1985 - 2007
83. Ni Ufalme Au Maafa
Jumbe za nyakati za mwisho kutoka mbinguni
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Katika Biblia Yako Soma
Ufunuo 14
Mstari wa Kukariri
”…Mcheni Mungu, na
kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya
mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji” (Ufu 14:7)
Baadaye Zungumzieni Jambo
Hili
Jadilini jinsi
mnavyowaona wale wapanda farasi wanne katika Ufunuo wanavyopita duniani katika
siku za maisha yenu.
Jambo La Kufanya Kabla
Hatujakutana Tena
Andika makala ukiwaonya
watu kuhusu unabii wa Biblia kuhusiana na kuanguka kwa biashara, na kuyapeleka
kwenye redio na magazetini. Usitumie mbinu za vitisho.
Kazi Ya Kuandika Ya
Stashahada
Andika ukurasa mmoja wa
mapendekezo ya namna bora ya kumfanyia Bwana ibada makanisani mwetu tukizingatia
njia za kumletea yeye utukufu.
Tafakari Mistari Hii
Ufu 19:1,2
Tumia Muda Mfupi Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Eritrea. Idadi ya watu ni 4,000,000 katika makabila tisa. Kumekuwako na miaka 30 ya vita na njaa. Asilimia 50% ni Waislamu; na asilimia 40% ni Orthodox. Wana changamoto kubwa ya kujenga upya taifa lao.
Watu wengi wanaamini kwamba sasa tupo katika siku za mwisho kabla Yesu hajarejea kama Mfalme. Hakika hakuna siku baada ya leo. Kumalizika kwa mwaka 1999 na kuingia 2000 na kuanza kwa milenia mpya kuna umuhimu mkubwa wa kinabii kwa watu wengi; na hata kutimia kwa mwaka wa 6000 katika kalenda ya Kiyahudi kuna umuhimu mkubwa kwa wengine pia. Wanasayansi wanahofia uharibifu wa mazingira, migogoro ya kisiasa inaendelea, na kiroho sisi tunajua ya kwamba dhambi, uhalifu, udhalimu na kukosekana usawa havitadumu milele. Kuna jambo linalokwenda kutokea.
Wapanda Farasi Wa Ufunuo
Katika Ufunuo 6:1-8 tunajifunza habari za wapanda farasi wanne watakaoiendesha dunia. Sauti za kwato zao hazikuwahi kueleweka vizuri. Aliyempanda farasi mweupe ni Yesu, naye atashinda mioyo ya wanadamu (Ufu 19:11).
Ni jambo la kushukuru kwa kuwa Biblia inasema kwamba dhambi inapoongezeka, neema nayo huzidi.(Rum 5:21). Tunakwenda kukutana na malaika watatu wenye jumbe zinazoeleweka kutoka kwa Mungu kuhusiana na nyakati za mwisho. Inawezekana ni viongozi wa Kikristo watakaousikizisha ulimwengu kwa sababu katika Ufunuo ule mlango wa pili neno malaika linamaanisha viongozi wa makanisa.
1. Malaika Wa Kwanza
Anahubiri Injili ya milele kwa kila taifa, na kabila na lugha kama yenye umuhimu wa kwanza mbele za Mungu. Malaika huyu ana jumbe tatu:
2. Malaika Wa Pili
Huyu anasema, ‘Umeanguka Babeli’ (Ufu 14:8). Babeli ni nyumbani kwa mapepo na roho chafu na kwa uchawi wao huwapotosha mataifa na kuwatia wendawazimu hata wakawaua watakatifu wengi. Wafalme, watawala na wafanyabiashara wakubwa wanafanya uasherati na Babeli, kwa kuwa Babeli unawapa maisha ya anasa na utajiri na kuwawezesha wafanyabiashara hao kuwa watu wakubwa. Babeli unawatimizia watu tamaa zao za mali na ufahari. Ni biashara ya ulimwengu katika vitu vya kifahari wakati watu kwa mamilioni wana shida ya chakula na hivyo kulazimika kujifanyia biashara miili yao, ya watoto wao na nafsi zao (Ufu 17 na 18).
Maangamizi Katika Saa Moja!
Katika muda wa saa moja
utaangamizwa! Je, hili linawezekana? Lakini Bwana ameshatoa maonyo mengi katika
siku za karibuni. Kwa mfano himaya ya Maxwell imeanguka. Mabenki ya Kijapani
yameshindwa. Bidhaa na hisa katika mtandao wa kompyuta hukua na kuporomoka. Je,
unaikumbuka taasisi yenye sifa mbaya iliyojulikana kwa jina la Black
Wednesday (Jumatano Nyeusi) mwaka 1992? Walanguzi wa kimataifa waliharibu
thamani ya pauni ya Uingereza na sarafu nyingine za Ulaya. Wawekezaji wengi,
wakiwemo wachungaji walipoteza katika kipindi cha saa moja tu mamilioni ya pauni
katika Soko la Hisa la London. Uchumi wa nchi kama Korea na Brazili uliporomoka
katika kipindi cha siku chache tu.
Ondokeni Kwake Enyi Watu
Wangu
Haya yalikuwa ni maonyo
tu kutoka mbinguni kwa ajili ya watu wa Mungu ili waitii amri ya Ufu 18:4.
Tunatakiwa kujikabidhi kwa Mungu sisi pamoja na mali zetu, la sivyo tutazipoteza
wakati mfumo wa ulimwengu utakapohukumiwa. Wakristo wanapaswa kuhakikisha kwamba
akiba zao, vitega uchumi vyao na hisa zao ziko katika mikono salama, na si
mahali pasipokuwa salama (Hag 2:6,7) (Yer 51:6,7). Babeli utaanguka.
3. Malaika Wa Tatu
Ujumbe wa malaika wa tatu ni wa kuwaandaa watu wa Mungu ili wasije wakakubaliana na utaratibu wa yule mnyama na pia wasije wakaipokea alama yake ili kwamba waweze kununua; la sivyo wataipokea ghadhabu ya Mungu (Ufu 14:9; 13:11-17).
Huyo Mnyama Ni Nani?
Huyo ni kiongozi ajaye
mwanasiasa mwenye hadhi ya kilimwengu. Atakuwa mwenye nguvu na ushawishi mkubwa
naye ataongoza kwa uwezo wa nguvu za giza zitakazodai kuabudiwa.
Na Hiyo Alama Ni Nini?
Teknolojia ya kuweka
alama tayari ipo katika nchi za Magharibi na inasubiri tu kukubalika na watu
wengi. Kifaa cha elektroniki kitakachowekwa kwenye mkono au kichwani ni wazo
zuri sana la kukabili uhalifu na kuondoa fedha kwenye mzunguko.
Wakristo wanatakiwa kugundua imani katika Mungu kwa ajili ya mahitaji yao (Isa 55) pamoja na kuwa na mtindo wa maisha usiokuwa na tamaa ya vitu yakinifu, Mdo 2:42-47, ili kwamba makubaliano na huyo mnyama yaweze kuepukika. Na hilo lina maana kwamba watu wa Mungu wanapaswa kuwa na subira na uvumilivu ingawa pia baadhi yao wanaweza kupatwa na mateso na hata kifo. Na hilo lina maana vilevile kwamba mtu wa Mungu atatakiwa kufa kila siku kutokana na dhihaka na kutengwa.
Ni Mambo Ya Kukisia Tu, Au
Ni Unabii?
Utayafanyia nini yote
haya? Soma Zekaria 1:4-6 kabla hujajibu.
4. Namna Mbili Za Mavuno Katika Dunia
Uvunaji Wa Kwanza
Utafanywa Na Yesu
Yesu anaamuru uvunaji wa duniani wa watu wa Mungu watakaoishi naye milele (Ufu
14:14-16) (Dan 7:13).
Uvunaji Wa Pili Ni Mauti Ya
Milele
Huu utafanywa na
malaika anayehusika na moto wa hukumu na uharibifu kwa hao wote waliokataa
kumcha Mungu, kumtukuza, na badala yake wakapendelea kuishi katika ufalme wa
Shetani. Ni mavuno ya shinikizo la mvinyo wa hasira ya Mungu ya kutisha (Ufu
14:11, 17-20) (2Pet 3:12).
Sasa tunaelewa umuhimu wa ujumbe wa yule malaika wa kwanza kutoka mbinguni wa kukamilisha Agizo Kuu. Tutahitajiana katika nyakati zinazokuja. Kwa wakati huu tunapaswa kujiwekea hazina zetu mbinguni kwa kuwekeza maisha yetu katika kazi ya Mungu kwa ajili ya waliopotea na walio maskini, tukitumia utajiri wa kidunia kupata marafiki kwa kupeleka injili ya Ufalme kwa kila taifa (Mt 6:20) (Lk 16:9).
Kwa Kumalizia Omba Kwa
Ajili Ya Watu Wa Ulimwengu Huu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili, Ukiwataja Kwa
Majina
Yemen | ||
Jina la watu |
Lugha Yao |
Idadi Yao |
Mahra (Mehri, Mahri) |
Mahri |
294,000 |
Malay |
Malay |
28,000 |
Persian (Irani) |
Farsi, Western |
14,000 |
1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya
for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index to All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk