1985 - 2007

 

81. Malengo Ya Ufalme

Mwandishi na mwamini Aleksandr Isayevich Solzhenitsyn aliyaona haya

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Isaya 11 na 12

Mistari Ya Kukariri
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe … (Isa 9:6,7)

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Je, pangekuwa na tofauti gani iwapo wakristo zaidi wangeingia kwenye jamii yo yote tuliyoiainisha na wakasimama kwa ajili ya Mungu na kwa ajili wa watu?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Andaa mkutano kwa ajili ya wafanyakazi, walimu, waandishi wa habari, watumishi wa serikali na kadhalika, ili kuwaombea na kuwahamasisha kama wamishenari wa ufalme.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Andika makala fupi kwa ajili ya jarida la kanisa au dhehebu ukiwahamasisha waamini ili waulete ufalme wa Mungu uwe kwenye nguzo za taifa.

Tafakari Mistari Hii Neno Kwa Neno
Mithali 11:10,11

Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Somalia. Idadi ya watu ni 8,000,000 wakiwa katika koo nne kuu. Asilimia 99.96% ni Waislamu. Taifa hilo limerudishwa nyuma na Uislamu, limeharibiwa na hali ya kutokuwepo na serikali; ni eneo hatari sana.

 

Tunagundua utume na mkakati wa ufalme wa kuutimiliza kila mara tunaposali sala aliyotufundisha Bwana Yesu katika Mathayo 6:9,10, “Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni.”

Umisheni Wenyewe Ni Kumkweza Mfalme
Kama ilivyo kwa watu wa dunia wanapoungana na mbingu katika kumsifu na kumwabudu Mfalme wao halali (Ufu 4:8-11; 5:9-14).

Mkakati Ni Kueneza Utawala Wa Ufalme Wa Haki Yake
Kuongezeka kwa serikali ya Kristo na amani yake hakutakuwa na mwisho (Isa 9:7), kwahiyo hatua kwa hatua, eneo lote lililoshikiliwa na Shetani kwa ulaghai wake na upumbavu wa mwanadamu pale Edeni, litakombolewa. Ufalme ni po pote anapotamalaki Mfalme na katiba ya ufalme wa Mungu, na kulazimika kuwa na mgongano na ufalme wa Shetani, mwanadamu na ulimwengu huu.

Pale Msalabani ni marafiki wachache tu waliomkiri Kristo kuwa Bwana, Mungu na Mfalme Ajaye; lakini leo hii watu kwa mamilioni wanasujudu kwa furaha na kukiri kwa vinywa vyao kwamba Yesu ni Bwana. Serikali yake inazidi kuongezeka.

Ufalme Utakuja
Siku moja kutakuwa na amani hapa duniani kati ya mwanadamu na Mungu, kati ya mwanadamu na mwanadamu mwenzake, asili na mazingira. Ufalme huo utakapokuja katika ukamilifu wake dunia itajawa na maarifa ya Bwana kama vile wingi wa maji baharini (Isa 9:1-9; 11:9).

1. Ufalme Unaoenea

Mkakati wa Ufalme kwa kazi za umisheni una sehemu tatu za kuongeza serikali ya Mfalme -

1. Umisheni ndani ya kila mwamini.

2. Umisheni ndani ya kila taifa.

3. Umisheni ndani ya ulimwengu wote.

"Kumrudia  Mfalme na Ufalme wake kutagusa kila jamii, vyombo vya habari, biashara na viwanda. Kurudi huko kutaathiri kwa kiasi kikubwa ulimwengu wa burudani, siasa, elimu na tiba, na kusababisha mgongano utokanao na pande mbili kupingana, lakini kimsingi ni mgongano wa roho kwa sababu Roho wa Ufalme wa Mungu ni tofauti kabisa na roho wa ufalme wa giza. Na si kwamba roho hizo zimetofautiana tu bali pia zinapingana!"
Kutoka kwenye kitabu cha Gerald Coates, kiitwacho Kingdom Now, yaani Ufalme Sasa.

