1985 - 2007

 

8. Ishara Na Miujiza
Kuguswa Na Mungu
 

Support Pages   Index To All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index


Katika Biblia Yako Soma
Kutoka 33:12-23;  Mdo 8

Mstari Wa Kukariri
Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. Ikawa furaha kubwa katika mji ule (Mdo 8:6-8).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Ina maana gani, leo, kusema kwamba Yesu ni yeye yule jana, na leo na hata milele?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Sasa, unatakiwa uende ukafanyie kazi yale uliyojifunza. Mwombe Mungu akuongoze na kukupitisha kwenye mazingira ambapo utukufu wake na uwepo wake vitadhihirika.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Orodhesha matukio makuu yasiyo ya kawaida katika kila mlango kwenye kitabu cha Matendo. Andika mstari mmoja kwa kila tukio.

Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Yn 14:12

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Morocco

Idadi ya Watu: 30,000,000. Waislamu ni 99.8%. Idadi ya Wainjili ni 400.  

Walikuwepo Wakristo wenye nguvu mwaka 500 AD, Leo kanisa linateswa sana.
 

 

Hakikisha umewafundisha wengine somo hili.
Kila mara omba na kujiandaa ukiongezea mistari mingine ya Biblia
na mifano yako mwenyewe ili kufanya somo lieleweke vizuri zaidi.

 

Je, umeona jinsi kanisa la kwanza lilivyokua haraka kwa idadi ya watu na kiroho?

Hayo yaliwezekanaje miongoni mwa watu waliokandamizwa na tena wasio wasomi? Sababu mojawapo ni ishara na miujiza ya mara kwa mara kutoka kwa Mungu. Lakini je, haya yanawezekana leo?

1. Imanueli – Mungu Pamoja Nasi

Baada ya kipindi cha Agano la Kale kilichokuwa na wingi wa ishara na miujiza, ndipo akazaliwa Bwana wetu na kuweka misingi ya Ukristo ambao ulikuwa karibu kuanzishwa. Ujio wa Yesu uliandamana na ishara, miujiza, malaika, mafunuo, ndoto za kinabii na kimiujiza (Luka na Mathayo 1 & 2).

Watu Wa Mungu
Ni kitu gani kinachowatofautisha watu wa Mungu na mtu mwingine ye yote hapa duniani? Musa katika Kut 33:15 alisema kuwa ni uwepo wa Mungu miongoni mwetu ndio unaotufanya kuwa watu wenye uwezo usio wa kawaida. Zaidi ya  elimu ya kawaida tunayojifunza, tunaishi kwa elimu ya ufunuo, kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu, riziki kwa njia zisizo za kawaida na kuingilia kati kwa Mungu katika maisha yetu (Mt 4:4).

Yesu Ni Mfano Kwetu
Bwana Yesu, si kwamba alifanya tu mapenzi ya Mungu katika kuonesha jinsi Baba alivyompenda na kumtunza mwanadamu, lakini pia alituamuru na kutupa uwezo wa kufanya yayo hayo na makubwa kuliko hayo (Yn 4:34) (Ebr 1:3) (Yn 14:12) (Mk 16:20) (Mdo 1:8).

2. Je, Yesu Alifanya Nini?

Miujiza Ya Uponyaji
Kijana wa yule mtu mkuu aliponywa (Yn 4:46); Mama mkwe wa Petro aliponywa (Mt 8:14); Kutakaswa kwa mkoma (Mt 8:3); Mwenye kifafa aliponywa (Mt 9:2).

Miujiza Zaidi Ya Uponyaji
Mtu yule dhaifu aliponywa (Yn 5:5); Mkono uliopooza (Mt 12:10); Mtumishi wa yule askari (Mt 8:5); Lile suala la damu (Mt 9:20); Watu vipofu (Mt 9:27); Malko aponywa (Lk 22:51); Binti wa mwanamke Mkananayo (Mt 15:22); Kiziwi na bubu aponywa (Mk 7:33); Wale vipofu (Mt 20:30); (Mk 8:23) (Mk 10:46); (Yn 9:1); Wenye ukoma kumi (Lk 17:12); Mwanamke aliyekuwa amepinda (Lk 13:11); Yule mwenye ugonjwa wa safura (Lk 14:2).

Miujiza Ya Kufufua Wafu
Kijana wa mama mjane (Lk 7:11); Binti wa Yairo (Mt 9:18); Lazaro (Yn 11:1-44); Kufufuka kwake Mwenyewe (Lk 24:6); (Yn 10:18).

Miujiza Ya Kufunguliwa
Waliopagawa na mapepo (Mt 8:28) (Mt 9:32) (Mt 12:22); (Mk 1:26); Mtoto mwenye kifafa (Mt 17:14).

Miujiza Juu Ya Asili
Dhoruba yatulizwa (Mt 8:26); Kutembea juu ya maji (Mt 14:25); Mtini walaaniwa (Mt 21:19); Alivyojidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufa.

Miujiza Ya Chakula
Maji yabadilishwa kuwa mvinyo (Yn 2:9); Samaki waliovuliwa (Lk 5:6; Yn 21:6); Kushibishwa kwa watu 5,000 na 4,000 (Mt 14:15; Mt 15:32); Fedha ya kulipia kodi (Mt 17:24).

Yesu ni yeye yule, jana na leo na hata milele (Ebr 13:8).

3. Matendo Ya Mungu

Kitabu cha Matendo Ya Mitume ni kitabu kwa ajili ya kanisa cha kutuonesha maisha ya kawaida ya Kikristo. Kitabu hicho kina milango 28 na katika kila mlango utakuta ishara zisizo za kawaida, miujiza na matukio mbalimbali.

Kuna matukio ya mara kwa mara ya kuonekana kwa Yesu, utendaji wa Roho Mtakatifu, na watu kutembelewa na malaika. Kuna maneno ya kusikika kutoka kwa Mungu, nabii, lugha mpya, njozi, maono, kupigwa butwaa na watu kuchagua kuamini.

Kuna kuponywa, kufunguliwa, kujazwa Roho Mtakatifu, hukumu za kutisha za kimbingu, na ishara nyingi na miujiza. Haya ndiyo maisha ya kawaida ya Kikristo, na si ya ajabu kama wengi wanavyofikiri hivi leo.

Nyaraka Zinaeleza Yote
Paulo aliegemea sana kwenye ishara na miujiza, angalia (Rum 15:17-20) (Gal 3:5) (2 Tim 4:17). Waebrania mlango wa pili mstari wa nne, ni ushuhuda mwingine wa mwandishi, na Petro na Yakobo walishawishika na nguvu ya uponyaji ya Mungu, (1Pet 2.24) (Yak 5:14,15). Kunako mwaka wa 400, mtumishi mmoja aliyeitwa Augustine aliandika habari za kutokea kwa miujiza eneo la Afrika Kaskazini; na huo ni udhihirisho kwamba ishara na miujiza hazikuondoka na mitume wa kwanza.

4. Ni Nini Kazi Ya Miujiza?

Miujiza si kama sarakasi inayowafanya kushangaa, wala haifanyiki ili kumfanya maarufu mtu yule anayetumiwa na Mungu. Halikadhalika miujiza si uchawi au namna ya mazingaombwe.

Kinyume chake ni ishara na uthibitisho wa ukaribu wa Mungu, na maeneo mazuri ya huruma zake kwa hao wanaoteseka au waliobanwa na mapepo wachafu. Miujiza inatuelekeza kwenye Msalaba wa Yesu na uweza Wake (Mdo 5:12-14).

5. Namna Ya Kuandaa Njia Kwa Ajili Ya Miujiza

Kwanza usisahau kumwomba Yesu atende leo yaleyale aliyotenda jana, akithibitisha neno lake kwa ishara zinazofuatana nalo, ikiwa ni za mara moja au ni za taratibu (Yak 4:2) (Ebr 13:8).

Kumbuka Mambo Matatu Yanayoleta Uweza
Kusifu, kuhubiri, na kuomba. Kama walivyofanya wafuasi wake nenda kila mahali, ukimwomba Bwana atende kazi pamoja na wewe (Mk 16:20).


Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu
Huu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili; Wataje Kwa Majina
 
 

Bhutan

Jina La Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Dzalakha

Dzalakha

50,000

 

 






 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index To All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk