusiwi kuwashuhudia Waislamu.

 

1. Huu Ufalme Ni Kitu Gani?

Je, ni uweza wa ndani unaoingia ndani ya mwanadamu? Adolf von Harnack.

Je, ni wa kipekee katika utu wa Yesu alipoingia ndani mwangu? C H Dodd.

Je, ni utawala wa kifunuo utakaozinduliwa na Mungu wakati historia itakapofikia ukomo na kuanza kwa utaratibu mpya wa kimbingu; kwa ujumla ni wa baadaye na wenye nguvu zisizo za kawaida? Albert Schweitzer.

Je, tunaweza kunyoosha mikono yetu na kuukamata na kupokea kwa wingi maisha ya ufalme, roho, kweli na kanuni katika maisha yetu, mahusiano yetu, fedha, maisha ya biashara, huduma na safari? Ufalme wa Mungu umekaribia? Roger Forster.

Au je, ufalme huo hauhusikani kimsingi na wokovu wa mtu binafsi au hatima yake bali unahusu tu matatizo ya kijamii ya wakati uliopo? Mtazamo wa Kiliberali.

Au je, ufalme huo unatambulikana tu na kanisa la kweli, ambalo kwa kadiri linavyokuwa ndivyo ufalme unavyoenea kwa njia ya umisheni na kwa taratibu kuupata ulimwengu wote kwa ajili ya Kristo na kwa njia hiyo kuubadili mfumo wa ulimwengu kuwa Ufalme wa Mungu? Augustine.

Je, yawezekana kwamba huo Ufalme na Kanisa si kitu kilekile, lakini kanisa ni Ufalme wa kijamii? Huo Ufalme ni utawala wa Mungu; ni upi basi ulio mkuu zaidi? John Wimber.

2. Ufalme Wa Mungu Hasa Ni Upi?

Hebu sasa tuangalie Biblia inasema nini kuhusu huo Ufalme:

Je, Umeelewa Sasa?
Hapana, usishangae. Kwanini kuna mawazo mengi yanayotofautiana? Je, ni hakika kwamba ufalme ni mmoja pekee?

"Yameandikwa mengi kwenye Biblia kuhusu huo ufalme na hii ni sababu ya tafsiri mbalimbali za mistari hiyo. Huo ufalme ni halisi kwa sasa, na ni baraka kwa wakati ujao. Ni baraka za ndani za kiroho zinazokuja kwa kuzaliwa upya na bado zinahusu serikali ya mataifa mbalimbali. Ni ulimwengu ambao watu wanauingia sasa, na pia ni zawadi ambayo Mungu atawapa watu wakati ujao, ingawa ni lazima ipokelewe sasa. Ni wazi kwamba hakuna maelezo rahisi! "

Maelezo yamefupishwa kutoka kwenye kitabu kiitwacho Injili ya Ufalme kilichoandikwa na G. Ladd.

(Mt 12:28) (1Kor 15:50) (Rum 14:17) (Yn 3:3) (Ufu 11:15) (Mt 21:31) (Lk 12:32) (Mk 10:15).

3. Ufunguo Wa Kufungulia Ufalme

Ufalme una maana gani? Kwa lugha nyepesi na ya kisasa una maana ya eneo la kijiografia lenye mfalme na watu anaowatawala. Neno la Biblia la ufalme ni basilea lenye maana ya uweza wa kifalme, ufalme, miliki, utawala, si ufalme hasa lakini ni uhalali au mamlaka ya utawala juu ya ufalme; uweza wa kifalme wa Yesu. Kwa lugha za zamani hii ndiyo hasa iliyokuwa maana ya ufalme. Wakati hukumu ya Mungu ilipomjia Belshaza, kilichoondolewa si Babeli yenyewe bali ni utawala wake wa kifalme (Dan 5:26). Katika mfano wa Lk 19:11 yule kabaila alienda kupokea basilea, au haki ya kutawala.

4. Ufalme Wako Uje

Yesu alituagiza tuombe ili ufalme wake uje, na tunapaswa kuutafuta huo kwanza kama watoto wadogo (Mt 6:33; 6:10; 18:3).

Lakini Tunachoomba Hasa Ni Nini?
Je, ni kanisa zaidi? Au ni mbingu duniani, jawabu la machafuko ya mwanadamu, au uweza wa kutawala ulimwengu huu kwa ajili ya Kristo? Tunamwomba Yesu, Mfalme, atawale maisha yangu na yetu sote. Tunaomba mapenzi yake yatendeke, kuongezeka kwa utawala wake, ubwana wake au ufalme wake. Kwahiyo maombi yetu kuhusu kuja kwa utawala wake yanapojibiwa, ndipo sasa mbingu inaingia maishani mwetu, familia zetu, makanisani na kwenye tamaduni.

" Unaweza ukajua tu kwamba ufalme wa Mungu upo mahali kwa kuona amani na upatanifu miongoni mwa watu kwa jinsi wanavyokaa vema na Mungu, na wao kwa wao. Ikiwa huoni amani na upatanifu, ni ishara ya wazi kwamba ufalme wa Mungu umezuiwa, na jambo fulani lifanyike kurekebisha hali hiyo”, John Wimber.

5. Sasa, Ufalme Wenyewe Uko Wapi?

"Ufalme wa Mungu umejawa na watu wenye njaa, kiu, na wanaotafuta; wakibisha kwenye milango ya mbinguni wakiwa na tumaini la kupokea kutoka huko kweli, uweza na uadilifu hadi mbingu ihamie hapa duniani. Ni wazi kwamba yapo mambo ambayo tayari yamekwisha fanyika na mengine ni wazi kwamba bado hayajafanyika. Katika Ufalme wa Mungu hatupaswi kuvuta na kukumbatia mambo ya zamani, bali kuvuta na kukumbatia mambo yajayo ya Mungu”.   Kutoka kitabu kiitwacho Ufalme Sasa, cha Gerald Coates.

"Ufalme wa Mungu upo katika kila taifa ambako watu wamempokea Yesu kama Mfalme. Ufalme huu ni wa kiroho lakini ulio dhahiri, na unaoonekana katika upendo uliotoka katika ulimwengu mwingine. Ufalme wa Mungu pia ni wa baadaye wakati ambapo Yesu ataukabidhi kwa Mungu na kukomesha kabisa utawala wote wa adui, uweza na mauti, na siku moja atatuletea mbingu mpya na nchi mpya (1Kor 15:24-26). Na mpaka wakati huo tunaendelea kuishi katika ulimwengu uliojawa na maadui wa Mungu na watu wake. Shetani anaitwa mungu wa zama hizi, mkuu wa uweza wa anga na ulimwengu wote uko chini ya utawala wake. Na yale yaliyoandikwa baada ya Msalaba! Kabla ya Msalaba Shetani alikuwa na udhibiti mkubwa wa karibu kila kitu; alitaka kumpa Yesu ulimwengu wote. Lakini ulimwengu sasa unakaribia kusikia habari njema kwa kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia na jeshi la ukombozi liko mlangoni kwa wanadamu”.  Kutoka kitabu cha C. Peter Wagner kiitwacho Kuusambaza Moto.                    (2Kor 4:4) (1Yoh 5:19) (Efe 2:2) (Lk 4:6).

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Uingereza

Jina la Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Parsee

Parsi (Parsee)

75,000

 




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk