1985 - 2007

 

82. Ufalme Wenye Umoja

Mtu mmoja mashuhuri Bw. George Bernard Shaw aliwahi kuulizwa, "Ulimwengu una tatizo gani?" Alijibu kwa kuliandikia gazeti la London Times maneno haya, "Kuhusu swali mliloniuliza, ‘Ulimwengu una tatizo gani?’ Mimi ndiye. Wenu, G.B. Shaw”

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  
World Christian News   
Who Are We?   Site Index
 

Katika Biblia Yako Soma
Yn 17 na Mdo 10

Mstari wa Kukariri
Kuna mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote (Efe 4:4-6).

Baadaye Zungumzieni Jambo Hili
Kila mmoja apeleleze moyo wake ili kuona kama kuna namna ya chuki bila sababu, mawazo yaliyojengeka kabla ya kuona, na mila; kisha ungama na kutubu kwa ajili ya wale waliotakaswa na Mungu bali wewe ukawaita najisi. Ni nani akina Kornelio katika eneo lako?

Jambo La Kufanya Kabla Hatujakutana Tena
Wiki hii watembelee akina ‘Kornelio’ wengi kadiri uwezavyo ili kuwatia moyo.

Kazi Ya Kuandika Ya Stashahada
Katika ukurasa mmoja andika mapendekezo yako kuhusu ni nini kifanyike katika eneo lako, ili kupitia umoja wetu, watu wapate kuamini.

Tafakari Mstari Huu Neno Kwa Neno
Efe 4:3

Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu

Ombea taifa la Colombia. Idadi yao ni 35,000,000.

Asilimia 93% ni Wakatoliki; na asilimia 3.1% ni wa madhehebu ya Kiinjili. Ni maarufu kwa madawa ya kulevya na fujo. Kuna kiasi fulani cha ukuaji wa kanisa.

 

 

1. Je, Maombi Ya Yesu Yatajibiwa?

Yesu aliomba ili kwamba sisi tupate kuwa wamoja kama vile Mungu alivyo Mmoja, angawa ni nafsi tatu katika Umoja huo. Mungu anataka kundi lake pia liwe moja, chini ya Mchungaji mmoja, ingawa kuna hali ya kuwa anuwai katika kundi hilo. Kebehi kubwa zaidi tunayoipata kutoka kwa watu ni kanisa letu kuwa na migawanyiko mingi; na vilevile hatuna udhuru kwa kupuuzia injili. Kwa ujumla watu hawana tatizo kubwa na Mungu, tatizo linaweza kuwa kwetu sisi, namna tunavyomtambulisha kwa mataifa. (Yn 17:11; 21:22; 10:16).

Je, Uinjilisti Wako Unafanya Kazi?
Wakati mwingine tunatoa kiasi kikubwa sana cha fedha kugharamia shughuli za umisheni, lakini hatutilii maanani mkakati wa uhakika zaidi wa uinjilisti.(Yn 17:21-23 na Yn 13:34,35).

2. Ahadi Ya Kuwa Wamoja

Kuongezeka Kwa Upako Na Chakula
Katika 1Nya 12:38,39; 2Sam 2:4 wakati Daudi na wale watu wenye nguvu walipokuwa wamoja.

 

Baraka Zilizoamriwa
Mlima Sayuni ni mahali pakame na penye mavumbi, lakini ndugu wanapokaa kwa umoja wanakuwa kama Sayuni inavyofurahia kila siku maji ya uzima yanayoufanya Mlima Hermoni kuwa maarufu. Mafuta kwa ajili ya uponyaji na kwa ajili ya upako hutiririka kutoka kichwani na kuufikia mwili wote (Zab 133).

 

Kwanini Tunapendelea Kulaaniwa?
Baraka za jinsi hiyo haziwezi kupatikana pale tunapong’ang’ania kugawanyika na kuwa na madhehebu mengi kila moja likiwa na makanisa yake, vyuo vyake, agenda zake, na shughuli zake za umisheni. Udhehebu unapingana kabisa na sala ya Yesu, na unajenga kuta za ubaguzi zilizoendelezwa na kudumishwa na vizazi vingi pasipo na makasisi wa kanisa. Kila anayeshabikia udhehebu ni mwasi mbele za Mungu.

3. Kwanini Haya Hutokea?

Watu Walioanguka
Ni vema tuelewe kuwa hata wakristo wanaweza kuwa na ubinafsi, mashindano katika tamaa ya makuu, uchu wa madaraka na kujijengea himaya binafsi, kama hali hii haitazuiwa.

 

Mkakati Wa Kishetani
Shetani ameingia kanisani siku nyingi ili aendeshe vita akiwa ndani ya kanisa badala ya kufanya tu mashambulizi akiwa nje (Lk 11:17).

 

Twajenga Kuta Na Wala Si Misingi
Kumbuka maneno haya kwa ajili ya umoja:

 

·         kweli zisizokuwa na shaka,

·         tafsiri

·         mafundisho

·         mawazo binafsi

Tunapoangalia kweli zisizokuwa na shaka kama vile imani kwamba Mungu yupo, dhambi ya mwanadamu, Kristo kama Mwokozi, na uzima wa milele; sisi ni wamoja katika mambo hayo. Kweli zisizokuwa na shaka ni hoja inayokubaliwa nasi sote na hasa tunapokabiliana na dini potofu kwa pamoja.

Lakini tunapoendelea na mtindo wa kuhubiri tafsiri zetu wenyewe kwa mstari fulani katika Maandiko, au mafundisho yetu wenyewe kutoka kwenye mistari kadhaa ya Maandiko, au mbaya zaidi tunapong’ang’ania kautamaduni ketu wenyewe au mawazo binafsi na hisia zetu hata kama si sahihi, basi tujue kwamba tunajenga kuta zinazotugawa.

4. Kuwa Wamoja

Tunapaswa kumshukuru Mungu kwamba katika maeneo mengi ya ulimwengu huu kuna mvumo mpya na mzuri, wa upepo kutoka kwa Mungu. Je, tunaweza kufanya nini ili kusaidia kuleta uponyaji kwa mwili wa Kristo uliopasuka na kugawanyika?

 

Toba
Mtu mmoja mashuhuri sana Bw. George Bernard Shaw aliwahi kujiuliza, "Hivi ulimwengu una tatizo gani?" Alijijibu swali lake mwenyewe kwa kusema, "Mimi ndiye." Tofauti iliyopo kati ya maneno mawili ya Kiingereza UNITED(-iliyounganika) na UNTIED(-iliyofunguliwa, mathalani mzigo wa kuni) ni mahali ilipo herufi I.(Na herufi I inaposimama yenyewe katika lugha ya Kiingereza ina maana ya mimi). Mara zote jibu linaanzia kwangu na mahali nilipo kuelekea kwako.

 

Tulinde Sana Kile Alichotupa Mungu
Efe 4:3 inatuagiza kuuhifadhi umoja wa Roho katika amani. Kuhifadhi kitu maana yake ni kwamba kitu hicho kilishakuwepo, kwa hiyo sisi tumeunganika sana kuliko tunavyodhani, ingawa yapo mambo mengi yanayotupa changamoto. Umoja wa Roho ni umoja unaoletwa na Roho Mtakatifu, na wala hauletwi na kufanana kwetu katika mafundisho, utamaduni, mtindo wa maisha au taratibu za ibada.

 

Tubu Kwa Ubaguzi Binafsi
Katika Mdo 10: 9-16, Mungu alimwonesha Petro katika maono bustani ya wanyamapori ikishuka kutoka mbinguni juu ya kitambaa. “Petro amka, chinja ule.” Petro Myahudi yule akajibu “Hasha Bwana, umekosea. Ninazijua fika sheria za dini yangu; siwezi kula hao wanyama.”

Na katika kuufikisha ujumbe Mungu anampa Petro changamoto mara tatu kuhusiana na ubaguzi wake, mawazo yake ya awali, ukaidi wake, ubinafsi wa dini yake na wa kabila lake. Kwanini? Alikuwa anamwandaa kwa ajili ya uamsho mahali ambapo hakupatazamia, mahali ambapo asingeweza kwenda kutokana na ubaguzi huo. Ni nyumbani kwa Mmataifa mmoja ambako Mungu alikuwa akimsubiri (Mdo 10:17-48).

Ni Najisi - Au Hajulikani Na Hapendwi?
Tunahitaji kuwafikia akina ‘Korinelio’ wa kileo ambao yawezekana tamaduni zetu zimetofautiana, na pengine hatuwapendi na tusijue kwamba Mungu anawajali. Na, je, ni watu wangapi wa rangi tofauti, dini na madhehebu tofauti ambao wanataka kumpenda Mungu wasiyemfahamu? (Mit 30:1-6).

5. Kufanyika Ufalme Uliounganika

Wakristo wanaweza kuwa watu wa mapokeo, au wana karismatiki, au wenye msimamo mkali; lakini, je, tunaweza kukua pamoja ili ulimwengu upate kuamini?

Tunaweza Kufanya Nini?

 

Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Ambao Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa Majina

 

Vietnam

Jina la Watue

Lugha Yao

Idadi Yao

Roglai, Southern

Roglai, Southern

20,000

Tai, Red (Thai Deng)

Tai Daeng

100,000

 




 1985 - 2007

With many thanks to Pastor Dastan Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com


© Dr Les Norman  The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial purposes. Freely you have received, so please freely give.

Support Pages   Index to All Lessons   School of Finances  

World Christian News   
Who Are We?   Site Index

www.dci.org.uk