Mwandishi maarufu ulimwenguni H G Wells, na ambaye alikuwa bado hajaamini, aliwahi kusema, "Kama kuna badiliko lo lote kubwa na la msingi lililowahi kuletwa katika akili za mwanadamu ni wazo la kuubadilisha mfumo wa ulimwengu na mfumo wa Mungu, yaani Ufalme wa Mungu uchukue nafasi ya mfumo wa ulimwengu ." Huo ni ufafanuzi mzuri sana wa umisheni wa ufalme.

2. Umisheni Kwa Kila Mwamini

Paulo aliandika katika Flp 2:12,13; na 1:6, "…utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.” Na “Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.” Kwa kadiri unavyoendelea na kozi hii utagundua njia nyingi anazozitumia Mungu kufanya kazi ya umisheni ndani yako.

3. Umisheni Kwa Kila Taifa

Kila taifa lina nguzo zinazoshikilia jamii yake na hizo huathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya watu wake, ama kwa wema au kwa ubaya, ama kumwelekea Mungu na maisha ya haki, au kumwelekea Shetani na rushwa na udhalimu, kutokuwepo na usawa, na umaskini mkubwa.

Nguzo Za Jamii

Serikali
Siasa za kitaifa na za kienyeji, utawala wenyewe, mahakama na magereza.

Familia
Ndoa, madawa, hospitali, kuwajali maskini, wasikwao, na yatima.

Vyombo Vya Habari
Waandishi, redio, magazeti,TV, kompyuta, na mtandao wa kompyuta.

Sanaa
Muziki na uandishi wa nyimbo, kupiga rangi, uandishi, mashairi, uchongaji vinyago na ubunifu.

Burudani
Michezo, kaseti, CD, video, kumbi za starehe na sinema.

Dini
Hizo imani, makanisa, misikiti, mahekalu, vinyago na imani potofu.

Elimu
Kuanzia chekechea na shule za msingi hadi shule za sekondari na vyuo vikuu.

Biashara
Chumba cha mikutano, benki, maduka ya hisa, na mahali pa kazi.

Mungu anataka kila mwamini kuungana naye katika utume wake wa kuongeza utawala wa haki wa ufalme katika taifa. Tangu enzi za Bustani ya Edeni kila moja ya hizo nguzo, kwa kiwango fulani imekuwa ikimilikiwa na ufalme wa Shetani; lakini tangu Msalaba, njia imefunguliwa ya kumfukuzilia mbali adui na nguvu za giza na mahali pake kuuleta Ufalme wa Mungu (Kol 2:15).

Chumvi Na Nuru
Utawala wa ufalme unaongezeka pale waamini wanapojitambua wenyewe kwamba wao si waajiri wala waajiriwa bali ni wamishenari waliotumwa na Mungu kwenda katika ulimwengu ulioko ndani ya taifa lao na kuwakomboa watu kwa ajili ya Mfalme. Utume wa Ufalme unasonga mbele kwa maombi, kwa imani na kwa kuishi maisha ya haki; Mungu anatukuzwa na taifa linabadilika kidogokidogo.

Watu Wayaone Matendo Yako Mema
Soma Mt 5:13-16

Mwenye haki anapostawi, mji hufurahia; na kupitia kwake mji huinuliwa. Lakini kwa kinywa cha mtu mwovu mji huharibiwa.  Haki huliinua taifa, lakini dhambi ni aibu ya watu wo wote (Mit 11:10,11; 14:34).

4. Umisheni Kwa Ulimwengu Wote

Isaya anasema katika mlango wa 11 ms.9 kwamba siku moja dunia yote itajawa na maarifa ya Bwana kama vile maji yaijazavyo bahari. Huu ni Utume Mkuu au Agizo Kuu la Ufalme na unaweza ukapata kujua kutoka kwenye maandiko wito wako wa kujiunga na Mungu katika utume huu (Mt 28:19; 22:36-40).

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

Vietnam

Jina la Watu

Lugha Yao

Idadi Yao

Kim Mun (Mun, Gem Mun)

Kim Mun

90,000

Phu Thai

Phu Thai

150,000

 




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk