
1985 - 2007
9. Ponya
Wagonjwa
Mwendee
Yesu unapomhitaji sana
Support Pages
Index To All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
Kwenye Biblia Yako Soma
Zaburi 103 &
Mathayo 8: 1-17
Mstari Wa Kukariri
Yeye mwenyewe
alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti; ili, tukiwa wafu kwa mambo
ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa (1Pet
2:24).
Baadaye Zungumzieni Jambo
Hili
Angalia orodha ya watu
wanaoombea wagonjwa. Je, upo mahali gani katika orodha hiyo?
Je, kinachokuzuia kuhudumu sasa ni nini?
Jambo La Kufanya Kabla
Hatujakutana Tena
Mwombe Mungu akuelekeze
kwa wagonjwa na hakikisha unatii anapokuongoza kukutana na mtu, kumwona au
kumsikiliza, hata kama ni mgeni. Waendee, na hata kama hawataamini lakini bado
unaweza kuwaombea ili waponywe kwa jina la Yesu.
Kazi Ya Kuandika Ya
Stashahada
Kutoka katika vitabu vya
Injili andika orodha ya matukio yote ambapo Yesu alihudumia wagonjwa mbalimbali,
katika mazingira tofauti, na mbinu mbalimbali alizotumia.
Tafakari Mistari Ifuatayo
Neno Kwa Neno
Mdo 14: 8-10
Tumia Dakika Moja Kuubadilisha Ulimwengu
Ombea taifa la Urusi.
Idadi ya watu: 154,000,000.
Baada ya kuanguka kwa Ukomunisti kumejitokeza ugumu wa maisha na uhalifu.
Hakikisha umewafundisha wengine somo hili.
Kila mara
omba na kujiandaa ukiongezea mistari mingine ya Biblia
na mifano yako mwenyewe
ili kufanya somo lieleweke vizuri zaidi.
1. Mimi Ni Bwana Nikuponyaye
Katika Mt 9:35 tunaambiwa kwamba Yesu alipita huko na huko akihubiri, akifundisha na kuponya wagonjwa. Katika Yn 14:12 Yesu anatazamia kwamba kila anayemwamini afanye kazi anazozifanya na kubwa zaidi ya hizo! Paulo aliandika katika Rum 15:19 akisema kwamba yeye aliihubiri Injili kwa ukamilifu, kwa kusema, kutenda na kwa ishara na miujiza.
Yesu anawaamuru wafuasi wake ‘kuponya wagonjwa’ na si kuwaombea tu. Waamini wengi ulimwenguni mwote wanaelezea jinsi Bwana anavyoponya kiroho na kimwili. Anaponya hata ndoa na matatizo ya kifedha kwa sababu lengo lake ni sisi tuwe wazima katika mwili, nafsi na roho.
2. Uponyaji Ni Katika Biblia Yote
Kama ungetumia pini na kutoboa karibu kila ukurasa wa Biblia neno lingechuruzika upendo wa Mungu na uponyaji wake.
Maradhi ni moja tu ya matokeo ya anguko, lakini tangu mwanzo Mungu anaahidi wokovu na neema (Mwa 3:15,21).
Katika Kut 3:7 tunaambiwa kwamba Mungu huona machozi yote na mateso. Yuko tayari kufanya jambo kupitia kwa mtu aliye mtiifu na tayari kutumika.
Katika Kut 15:22-26 Bwana anajidhihirisha kwa mara ya kwanza kama Bwana aponyaye. Anamwonesha Musa kipande cha mti kama picha ya Msalaba. Yatupasa kutupa kipande hicho cha mti katika maji machungu ya maisha yetu ili yabadilike kuwa matamu.
Katika Hes 21:4-9 watu wanang’atwa na nyoka kwa kosa lao wenyewe. Hata hivyo Bwana anawataka waache kuangalia majeraha yao na badala yake watazame juu ili wapate kuishi. Hii ni picha ya Ebr 12:2 ambapo tunatakiwa kuacha kuangalia ugonjwa na badala yake tumwangalie Yesu. Hatuwezi kuangalia sehemu mbili kwa wakati mmoja kama kinyonga. Yatupasa kuchagua; ama tuangalie magonjwa yetu au tuangalie ahadi ya Mungu.
Ayubu alivumilia mateso makali yasiyoelezeka mpaka hatimaye akaponywa na kupokea baraka mara mbili (Ayubu 42).
Daudi anatutahadharisha tusijesahau kuwa moja ya fadhila za Bwana ni kutuponya na magonjwa yetu yote (Zab 103:1-5).
Malaki anasema kwamba Bwana ana uponyaji katika mbawa zake (Mal 4:2).
Yesu Alikuja Kuyafanya
Mapenzi Ya Baba Yake (Ebr 10:9)
Kuna mifano 26 tofauti
inayomwonesha Yesu akiponya watu wenye uhitaji; na hii inatuonesha mapenzi ya
Baba. Angalia somo la 8 Ishara na Miujiza.
Shuhuda tatu za kuaminika sana kwenye Biblia zinathibitisha kwamba Yesu anaponya wagonjwa.
3. Uponyaji Wangu U Wapi?
"Injili yetu ni rahisi, yenye nguvu, inamhusu Kristo na imekamilika milele”.
Je, waweza kuona kwamba neno la Mungu linatuambia kuwa uponyaji wetu ulitimilizwa na Yesu pale msalabani miaka 2000 iliyopita? Pale ndipo tunapotazama kuupata uponyaji wetu; hatuangalii nyakati zijazo. Tunamwona Yesu, tunamwamini na kupokea; tunatoa shukrani kwa imani, na kupumzika, na huku tukiwiwa na Bwana kutenda kazi.
4. Je, Ni Karama Moja Kwa Mmoja Au Nyingi Kwa Wote?
Katika 1 Kor 12:9 tunajifunza kwamba Roho hutoa karama za uponyaji kwa wagonjwa. ‘Karama za uponyaji’ ni maneno yanayoonesha wingi. Hii si karama ya uponyaji ya kutumiwa na mtu mmoja, ingawaje baadhi ya wanaume na wanawake wana imani zaidi na upako zaidi kwa ajili ya huduma ya uponyaji.
Sisi Sote Twaweza Kuwaombea
Wagonjwa
Unaweza ukadhani kwamba
imani yako ni ndogo sana; lakini fahamu kwamba kila mmoja wetu anaweza kuombea
wagonjwa kwa neema ya Mungu tuliyonayo katika wito wetu na ofisi zetu, bila
kutegemea viwango vyetu vya imani.
5. Ni Nani Awezaye Kuombea Wagonjwa?
6. Jinsi Ya Kufanya Huduma Ya Uponyaji
Kwa kuongozwa na Mungu, unaweza kuwahudumia wagonjwa; mahali po pote na wakati wo wote; si lazima kusubiri mpaka wakati wa ibada au katika mikutano ya injili.
Kwa Kumalizia Omba Kwa Ajili Ya Watu Wa
Ulimwengu
Huu Ambao Bado Hawajafikiwa Na Injili; Wataje Kwa Majina
|
Bosnia-Hercegovina |
||
|
Jina la Watu |
Lugha Yao |
Idadi Yao |
|
Rumelian Turk |
Turkish |
50,000 |

1985 - 2007
With many thanks to Pastor Dastan
Mboera, Dar es Salaaam, Tanzania
and EAPTC Nairobi, Kenya
for this revision and translation from the original English.
mboeradsk @ yahoo.com
© Dr Les Norman The DCI Trust, UK
Permission is granted to provide
copies at cost price for study purposes
but not for sale or commercial
purposes. Freely you have received, so please freely give.
Support Pages
Index To All Lessons School of Finances
World Christian News
Who
Are We? Site Index
www.dci.org.uk